Viongozi wa TUCTA wakiimba wimbo wa Mshikamano Uwanja wa Uhuru
Daily News na HabariLeo walikuwepo pia
moja ya mabango ya waandamanaji
mshikamano
umati wa wafanyakazi uwanja wa Uhuru
Wafanyakazi wa kampuni ya Tanzania Distrilleris wakionyesha bidhaa zao wakati wa maadhimisho ya kilele cha sikukuu ya wafanyakazi Duniani iliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, leo yaliyoandaliwa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA). Wafanyakazi walioshiriki maadhimisho sikukuu ya wafanyakazi Duniani mkoa wa Iringa wakiimba wimbo wa wafanyakazi katika uwanja wa Samora mjini Iringa ambako maadhimisho hayo yalifanyika kimkoa. Picha na Francis Godwin. Wafanyakazi katika mkoa wa Iringa wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani iliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Samora huku wakiwa na mabango yenye jumbe mbali mbali.Picha na Francis Godwin.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam William akizungumza na wafanyakazi katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam William Lukuvi (katikati) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani akishiriki kuimba wimbo wa Mshikamano Daima pamoja na viongozi wa vyama vya wafanyakazi ambavyo havishiriki katika mgomo ulioitishwa na Shrikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) .



Wafanyakazi kutoka Mashirika na Taasisi mbalimbali na vyama vya wafanyakazi ambavyo havishiriki katika mgomo ulioitishwa na Shrikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) wakiwa kwenye maadamano kuelekea viwanja vya Mnazi mmoja kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani inayoadhimishwa leo kitaifa jijini Dar es salaam.








Maandamano yakiendelea kuelekea viwanja vya mnazi mmoja
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki za NBC, NMB pamoja na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO) wakiwa wameshikana mikono huku wakiimba wimbo wa “ MSHIKAMANO DAIMA” leo katika viwanja vya Mnazi mmoja kuadhimisha siku ya Kazi Duniani.
Wasanii wa Muziki wa Dansi kutoka katika kundi la Akudo Impact (Vijana wa Masauti) wakitoa burudani leo katika viwanja vya Mnazi mmoja katika maadhimisho ya siku ya Kazi Duniani.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wakiwa wameungana na wafanyakazi kuadhimisha siku ya kazi Duniani iliyofanyika kitaifa leo katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar.
Baadhi ya vijana waliohudhuria sherehe hizo wakicheza kwa furaha ndani ya viwanja vya Mnazi mmoja kuunga mkono maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yanayoadhimishwa leo kitaifa jijini Dar. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2010

    Ankal,
    Hawa ndio wapiga box wanaolipwa vizuuriiiiii sana huko bongo. Tazama walivyo nona kama huyo jamaa aliyeonekana kwenye taswira ya pili akiwa ameinua mikono juu kushiriki kuomba winbo wa solidarity forever. Tazama alisahau hata kuvaa kafulana ndani baba mzima tumbo na kitovu choote njeee! na nikiongozi wa chama bila shaka. mambo ya aibu sana haya kukaa meza kuu pasi na staha

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2010

    Migogoorooo, na migongaanooo, makaazini, ni ukosefu wa nidhamuuuu! Same applies kwa majungu!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 01, 2010

    na wewe ni walewale tu, unatuwekea picha za hao wafanyakazi wachache unaacha kuweka za wafanyakazi wengi wanaopata shida za mishahara midogo na mafao duni kiza wametangaza kugoma. muache siasa kwenye haki za watu! jehanamu inawasubiri. hata usiporusha hii komenti poa tu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 01, 2010

    Hizo taasisi wanalipwa mishahara mikubwa, hata mimi ningewashangaa kama wangejiunga nasi kutaka nyongeza. Hapo ni NBC, NMB, NSSF, DAWSCO nk hakuna walalahoi hapo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 01, 2010

    Ankal hebu tuweke sawa,mi nipo ya Tz. Nimesikia leo kulikuwa na maadhimisho ya aina mbili.Wale waliopo chini ya Tucta maadhimisho yalikuwa uwanja wa Taifa na walio ambao hawapo chini ya Tucta ndio hayo ya Mnazi mmoja.Ni kweli? kama ni kweli utakuwa bias ulitakiwa uweke na yale ya uwanja wa Taifa tulinganishe.

    Bongo tambarare,kweli Tucta noma. Hakuna cha President wala cha waziri wa kazi wala kiongozi yyt toka serikalini.

    Mdau ughaibuni

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 01, 2010

    Leo hutaki kupokea maoni kabisa, sawa... Weka basi na picha za Maadhimisho halisi ya Mei Dei Kitaifa yamefanyikia Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Acha hizo... Ankal

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 01, 2010

    hayo siyo maadhimisho ya ukweli ya MEI MOSI, hizo ni propaganda za kapuya na hao wafanyakazi wasio na shida, utaona matumbo makubwa yasiyo na afya. MEI MOSI ya ukweli kitaifa ilifanyika uwanja wa Uhuru na siyo mnazi mmoja. naona na wewe unapenda propaganda za serikali kudharau wafanyakazi na kuwakebei kwa kutengeneza mei dei yao. hawa NSSF ndo wanapunja mafao ya wastaafu na kujipa mishahara mikubwa watagoma saa ngapi, wanajiona wao ni bora kuliko wanachama wao! kweli nchi hii ubinafsi unashika kasi.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 02, 2010

    Hao ndo utasema wanashida?Wengi wao hapo maumbo yao ni 2 by 1,3 by 1 na 4 by 1. Na ndo maana wameamua kujitenga,hasa hao wafanyakazi wa bank watawasubiri madirishani(Kaunta) wale wote walioenda kushereheka uwanja wa Uhuru.

    Wafanyakazi Tz muda ndo huu msirudi nyuma kuweni na mshikamano hasa katika kudai haki zenu.Msije mkawa kama wahadhiri wa vyuo nao waoga tu, waonyesheni mfano kuwa km mkiungana linawezekana. Kuna gap kubwa sana la kimaisha la mwanasiasa na mfanyakazi wa kawaida hili lipo wazi. Na mwisho na nyie mnawachagua tena hao hao.Mnanikera nyie hata mkielimishwa wapi.Msikubali kuburuzwa.
    Burudikeni na wimbo wa wagosi wa kaya- Maumivu ya miaka kumi.

    Ankal acha kubana comments,hii blogu inakuwa active pale watu wanapochangia usije kubaki pekee yako watakimbia wadau. Ni ushauri tu,ona kama mimi nilivyo comment hakuna hata tusi moja,labda ubane tu.
    Pia acha kuwa bias ww ni mtoto wa mkulima na hao waliokuwapo uwanja wa Uhuru wanakilisha watoto wa wakulima,nionga ingekuwa vyema na wao ungewapa nafasi hapa.

    Mdau

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 02, 2010

    Haya maadhimisho yaliyofanyika Mnazi Mmoja hayakuandaliwa na TUCTA bali FIBUCA ambacho ni chama cha wafanyakazi taasisi za fedha. Maadhimisho yaliyoandaliwa na TUCTA yalifanyika Uwanja wa Uhuru.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 02, 2010

    Jamani nisaidieni, tuwe honest! Hivi hawa jamaa waadhimisha nini?? wanasheherekea kipi?? mafanikio yepi?? furaha yao imetoka wapi??Kweli mazingira ya kazi ni mazuri?? watanzania ni hypocrite tuliopindukia! Shame on us!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 02, 2010

    Bro mithupu acha kuleta siasa kwenye blogu ya jamii, tuwekee picha za uwanja wa uhuru ambazo ni asilimia 95% ya wafanyakazi wote

    Mdau,

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 02, 2010

    Michuzi!
    Umeshindwa kutuhabarisha sawasawa, hizi picha ulizotundika hapa zina kaharufu karushwa ka namna fulani, siamini kama unaweza kuwa cheap kiasi hiki. Kwanini utuwekee maadhimisho ya wanaofadi jasho la wafanyakazi wa nchi hii! NBC, NSSF na mashirka mengine ya pensheni yanawanyonya wachangiaji ambao ni wafanyakazi wengi walioadhimisha sherehe zao pale shambani kwa BIBI, acha hizo, huu si muda wa kujipendekeza bali kufanya maamuzi sahihi kwa ajiliya tanzania bora na si matumbo makubwa

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 02, 2010

    "All the workers of Tanzania unite, there is nothing to lose except your chains"
    Wangejua falsafa ya Mei Mosi basi hayo makundi mawili yasingekuwepo ama hili kundi moja ambalo limeungana na watawala lisingehusika kufanya sherehe, ndiyo maana sherehe za kweli kadiri ya Falsafa ya Max, ni ile ya Uhuru stadium. Waungane sasa dhidi ya tabaka hilo la pili. Solidarity forever!
    Mdau, China.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...