Bw. Kigula (shoto) mwenyekiti wa kwaya ya Kanisa la Kilutheri ya Kijitonyama jijini Dar akikabidhi zawadi kwa Bw. Derick kiongozi wa Kituo cha Kurasini Orphanage
Bw. Edmund Mushi, Mwenyekiti wa Kwaya hiyo akitoa salam za kwaya ya Kanisa la Kilutheri Kijitonyama kwa uongozi wa kituo na watoto walipofanya ziara ya kuwatembelea na kula pamoja na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wa KURASINI ORPHANAGE, na kuwapatia msaada wa vyakula mchele, sukari, unga,mafuta ya kupikia nguo, colgate, sabuni
Kwaya hii inautaratibu kila mwaka kufanya huduma hii ikiwa nipamoja nakwenda kuimba na watoto,
Wanakwaya wakiwa na watoto wa Kurasini Orphanage
Bw. na Bi Muchkuski ambao ni marafiki wa kwaya hiyo toka
Michigan, Marekani, wakisalimia watoto ambapo pia walitoa zawadi ya mipira ya kuchezea na kuahidi kuleta zawadi zaidi
wanakwaya wakiwa na watoto wa kituo hicho
sehemu ya zawadi wanakwaya walipeleka kituoni hapo






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 25, 2010

    Hongereni sana wanakwaya wetu kwa jambo jema mlilochachua. Lakini hivi haiwezekani kuwa na wazo la kuanzisha mradi madhubuti na endelevu ambao utakuwa unawapa yatima hawa riziki yao ya kila siku ?? badala ya kuwa wanapelekewa misaada kwa msimu pasipo na uhakika wa kuipata pindi wanapo hitaji? hebu tulifikirie hili na huenda mungu aliye juu akatenda. na kama yawezekana na iwe kwa vituo mbali mbali

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2010

    Wapi mamaa Joyce Chilolet....!!!! Uimbaji mwema.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 25, 2010

    Wapi mamaaa Alatufisa Maketi...... Nimeimisi sana hii Kwaya.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 25, 2010

    Picha ya tatu huyo mtoto wa kwanza aliyeshikwa hapo amenifanya machozi yatoke...

    Mungu atawabariki tu

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 25, 2010

    duh! hichi kituo kimenikumbusha miaka ya 77 na 78 tulipokuwa tunaenda pale kusoma chekechea. chekechea ilianzishwa ili kuwapa kampani watoto wa pale. one day nitawatembelea hawa watoto.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 25, 2010

    Kwaya ina wenyeviti wangapi? is it Kigula or Mushi?

    Nauliza tu , msinimeze wala kunizozomokea.

    Nakubaliana na mdau pia aliyesema juu ya mradi endelevu na ambao una wa include hawa watoto kuliko hii Faza Kilisimasi ambayo hujui lini yaja, wala ya taipu gani.

    FANTA-KIPAPLI

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 25, 2010

    Kwaya ya Uinjilisti Knyama tunaomba mfanye mpango wa kuingia studio mtoe albam mpya.Mnatuweka sana sisi mashabiki wenu jamani.

    Tunawapongeza kwa kazi nzuri za kijamii mnazofanya pamoja na uimbaji wenu mzuri kila Jumapili.

    Mungu awabariki sana kwa moyo wenu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 25, 2010

    aleluya wanakwaya

    mimi naenda kusaidia watoto wa MAKETE-IRINGA kwakweli na Mungu ansaidie nipate viongozi wasio na uchu wa kutafuna huo mradi maana nataka uwe endelevu kwa taifa hili la baadae

    wanaitaji mapenzi/upendo wetu sana Mungu awalinde malaika hawa

    uwa nalia tu nikiwaona hivi!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 25, 2010

    Wewe FANTA KIPAPLI sikiliza majibu yako. Kwaya ina Wenyeviti wawili kwa maana ya Mwenyekiti mkuu na mwenyekiti msaidizi. Imetokea bahati mbaya tu mwandishi wa habari hii hakutabanaisha. Halafu wewe inaonekana ulikuwa ama ni mwanakwya wa hii kwaya mana kulikuwa na Uniform yaitwa KIPAPLI PAPLI. Nagira A Town.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 25, 2010

    mchangiaji wa mwisho kabla yangu... anajaziba ama na yeye ni mwanakwaya hivyo anacho anachokijua huyu...ndo maana kaaongelea suala la uniform...

    mzee wa kuweka kapuni haya na hii tena weka

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 25, 2010

    sawa hata hivyo wamechoka mbaya siku hizi

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 26, 2010

    Mshamba wa Nagira sijui kitu gani, sijawahi hata kuwa Mwanakwaya hapo, nimeuliza tu ili kujua maana hiyo bahati mbaya mi ningeijuaje? kwani nalala kitanda kimoja na Ankal au mwandishi hadi nijue?

    Kuhusu ya Yuniform, utajibeba mwenyewe, mi hata habari sina . Maana mbona hapo hawajavaa? Wakati mitoko kama hiyo ndo wangevaa kuonesha ni kundi moja lenye kunia mamoja! au hadi waitwe kwenye matamasha?
    Au wanaona kuwavalia Yuniform hao watoto ni kama haistahili?

    Na kama uko Nagira haya ya Kijito yanakuhuuuu?




    halo!

    SPRITE-KIPAPLI

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 26, 2010

    Huyo mama aliyeshika mtoto hapo mbele amemshika akudhihirisha kuwa si wake wala hana upendo naye. Hebu jamani angalia, hata hajamfunika tumbo la mtoto, na kutengeneza gauni lake vizuri kama kawaida ya upakataji mtoto. Mtoto ukimpakata unamtengeneza nguo zake zilizovulugika wakati ukimnyanyua. Nina wasi wasi watu wengine huwa wanaenda vituoni kijionyesha tu. Hizo zawadi wapewe walengwa sio wengine kuzikodolea macho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...