Dk. Karl Peters (kati) akiwa na wenzake Dk. Karl Juhlke na Joachim Graf. Huyu Dk. Karl Peters ndiye aliyewaingiza mkenge babu zetu wakati wa kuingia ukoloni wa Ujerumani nchini kwa kuingia katika mikataba ya kilaghai na watawala wetu wa jadi
Mbwela, Chifu wa Wazigua mkoani Tanga, ndiye aliyekuwa mtawala wa jadi wa kwanza kutia saini mkataba na Dk. Karl Peters mwaka 1884.

Haya na mengi mengineyo yanayohusu historia ya nchi hii yanapatikana katika Makumbusho ya Taifa jijini Dar ambako kwa sasa ukarabati wake unakaribia tamati ili kuifanya sehemu hiyo isiwe tu ya makumbusho bali sehemu ya kukutania wadau wakubwa kwa watoto, wake kwa waume kwa shughuli mbalimbali ikiwemo utamaduni, sanaa na mengineyo.

Makumbusho hiyo ya Dar (katikati ya jiji karibu na IFM na sio Kijiji cha Makumbusho Kijitonyama kama ambavyo wengi wamezoea kuchanganya) hivi sasa inajulikana kama Makumbusho na Jumba la Utamaduni - Museum and House of Culture.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

 1. AnonymousJune 13, 2010

  mimi nilizani watanga ni wajanja kumbe sikuizi tu ndo Wanajifanya wajuaji. kumbe ki historia ni wajinga tu.huyu babu wa kitanga ndo aliyewauza waynga wenzake na yeye mwenyewe!!

  ReplyDelete
 2. AnonymousJune 13, 2010

  Mimi naomba msiwalaumu machifu wetu kuwa waliingia mkataba wa kilaghai na Wajerumani.

  Mkumbuke kuwa kipindi hicho mababu zetu walikuwa hawana elimu hata ya darasa la kwanza na kina Dk.Karl Peters walikuwa ni wasomi waliobobea(Madokta).Hasa hapo unategemea nini kwa mtu asiye na ufahamu kufanya dili na Dk lazima akubali tu matakwa ya huyo dokta.Hata ungekuwa wewe ungeingia tu kwenye huo mkenge.

  Tusiwaite wajinga bali tuwalaumu viongozi wetu wa sasa ambao ni wasomi na wanaoingiza nchi yetu TZ katika mikataba mibovu kama TRL,madini(Buzwagi),Richmond nk.

  Nicholas-Netherlands

  ReplyDelete
 3. Mzee wa KidukuJune 13, 2010

  Kina Karl Peters bado wapo hapo Barrick Gold na kwingineko migodini.

  Na kina Chifu Mbwela na Chifu Mangungo wako hapo Ikulu wakiendelea kusaini mikataba ya kilaghai especially kuhusu madini yetu.

  Na mwisho kabisa hapo zamani Chifu alikuwa hachaguliwi bali anarithi toka kwa baba yake.

  Sasa ukiwa kama mpiga kura jiulize uwepo wa kina Chifu Mbwela na Chifu Mangungo hapo Ikulu unasema nini kuhusu wewe mpiga kura ambaye umewaweka hapo?

  ReplyDelete
 4. AnonymousJune 13, 2010

  Duuuh kumbe ufisadi tumeuanza mapema,Watanga na ujanja wao kumbe ndo waloanzisha UFISADI.

  ReplyDelete
 5. HUU NI UTHIBITISHO KUWA MAKIMA(MONKEY)NI LAZIMA WATAWALIWE NDIO MAMBO YAENDE.

  NIKO TAYARI KUTAWALIWA NA WAZUNGU KULIKO KUONGOZWA NA MAKIMA WANAOJALI MATUMBO YAO .

  AFRIKA HATUNA UWEZO WA KUJITAWALA.USHAHIDI NI HUU WA BAJETI ZETU

  UMEONA WAPI ETI SERIKALI INAPANGAGA MATUMIZI YAKE THEN PESA ATOWE MZUNGU !!!  HAHAHAHAHAHA.

  HONGERA UKOLONI!

  ReplyDelete
 6. AnonymousJune 13, 2010

  Hiyo mikataba ya ulaghai unayoongelea mbona ipo mpaka leo miaka 126 tangu ilipoanza 1884? Hii ni kasumba ya waafrika na miafrika ndivyo tulivyo. Na bado tutaliwa mpaka mwisho wa dunia kama hatutaki kubadilika.

  ReplyDelete
 7. AnonymousJune 13, 2010

  Hivi mikataba ya wakati ule ilikuwa imeandikwa kwa lugha gani? Je wakati wanajadili hiyo mikataba walikuwa wanatumia lugha gani? Naomba msaada kwenye tuta wadau

  ReplyDelete
 8. AnonymousJune 13, 2010

  hivi hawa ma-dokta wa kizungu waliweza vipi kuwasiliana na hawa machifu, manake najua hata watafsiri hawakuwepo kipindi hicho, nampa shavu mdau aliyesema tuwalaumu viongozi wa saivi, pamoja na uelewa wao lakini tamaa wameziweka mbele ya uzalendo na kujali mfuko binafsi, hii ni dhambi na aibu hata kwetu kuwa na viongozi hao. Mtu unaweza kujikuta unatoa maneno hata yasiyofaa kwa viongozi wanaoiuza nchi kama viongozi wetu hawa wa saivi.

  ReplyDelete
 9. AnonymousJune 13, 2010

  hawa watu waliwasiliana kwa kutumia lugha gani? je upande upi uliijua lugha ya mwenzie? miaka ya 1889 sidhani kama walisainishwa mikataba huku wakielewa, bali waliweka madole gumba(nadhani) basi na wao kupewa viofa kidogo kwa familia zao ikawa imetoka
  Mdau Bradford

  ReplyDelete
 10. Tuachane na kuwalaumu watu waliotangulia mbele ya haki.Hawakuwa na maarifa tuliyonayo sasa.We mwenzangu saa hii,mathalani uchaguzi ujao utachagua watu makini au utatumia mazoea.

  Ankal na wadau wote salam toka stockholm,sweden hapa wao wanaita summer lakini temp ni 10c.

  Tuache hayo,jana mwenyeji wangu amenipeleka National Museum hapa Stockholm.Nimejionea wenzetu wanavyohifadi jadi zao.Kuna kumbukumbu za vitu vilivyotumika toka mwaka 1452.

  Pia nimeona mashua yao ilyozama mwaka 1670 wakaiibua mwaka 1960 kila kitu wamejaribu kukirudisha kama kilivyokuwa.Ni mambo ya kustaajabisha sana.Naweza watumia picha mkitaka.

  frederick.sangawe@gmail.com

  ReplyDelete
 11. AnonymousJune 13, 2010

  Lo!, taabu kweli! kufikiri kumbe ni kugumu sana! Yaani huyu ndugu yetu mtoa maoni wa kwanza hapo juu amejieleza mwenyewe jinsi alivyo na ufinyu wa kufikiri. kumtukana Chifu Mbwela kwa kile alichofanya, ni kumkosea adabu yeye na wenzetu wa Tanga kama alivyoandika. Mtoa maoni kwa ujinga wake hakufahamu kuwa Karl Peter alikuwa tapeli au laghai. Matapeli kama Karl Peter wapo hata siku hizi kati yetu. Unamwamini mtu kwa mambo anayosema kumbe unatapeliwa.Watanzania wangapi tumeshalizwa kwa utapeli wa aina mbalimbali hapa Tanzania? Machifu wetu walitapeliwa na Karl Peter. Walisaini mkataba na karl Peter wakiamini kuwa wangefaidia jamii zao kutokana na ahadi alizotoa Karl Peter. Bahati mbayo karl Peter hakuwa mkweli. Ndiyo maana ikaitwa MIKATABA YA ULAGHAI AU UDANGANYIFU na kwa lugha ya sasa ni MIKATABA YA KITAPELI. Mwisho Namwalika mtoa maoni wa kwanza achunguze mikataba mingapi ambayo serikali yetu ilisaini na wawekezaji bila kujua kuwa wanaiingiza mkenge nchi yetu ambapo mikataba mingi ya uwekezaji imezua tu taabu na karaha nyingi kwa watanzania. Na ndivyo ilivyokuwa wakati wa wazee wetu akina Mbwela. Hawakuwa wajinga ila walitapeliwa.

  Mdau, Kihonda.

  ReplyDelete
 12. AnonymousJune 13, 2010

  afadhali hawa wazee waliingia mikataba na wasomi wazungu viongozi wa sasa wanaingizwa mikataba na wahindi kama kina manji,na chavda

  ReplyDelete
 13. AnonymousJune 13, 2010

  Nakuunga mkono bwana Nicholas-Netherlands. Hiyo mikataba iliyosainiwa na mababu zetu ilikuwa tu wametia dole gumba lakini hata wangekataa kutia dole gumba wangelazimishwa. Kwani hata wangekataa kutia dole gumba,wangetumia njia nyingine kuwawezesha kusaini mikataba.

  Kwa sasa hivi watu wanaelimu lakini bado twadanganyika sijui kwa nini? wewe angalia lile dude lilonunuliwa toka UK, aircraft control wataalamu wanaita. Hivi ni kipofu gani aliamua kununua? halafu inabidi tuangalie sana huu uwekezaji wa kampuni toka nje siku twaweza kujikuta wote watumwa.

  Mkulima wa Lupalilo Iringa

  ReplyDelete
 14. AnonymousJune 13, 2010

  ni bora walivyoingizwa mkenge ungekuta hadi leo tuko zama za mawe habari ndo hiyo

  ReplyDelete
 15. AnonymousJune 13, 2010

  Tarehe Sun Jun 13, 09:55:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
  umeonge point ndugu yangu !! viongozi wa sasa ni bomu kabisa. mimi naona boa mkoloni ange tutawala tu adi sasa

  ReplyDelete
 16. AnonymousJune 13, 2010

  Susi na Chuma

  ReplyDelete
 17. ADILI NA NDUGUZEJune 13, 2010

  Michuzi mbona mchango wangu juu ya mlima Kilimanjaro hujauchapisha kwenye hii blog ndugu yangu. Tangu wiki iliyopita. Ilikuwa response yangu kwa Dr Hildebrand Shayo.

  ReplyDelete
 18. AnonymousJune 13, 2010

  Shida wawekezaji washatujua kuwa sie Watanzania ni 'vipofu', hivyo wakila nasi hawatushiki mkono! Ni mpaka watokee wazawa wa ukweli ukweli ndio 'dili' linashitukiwa. Billioni 10 na Trillioni 10, wapi na wapi?

  Vinginevyo hii inji ilishauzwa siku nyingi, kwa maana ya kwamba, uki-compare assets zake vs. Liabilities ilizonazo, the deficit / difference is enormous.

  La kusikitisha zaidi wazawa wanatupiliwa mbali na miti yao kama jongoo, preference wanapewa Brazil, na hasara juu yake!

  Kaazi Kweli Kweli!

  ReplyDelete
 19. AnonymousJune 13, 2010

  Kwa kweli watu weusi Mungu na atusaidie. Hivi unajua bila wazungu inakuwa hard kwetu kuendelea. we hebu angalia South Africa, hivi kusingekuwa na weupe ile nchi leo kungekuwa na WORLD CUP AFRICA??? Angalia Zimbabwe, kama wasingewafukuza wazungu leo ingekuwa mbali, lakini tangu Mugabe aingiwe na mashetani yake na kuwatimua wazungu sasa nchi iko ground ZERO. Jamani hivi wazungu wana nini ambacho weusi hatuna mpaka mahali wakiwepo ndio maendeleo yanakuja, mi nimeshajiuliza sana hili swali, sijui jibu.....yaani naona km inawezekana hata Tanzania labda tumrudishe muingereza au mmarekani atawale kwa muda walete mabadiliko especially barabara, otherwise I don see a lot of changes in the next 5 yrs, eeeh MUNGU UTUREHEMU WEUSI

  ReplyDelete
 20. AnonymousJune 13, 2010

  NDUGU ZANGU HAKIKA MMENENA YA KWELI MIMI KWA KIFUPI TU WAKATI WA UKOLONI TANGANYIKA ILIKUWA IKEPELEKA PESA UNINGEREZA KAMA 60% YA PATO LA NCHI NA 40% NDIO TUNAONA MAENDELEO YALIYOLETWA NA WAKOLONI BARABARA, TRAIN, NATIONAL HOUSING, MAHOSPITAL, MASHULE KARINU YOTE YALIJENGWA NA WAKOLONI HADI MAGOMENI YOTE NA HII NI 40% AMA LEO 100% HATA BAJETI YA NCHI HAITOSHI BAJETI YA NCHI INACHANGIWA NA WAKOLONI 40%. HAPA INAJULISHA KUWA MWAFRIKA YEYE NI KULA TU HAKUNA KUENDELEZA NCHI IKIANGALIA HAMNA HATA KITU KIMUJO KIMEFANYWA ZAIDI YA MANENO MATUMPU MIAKA 60 KARIBU YA UHURU KILA KITU WAFADHILI HAKIKA NI BORA KUTAWALIWA NA WAZUNGU TUNGALIKUWA MBALI SANA KIMAISHA AMA MWAFRIKA NI KULA VINGOZI NA KUJIPA VYEO YAANI NI USULTANI WA KIJANJA KWA KUTUMIA RANGI KUWA MWEUSI MUNGU TUBARIKI TUPENDANE

  ReplyDelete
 21. AnonymousJune 13, 2010

  Alitiaje saini wakati hakujua kusoma wala kuandika? Walimtapeli..wakampa peremende....!!

  ReplyDelete
 22. AnonymousJune 13, 2010

  big up kwa sana mdau hapo juu, halafu tukiwasifia wazungu wapo juu watu wanakuja juu kama vile kuna injiania yeyote bongo amewahi kuvumua kitu. wazungu wadumu bila wao tusingeendesha magari, ndege, meli yani ni wavumbuzi wakila kitu, barabara za ukweli si tunaona huku kwaoo mambo ya ajabu acha kabisa mzungu yuko mbali saaaaaaaanaaana. nakubaliana na mdau mmoja kuwa south africa isingekuwa hapo ilipo leo, kama na wao wangepata uhuru mwaka 61 kama kina sie wangekuwa ovyo tuu, hata zimbabwe ni pazuri sana sema tuu lile jongo lao ni korofi linaaribu nchi. natamani tungepata uhuru mwaka 2000 hata ufisadi usingekuwepo. viongozi wa africa wamezoea umimi sana ni wezi tamaa kwa sana wanakomba bila huruma hayo maendeleo yatatoka wapi?? kila kitu msaada hadi vyandarua , jamani si kuna viwanda?? mie nadhani wazungu wana ubongo wa akili extra si bure, wako smart sana wanaona kuleeeeeeee.

  ReplyDelete
 23. AnonymousJune 13, 2010

  kweli nakubaliana nabaadhi ya wadaumimi siku zote nasema ingebinafsishwa kila kitu mpaka ikulu bora wazungu watawale kuliko hawa wasikuwa nahuruma na binadamu wenziye wananyonya hadi damu ngoja tu iko siku kilio chawatanzania kitasikika na wasifikiri watatawala milele kilicho na mwanzo hakikosi kuwa na mwisho wao wanaona wako juu lakini kuna siku ambayo haina jina wataachia ngazi watanzania wanateseka wamekuwa km yatima wasikuwa na mtetezi wengine watesa km wapo peponi na wengi wanaishi maisha ya kubuni hawajuii kesho itakuwaje wakilalamika hakuna wakuwasikiliza acha tu nina uchungu sana tz

  ReplyDelete
 24. AnonymousJune 14, 2010

  Karl Peters ndiyo Baba wa Taifa wa kikwelii.

  Hakuna mkataba wa kitapeli au sijui nini. Mikataba inaweza kuwa aitha halali au batili kutokana na vigezo thabiti vya kisheria - Full Stop. Anayekuambia kuna mkataba feki, mkataba wa kitapeli, mkataba mbovu, ni mtu asiyejua mambo yanavyoenda.

  Hata wewe leo ukienda kununua shamba kwa mwanakijiji pale Arumeru, halafu ukapaendeleza, ukajenga hoteli la kisasa, baada ya mwaka utasikia - oh, huyu alimtapeli mwanakijiji kiwanja kwa shin laki moja tu..."

  Shukuruni kazi ya Karl Peters kuzunguka nchi nzima na kuinguanisha iwe kitu ambacho leo mnajifanya mna uchungu nacho sana. Kwani kabla yake kulikua kuna hata wilaya hapa, sembuse taifa.

  Kila mchangiaji hapa kwa namna moja au nyingine amekuwa akisema Karl Peters ni shetani. Hii hali inasema mengi sana kuhusiana na Education System yetu baada ya Uhuru. Elimu imekaa kisiasa mno kiasi kwamba imetengeneza taifa la Wananchi mazumbukuku, wasioweza kuchanbua hata matokeo muhimu ya kihistoria - hata jinsi taifa lilivyoundwa. Elimu ya namna hii haitaweza kulitoa hili taifa na tutabakia kuwa mabuingwa wa kuita watu mafisadi, kuita mikata kuwa ni hewa, kushutumu wawekezaji kuwa ni makaburu na wanyanyasaji.

  ReplyDelete
 25. AnonymousJune 14, 2010

  bora mangungo asiyesoma na asiye na historia ya kujifunzia kuliko mangungo wetu waliosoma na wenye historia ya akina mangungo halafu wanarudi umangungoni.

  ReplyDelete
 26. AnonymousJune 14, 2010

  Michu, nahisi huyu chief Mbwela ana unasaba na Williams- baba yao Venus na Serena... Kama watahitaji kuchimba asili yao; ningeshauri waanzie uziguani.

  ReplyDelete
 27. AnonymousJune 14, 2010

  Lawyers where are you? Doesnt this qualified for "not my deed"? What language did Karl Peters use in that contract? One can be sure that if we decide to make a claims on specific items in colonialism we can have at least 1/8 of what has been taken.

  ReplyDelete
 28. AnonymousJune 14, 2010

  tutamlaumu bure mbwela inawezekana wagerman walimwaidi kuwa watajenga shule,reli pamoja na kuleta maendeleo...lakini pia inawezekana wagerman wametimiza yaliyomo kwenye mkataba kwani si tumeona wamejenga reli,wamejenga bandari ya tanga,tanga tech iyo shule....hivi ukiacha shule zilizojengwa na wajeruman katka nchi hii kuna awamu yoyote iliyofikia kujenga shule zaidi ya zilizoachwa na wajeruma...sometime ni bora jamaa wangeendelea kutupa adabu tu..mnang'ang'ania kujitawala mmpewa nchi hamna kipya mlichofanya zaid ya kuharibu mliyaoyakuta....nyerere aling'oa baadhi ya reli katika baadhi ya mikoa cjui alikuwa anafikiria nn yule mzee....ni bora wajerumani waliijenga nchi shule zote kubwa walizijenga wao..jangwani,azania,tambaza na nyngne karibu zote ukiacha ben mkapa sec. sasa c afadhali chifu mbwela aliingia mkataba na wa2 wa maana angalia mikataba tuliingia sasa ivi jamaa wanavuna dhahabu,gesi hawajajenga hata darasa ktk nchi hii..tuamke bora tuwe kama mbwela kuliko kuwa kama chenge mwanasheria wetu

  ReplyDelete
 29. AnonymousJune 14, 2010

  WAJERUMANI WAMECHANGIA MAENDELEO YETU KULIKO TAIFA LOLOTE DUNIANI ZAMA HIZO.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...