-------------------------------
Ankal hongera kwa kazi ya kutukumbusha kule tulikotoka, miye hiyo picha ya embe imenikumbusha mbali sana miaka ya Sabini wakati huo nikiwa shule ya msingi iliyokuwa ikijulikana kama Kisarawe Primary School hapo Kidongo Chekundu maarufu kama Gerezani, basi wakati wa Half time ( mapumziko) kengele ikigonga tu tuna toka mkuku tunakimbilia kulikuwa na Mti Mkubwa hapo kulikuwa na Babu Omar akituuzia mihogo ya kukaanga na pilipili, embe kwa pilipili, mabungo kwa pilipili, ice cream tu hazikuwa na pilipili, yalikuwa maisha ya raha kweli enzi hizo. Hapo sijataja ubuyu na visheti...Acha!
Mdau New New York.
Hahahaha jamani vibaya hivyooooo...natamani niruke bongo sasa kwa utamo wa hilo embe..
ReplyDeleteDah mate tele mdomoni yani kitambo, Yani umefanya nikumbuke na Mabungo... Home is the best place ever!!!
ReplyDeleteSISEMI
ReplyDeleteUtamu mpaka kisogoni....manake ugwadu unachanganika na utamu kwa pilipili kiaina...Oh lord have mercy!!
ReplyDeleteHivi mabungo yanaitwaje kizungu?
meno jamani meno yameshaanza kuuma.
ReplyDeleteUncle usiweke picha kama hizi tunakumbuka mbali.enzi za school ukinunua hilo kila mtu naombaaaaaa naombaaaaa.ukigawa ulitahamaki umebakia na kokwa haaaaahaa
ReplyDeleteHoneypie
ha ha ha! watu wengine! wewe hapo juu unayetamani uende bongo kwa utamu wa ilo embe. umelionja? umejuaje kama tamu kama chachu je? we utakuwa na mimba changa wewew
ReplyDeleteyaani jamani nimeyatamani lo , unanikumbusha na maembe ng'ong'o na makungu. home sweet home asikwambie mtu
ReplyDeleteDuu! Kaka Michu unaniua mdogo wako. Maembe ya UK wala jamani natamani kupaa. Nakumbuka enzi hizo primary shilingi 5, lilivyokatwakata unagawa vipisi kwa wenzio na kushtukia umebakiwa na kokwa.
ReplyDeleteMimba zitatoka duh Kweli Mabungo kwa Kiengereza yanaitwaje sio Kwa kizungu kwa Kiengereza wekeni Topic ilitujue au ni "M" BUNGOZ.
ReplyDeletehayo bwana kama una mimba changa ndo penyewe, manake ukiyaona tuu mate yanajaa mdomoni, jamani kwa kweli huwa yana utamu flani ugwadu, utamu, kipilipili, chumvi basi mmmh
ReplyDeleteWankumbusha Tanga miye yakheee, nilikuwa babu muuza anapita na tenga kwenye baiskeli mitaabya raskazone akiimba "maeeeemb eembeee, maembeee" au siku zingine anapita na samaki utasikia "samaki bongebonge" lol beutiful memories.
ReplyDeleteMdau Uswidi
Jamani haya maembe ndio yalikuwa yanasabisha kipindupindu.
ReplyDeleteEmbe Tanga hizo, zina kaharufu fulani hivi natural. Ila pale Tanga mjini kuna wale ngedere walikuwa wanaziharibu sana maeneo ya mkwakwani, nakumbuka hiyo ilikuwa 1994 nilipokuwa pale hostel ya Eukernford avenue, Uhuru park hostel, nakula kitabu cha PCM Usagarani. Ila watoto wa kitanga walinifanya nifikirie kuishi Tanga japo toka nimalize shule nirudi mara moja tu kuchukua cheti changu.
ReplyDeleteJamani nyie watu mbona hivi. Mwanifanya mate yanitoke ati?
ReplyDeleteWadau wa Mlimani Pr. School mwamkumbuka Mzee Mombasa na Kassim muuza mihogo? Good gone old days!!
ReplyDeletehahaha wa msimbazi mseto tulikuwa na mzee wasiwasi!!!.
ReplyDelete