Anko wa libeneke naomba uwafikishie watanzania mambo mema!
"Timu nzima ya AfroIT imekamilisha hatua ya pili ya AfroIt ambayo imesheheni kwenye kila kona ya ICT ndani ya muonekano mpya wa kuvutia huku ikimuwezesha mtumiaji kupata kila kitu kwa pamoja.Usipitwe kwa kutembelea AfroIT kama unahitaji kudownload vitabu vya ICT,kujadiliana matatizo ya ICT,blogs za ICT.kuangalia video za ICT,kusikiliza Podcast za ICT na mengineyo mengi.
http://www.afroit.com
Walenga walisema "Azabu ya kaburi aijuaye maiti". AfroIT ikiwa ni mtandao wa Watanzania unaelewa kwa undani nini Watanzania tunahitaji hivyo hufikisha Elimu sahihi kwa watu sahihi ndani ya muda sahihi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2010

    EBU KWANZA KIDOGO MDAU.....HIYO AZABU YA KABURI APO INAINGIAJE?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 29, 2010

    Hawa AfroIT.com wanasambaza wizi wa kazi za watu wengine (haki miliki/copyright infringement), pirates wa materials zilizotengenezwa kama biashara, wao wanasema wameziokota na wanawapa watanzania mali za wizi. Hamna hata kitu kimoja wao, wanaICT hawa wa AfroIT wamekitengeneza na kukiweka katika kiota chao, bali, wapo macho juu juu kutafuta mali za watu na kuziweka kwenye site yao.

    Nasema tena, hatutaki vitu vya wizi!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2010

    shida yako ni nini?hata UK kuna website kibao wanatoa material free.Sioni tatizo lolote kwa afroit.Sisi watanzania tunalalamika sana ,badala ya kufurahia ni kupiga majungu.

    Mimi imenisaidi sana hii afroit,Chuo kikuu chetu ukiingia bado wanatumia vitabu vya zamani.leo

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 29, 2010

    Usipoteze watu kijana,AfroIT ni mkombozi wetu,pia tatizo umeshaoshwa na sera za kubepari wewe.Binafsi nimefaidika sana na AfroIT.Kule kuna watu waliobobea na moyo wa kuwasaidia watu,kama huna la kusema bora ulala.Youtube hausemi ila kwakuwa hii AfroIT ni ya watanzania ndio unafungua mdomo.
    Nakushauri tembelea website nzima halafu ndio uje kutoa maddongo.

    Mdau-Leads

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 30, 2010

    Sio kuwa nina shida, nahoji hiyo position kuwa wanawasaidia watanzania bila kuweka uwazi kuwa hii "mali" ni ya wizi. Ningekuwa na shida ningekuwa hospitali. Sito furahia uhalamia wa aina yoyote, sidhani kwa hilo nitapungukiwa kuwa mtanzania.
    Kama umefaidika basi, jitolee na'wewe utengeneze hicho kitabu, hizo lessons halafu uwakabidhi hawa afroIT waziunganishe kwenye jalala lao. Ninasubiri hiyo kutoka kwako...
    Sasa lawama ya chuo chako kuwa backwards basi inakupa go-ahead ya kuwa mwizi....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...