Mzee wa Nondozzz Makulilo jr na mai waifu
wake baada ya kula nondo yake karibuni
MAKULILO SCHOLARSHIP BLOG
INAADHIMISHA MIAKA 3.
BLOG ilianza kufanya kazi rasmi kuanzia JULY 2008. Mwezi huu JULY 2010 ni mwezi wa maadhimisho. Nipo katika hatua za mwisho za maboresho ya BLOG hii ambapo nitaongeza kipengele cha SCHOLARSHIP AUDIOS/VIDEOS ambapo nitakua najibu maswali ya wadau na kuweka dondoo za maandalizi ya mtu kuweza kupata scholarships North America na Western Europe.

Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadau wote ambao wamekuwa katika mstari wa mbele kunisaidia katika mambo ya BLOG hususani MICHUZI (WWW.ISSAMICHUZI.BLOGSPOT.COM) na DA SUBI (WWW.WAVUTI.COM) . Pia nawashukuru wale wote walionisaidia kuweza kuongea ktk ITV, TBC1 na TBC TAIFA kuhakikisha watu wengi wanajua taratibu za uombaji scholarships ughaibuni.

Naomba maoni yenu katika kuwezesha maboresho ya BLOG hii. Pia natoa wito kwa wengi kujiunga na SCHOLARSHIP FORUM WWW.SCHOLARSHIPNETWORK.NING.COM

ambapo unatakiwa ku-SIGN UP na kuwa member. Mara uwapo member utakuwa unapata scholarship updates kwenye E-MAIL INBOX yako kila ninapoweka taarifa kwenye FORUM na utakuwa na nafasi ya kuweka comment au kuuliza swali na kujibiwa papo hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 15, 2010

    Hongera Mdau Makulilo na my wife wako. Nilipata bahati ya kukusikiliza/kukuona kwenye ITV ulipofanya interview yako ya nguvu. Naamini ukiweka interview ile kwenye youtube na blog yako itakua njema sana. Nakushauri ushirikiane na magazeti ya hapa nyumbani uwe unatoa articles za scholarships walau kwa wiki mara moja ili watu wengi wapate info hizo.

    Unachokifanya hujui impact yake. Unasaidia watu wengi mno, na unapunguza uzandiki uliokuwepo na wizi/rushwa kwa wanaojiita maajenti wa vyuo na wizarani.

    Mungu akuzidishie upendo wako, na uendeleze libeneke jema.

    Hongera kwa master's degree yako. Unaongoza kwa mfano, wewe mwenyewe umepata scholarships na unasaidia wengine nao wapate scholarships.

    Mdau wa nondoziiiiiii

    Political Science, UDSM, 2009

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 15, 2010

    makulilo hongera sana kwa kupata masters lakini kaka naona hypertension inakusogelea jaribu kula sana mboga za majani acha mapochopocho bado tunapenda kukuona ukitupa news za ulaya.

    mdau, bongo

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 16, 2010

    hongera sana kwa ku graduate na pia kutuhabarisha kuhusu scholarship
    may God bless you.
    Mdau USA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...