Kwako dada Subi.
Hii clip inatia machozi. Mimi si tajiri lakini nataka kusaidia, lakini sijui nisaidieje? hasa yule mtoto alibakwa na boss wake kule musoma na akazaa mtoto. Niliona jina lake ni Neema na yule biti mdogo ambaye wazazi wake waliachana na mama yake kurudi Rwanda, nakumbuka jina lake ni christina.

Je unaweza kuongea na yule dada msimuliaji akapendakeza ni nini la kufanya kuhusu hawa watoto. Je shule itawafaa na wale wakubwa kidogo wakipatiwa mitaji je wanaweza kujikomboa kwa biashara? inatia huruma sana Mshahara eti shilling 6000 kwa mwezi. huzuni sana.

pendekezo langu kwa wizara ya ustawi wa jamii na watoto ni kwamba mtu yoyote anayetaka kwenda vijijini kuchukua watoto wa kazi ingekuwa vizuri kama angepatiwa kibali cha wizara na kujulikana kabisa kwamba atamlipa huyo mtoto na kwamba anatabia nzuri na si mtu ambaye anaweza kumwa-buse mtoto.

Huku ulaya wanafanya hivyo, mtu ni lazima apate kibali cha wizara husika na awe hana historia ya kudhuru watoto ndiyo anapewa hata mtoto wa kumsaidia iwe kumsomesha au kumulea.
Yangu ni hayo tu.
Mwakipesile

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. MUNGU WANGU UWASAIDIE HAWA WATOTO KATIKA JINA LA YESU...SIAMINI KAMA TUNA SERIKALI INAYOANGALIA WATU WAKE NA KUWAJALI,SIJUI NISEME NINI ILA HAO WAAJIRI WA NDANI NA SERIKALI WOTE WANA DHAMBI.

    ReplyDelete
  2. This video is of nothing surprising or new in Tanzania.This is just a tip on the ice.Such activities are well known and practiced by mostly all, more or less the very people who are in the top positions of the hierarchical ladder in tanzanian government. For a long time everyone seem to turn a blind eye on this, but as one of the girls put in her narrations soon or later such atrocities will reciprocate to the one who commit them. The solution here is to form some sort of organisation helping nanies and house workers. The government should also be sincere and commit itself to help solving this problem. A question here is- what will those who benefit from misery of these children do without them? visit a ministers home you will find one,two or more of such house workers

    ReplyDelete
  3. Hawa ni watumwa tuu. Inasikitisha kuona kwamba utumwa unaruhusiwa Tanzania kwa kupewa majina kama "house girl, au msichana wangu wa kazi".
    Ukitaka kuamini kama huu ni utumwa, jiulize watu wangapi wenye hao "wasichana wa kazi" wangekubali watoto wao wa kike wakaajiriwe kama "wasichana wa kazi".
    Kama kawaida yetu, Wauza samaki, oooops...., meant to say "waselfish"...., kama anayetumikishwa siyo wako wa damu, basi wala haikuhusu.

    ReplyDelete
  4. Mmmh....waajiri nafikiri hata wengine mpo hapa mnaangalia..badilikeni, mkuki kwa nguruwe mtamu kwa binadamu...Ole wao

    ReplyDelete
  5. nchi yenye amani ndio hii????? usiusemee moyo. pole sana dada mpo wengi mnaolalishwa sehemu moja na mifugo.pole dada..

    ReplyDelete
  6. i love these kids..wanastahili kila upendo kama watoto wengine.mungu wabariki sana na waongoze katika njia salama.

    ReplyDelete
  7. Sisi wadau tufanye mpango wa kuwasaidia hawa na sio kutegemea serikali,nafikiri kuna haja ya kuwa na House Girls Safe Heaven Tanzania Foundation(HGSHTF)na hapo tunawezakutuma misaada na kuchangisha kila mwezi,mfano mzuri mama Theresa wa kalkata alikuwa anapokea watoto wanao tupwa na wazazi wao kwa pamoja tunaweza kwa hiyo tuache maneno na tuanze vitendo,inasikitisha sana na kuumiza huu sio ubinadamu kabisa.2010 bado tuna slave jamani??damm so sad

    ReplyDelete
  8. Nimeskikitishwa kwa kiasi kikubwa na manyanyaso wanayopata hao mabinti, pia ni aibu kwa waajili wao wanaposhindwa kulinda dhamana ya utu na uaminifu wa kumtunza mtu anayejituma kukusaidia shughuri zako tena kwa ujira mdogo kama huo, ama pia ni ushamba wa baadhi ya watu kusahau walikotoka kwani hata baadhi ya waajili wao wengi wao wamepitia maisha magumu lakini leo hii baada kufanikiwa kupata kazi nzuri basi wamekuwa na viburi na kuwa na mioyo ya kutu, very sad,

    ReplyDelete
  9. Serikali imeweka kima cha mshahara anaotakiwa kila mfanyakazi wa ndani, hii iko wazi kabisa na inajulikana na watu wote. Pili hairuhisiwi kumuajiri mtoto mdogo kama mfanyakazi sheria iko wazi.Tatu kosa la ubakaji au unyanyasaji wa kinjisia adhabu yake ni kubwa TZ ilimradi tu kesi ifike mahakamani.

    Hapa kinachotakiwa ni msaada wa kisheria ili haki ipatikane na sheria ichukue mkondo wake

    Tuna TAWLA, TAMWA na Kituo cha kutetea haki za binadamu, hivi wanasubiri kesi za aina gani ndio wachukue hatua? Au kwa sababu kwa hili hakuna Ulaji au posho za vikao wamekaa kimya? Kinawashinda nini kupeleka kesi kama ya huyu mtoto mahakamani? Serikali ifanyeje sasa?

    PELEKA HAO WATUHUMIWA MAHAKAMANI ILI WENGINE WAJIFUNZE KUTOKANA NA ADHABU WATAKAYOPEWA WAHUSIKA.

    ReplyDelete
  10. Haya mambo yanatia aibu hasa tukinzungumzia kwamba utumwa umekwisha sio kweli bado upo na ni mbaya sana maana tunatesana wenyewe kwa wenyewe na tulikuwa tunalia kwamba waarabu walitutesa na utumwa na kuchapwa viboko na kupewa kazi nzito.Kwa kweli sioni tofauti.Hawa wanawake ambao nao wamezaa na kutaka watoto wa wenzao kuwasaidia kazi za kuchunga watoto wao na wakuwatesa kama wanyama,hawa sio binadamu hawana utu ni wanyama pia maana fikiria mtoto huyo huyo unayemtesa angekuwa wa kwako ungefanya nini.Na ni kweli hao ni kama watoto au binadamu yoyote ana haki zote kama wewe mwajiri na sio mashine hawana hata muda wa kupumzika hata mashine inahitaji kupumzishwa.Hii sio haki watu wote mnaoajiri watoto wa watu kama hamuwezi kuwahudumia kama binadamu,ni bora kutowaajiri maana hamjui kuishi na watoto wa watu.Kwa sababu wanafikiria wanaenda kubadilisha maisha katika hatua nyingine ya kusaidia familia zao inaishia mateso.

    ReplyDelete
  11. Hi,
    Nilikuwa nataka kuangalia hii documentary lakini nimeshindwa kwa jinsi ilivyokuwa inasikitisha. nimeangalia huyo msichana wa kwanza tu. nikaacha imenitoa machozi. Nataka kuwasiliana nae na kumsaidia. tafadhali naomba mnieleze nitawazade kuwasiliana nae na kujua ni yeye. nifuate njia gani .Please, I want make a difference at least in one life. God told us to love one another.
    I hope to hear from you soon.

    ReplyDelete
  12. Mara ya mwisho nililia mwaka 2006, leo nimekumbuka machungu mengi sana na maisha ninayotoka pamoja na unyanyasaji kwa masikini hasa wa jinsia ya kike, kwa kweli machozi yamenitoka tena. Nimesikitika sana. Lakini pia nimefarijika sana kwa vile kumbe kile ambacho mimi na mke wangu tunamfanyia binti wetu wa kazi (ambaye sisi wote pamoja na watoto wetu tunamuta dada, na watoto humuamkia kila asubuhi kama vile wanavyotuamkia sisi wazazi wao) kinastahili kuigwa. Tunampeleka shule, na sasa yupo sekondari na anafaulu vizuri sana. Tunampandishia mshahara kama sisi tunavyofanyiwa maofisini kwetu, na tunampa bonus pia kila mwisho wa mwaka, ikiwa ni pamoja na kumdhamini safari za kwenda nyumbani kwao kuwasalimia wazazi. Sasa hivi tunapanga namna ya kumsaidia zaidi, hasa kwa kumuanzishia biashara yenye hadhi kwa mtaji wa bure, na tutamsaidia kuisimamisha biashara yake. Maana anakua, na muda si mrefu atahitaji familia yake pia, tusipomsaidia atasaidiwa na nani wakati wala hajiwezi? Waajiri wenzangu, tubadilike, tuwe na mioyo ya utu, na tumuogope Mungu. Pia kumsaidia asiyesiweza ni jambo la baraka. Poleni sana waajiriwa wa ndani mnaopitia manyanyaso yote haya na hata zaidi, nami nilitoka huko pia, ushauri wangu ni msikate tamaa na maisha, Mungu yupo.

    ReplyDelete
  13. Haya mabo yanasikitisha sana....Yule mwenye mtoto mdogo ameniliza sana....Si ajabu kuna watu humu wanasoma na usiku wanawatreat hawa watoto the same way as these people....Inasikitisha sana. Ila mimi nasema haya mambo hayataisha kabisa kama tusiporudisha uongozi wetu kuanzia down to t top badala ya top to bottom. Nakumbuka mama anasema tukiwa wadogo kulikua kuna mashina ya mitaa na balozi wa nyumba kumi. Mgeni akija lazima ukareport kuwa kuna mgeni. Atakaa siku ngapi na etc etc. kama ni mfanyakazi ni lazima ukareport kuwa kuna huyu mtu hapa anaishi na mimi. Hii ingekuwapo na kila mtu angejulikana ni nani na anaishi wapi. Na hao watu wa nyumbani waambiwe kuwa kuna mahalai pa kwenda kulalamika kama unateswa.

    Pili hivi si nimeona siku hizi kuna DNA test kwa nini hawa watu wanaoclaim wamebakwa na waajiri wao wasisaidiwe kupima kwa free na kamahuyo mtu ni mtoto wake 1) apelekwe jail kwa vile hiyi ni kurape. 2) Atoe hlea za kutunza huyo mtoto ...Just look at that babay ...Nimeona uchungu ananyonya na wala mama anaonyesha hana maziwa ya kutosha. Ameshoka katoy kamoja . I felt so bad..Nimemwangalia mwanangu nikasema why them....He is very lucky and we should thanks God for that

    ReplyDelete
  14. Jamani nyie mlio publish this document why don't you help me to get the contanct to the girl as I ask you.Please let me know how I can help. If you do not help me what is the purpose of puting such an information and then you do not want to help.
    bye for now.
    I hope you will help me.

    ReplyDelete
  15. ankal pole na kazi je nawaze mmpataje huyo dada mwenye mtoto.ili nimtumie chochote kidogo asante . mdau wa texas

    ReplyDelete
  16. Kma kweli Mungu yupo hawa wakina baba wanofanya haya matendo ni wabaya sana na mungu atawalipa tu kwa nguvu. Hili tatizo siyo kwa Housegils tu hata wasomi ambao wamemaliza chuo hawana kazi wakienda kuomba kazi Boss ni mapka awadanganye apate kitu kwanza ndiyo awape kazi na siku hizi hata hata hizo kazi hakuna sasa ni wanchezewa tu halafu wanawaacha hapo. Its shame, kama tungeakuwa na vyombo vya habari vinavyohusika kikamilifu wanwake wa tanzania wanbakwa kila dakika ipitayo. Wewe waone tu hao wakina baba wanapita hapo njiani unafikira kweli huyu ni mzee wa heshima hakuna kitu kama ufisadi ungkuwa unaandikwa usoni basi watu wasingetoka nje kwani kila mtu angejuwa siri zao. Maoni yangu kama hutaki binti yako atendewe hiyo naomba usiguse bint ya watu. KUna vibaka hapo Dar wantembea na magari kazi yao ni kutafuta watoto wa shule tu. Naomba kama unadini muogope mungu kwani adhabu utakayopata ni kali sana. Michuzi tafadhali usibanie.

    ReplyDelete
  17. Mawasiliano ya watengeneza filamu na walioiweka mtandaoni yapo katika ukurasa wa tovuti yao wa <a href="http://www.maweni.com/contact/>http://www.maweni.com/contact</a>
    Maelezo ya ziada yanaonekana katika video hii kuanzia dakika ya 24 tafadhali yanakili na kutafuta namna ya kuwasiliana na wahusika.
    Mimi niliyeiona na kuishirikisha watu wengine sina mawasiliano ya moja kwa moja na watengeneza filamu hiyo zaidi ya yale yaliyomo kwenye tovuti niliyoandika hapo juu. Ningeweza kufuatilia zaidi ya hapo ningefanya, lakini uwezo huo sinao ndiyo maana nikaafiki ombi la video hii kuwekwa kwenye blogu inayotemebelewa na watu wengi ili kuweza kuwafikia walwengwa au kupata ufumbuzi wake.
    Asante!

    ReplyDelete
  18. Hii hata haitasaidia!,.Hili ni jukumu la serikali kupitisha sheria iliyoko bungeni kwa miaka mingi kwamba hakuna ajira kwa watoto wakijumuishwa pia na hawa mahausi girl.Then,haya matatizo ya familia yaachiwe wizara ya ustawi wa jamii lakini kwa kuchelewesha hii sheria kisa njia haijapatika ndio haya sasa matokeo yake .

    ReplyDelete
  19. unaetaka mawasiliano ingia ktk web yao www.maweni.com simu +255784279371 na ktk web yao utaona mengi zaidi ya hayo ya wafanyakazi ukibonyeza video ya kwanza basi zinaongozana zingine nyingi tu inahitaji muda tu wa kuziangalia

    ReplyDelete
  20. jamani mie nimekerwa na hayo manyimbo kama wanaongea yani mbaya kupindukia sijui waliziweka za nini, mabinti poleni na wako wengi wananyanyasika sana,tatizo nchi yetu sheria hakuna kabsaaaaa, hata hao viongozi na wenyewe wanyanyasaji tuuu, kiundwe chama cha kutetea haki za wafanyakazi wa majumbani itasaidia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...