Gari walilokuwa wakilitumia

Michuzi pokea hizi image za mwizi aliyeuwa Tegeta. Hawa wezi inaonyesha wana mtandao wamevamia nyumba mbili alfajiri ya leo ambapo nyumba zote wenye nyumba walisafiri wakabaki wanafamilia. Hii inaonyesha wanapewa information na watu fulani. Pia wamekutwa na diary ya matukio ya uhalifu lini na wapi na no za magari na madereva watakaokuwa zamu.Inaonekana kwenye diary yao kuna mpaka no za maafande, na picha za magari waliokusudia kuiba pamoja na ratiba kamili.


Mdau
Tegeta
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Muda mwengine Askari na MAjeshi ndio wanakuwa Wezi Sana Kamati za mtaa lazima zianze kuwa karibu na ujirani na urafiki na kuaminiana kama zamani.

    Lazima mtaani waweke sungusungu wasisubiri Serikali sababu inaonesha hao Askari pia wezi.

    ReplyDelete
  2. Watu kama hawa hawastahili kuishi. Wauawe mpaka wote waishe. Safi sana.

    ReplyDelete
  3. Sitashangaa ndugu zake jambazi hili wakijitokeza na kudai kuwa polisi wameua malaika asiye na hatia. Huu ndio mtindo uliozuka Bongo. Majambazi yenye silaha yanauawa halafu ndugu zao wanadai polisi wameua watu wema wasio na hatia. Wamalizwe wote washenzi hawa ili raia tunaoheshimu sheria tuishi kwa amani.

    ReplyDelete
  4. ni kweli ni wezi na ni wadhambi lakini adhabu (mshahara wa haki) yao si mauti.

    Nyie mlomwua huyo mkiambiwa mikono husema si haki.

    Acheni sheria mloichagua ifate mkondo wake, msiwe wakatili na wanafiki.

    ReplyDelete
  5. 1. kulikuwepo na haja gani ya kuwekwa picha ya maiti?

    2. Kuchukua sheria mikononi hadi kuua ni kosa, na kila alieshiriki kumpiga huyu mwizi ajue mikono yake imejaa damu.

    ReplyDelete
  6. Mwili wa binadamu huheshimiwa - akiwa hai au amekufa. Ndiyo ubinadamu.

    Kati ya watu wote hao hakuna hata mmoja mwenye ubinadamu akajitolea angalau kipande cha kanga au gunia na kuifunika maiti hii?

    Nilishawahi kuligusia suala hili hapa:

    http://matondo.blogspot.com/2010/09/kibaka-akiona-cha-moto-abanikwa-kama.html

    ReplyDelete
  7. HA HAAAA....RAIA NAO KUMBE WEZI TUU ONA WAMEIBA HADI TAIRI NA TAA ZA GARI LA WEZI...WIZI HAUWEZI ISHA KW HALI HII... ITS ME

    ReplyDelete
  8. Kuhusu hili Tukio,mimi ni mmoja wa watu walioshuhudia kuiangalia na kusoma contents za hii diary aliyokuwa nayo kwenye gari lake usiku wa manane pale Tegeta maeneo ya Ununio...kwenye hii Diary kulikuwa na namba za Simu za Maaskari wa vituo ambao hukaa standby kwa ajili ya kujulishwa kusaidia kwenye uharifu punde noma inapotokea...Kulikuwa na ratiba za madereva ,ratiba za nyumba zitakazovunjwa...magari yenye namba za bandia ambapo vibao vyote vya namba vilikuwepo kwenye gari....Kosa moja lililo fanyika na wananchi wa tegeta ni kupoteza ushaidi kwa kumuua mapema yule driver(jambazi) kabla ya kumhoji vizuri,alikuwa na simu ya mkononi ambayo alikuwa akipigiwa na mtu ajulikanaye kama Manager...Huyu manager ni Fanancier ambaye aanaishi Sinza ndio sponsor wa matukio ya wizi...inaonekana wana mtandao mkubwa sana ambao wadau wake wakubwa ni askari police ....Hasira za wananchi kuamua kumpiga hadi kumuua ilikuwa ni kuogopa kuona yule mtu angeingia mikononi mwa police ,ushaidi wote ungepotea kama vile Zombe, na matokeo yake ingekuwa ni mtaji wa police kupeleleza na kuchukua hongo kutoka kwa waharifu....siku hizi hakuna sheria...wezi wanakamatwa lakini wakifika police wanahaonga na kutolewa nje.Kweli kuchukua sheria mkononi ni kosa...lakini unapoamua kutumia sheria ambayom haifuatwi ndio hasira zinawapanda wananchi na kuamua kuchukua sheria mkononi

    ReplyDelete
  9. aliyeiba na aliyeua wote manjakayanja i do know baba wa taifa alijisemea

    ReplyDelete
  10. We anon wa Sun Sep 26, 05:11:00 PM, japo umetetea uhalali wa kujichukulia sheria, basi mbona hukusema kuhusu kadiri/au kiasi?

    Muuaji hamumuuwi mnauwa mwizi.

    Na we wa Sun Sep 26, 05:53:00 PM,
    Muuwaji huuliwa lakini mwizi hulipa fidia na adhabu kadhaa, sio kumwua. Hawawezi kuwa sawa japo woote ni wakosefu.

    Hata wizi, aliyeiba shilingi moja huchekwa na aliyeiba milioni hufungwa.

    ReplyDelete
  11. Ikiwezekana tutumieni hapa jamvini picha za hayo magari yatakayoibiwa ili tujihadhari

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...