Mwenyekiti wa Muungano wa Machifu Mbeya, Shayo Masoko
(kulia) akimkabidhi Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja
wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete zawadi ya kuku wakati wa mkutano wa kampeni za ndani za chama hicho, Mbalizi, mkoani Mbeya juzi.(PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Vyuo na Vyuo Vikuu, tawi
la Mbeya, Timotheo Mnzava akimkabidhi Mjumbe wa Kamati ya
Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete taarifa ya mikakatiiliyofanywa na wananfunzi wa umoja huo kuhakikisha CCMinapata ushindi wa kishindo katika mkutano wa ndaniuliofanyika juzi jijini Mbeya. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete akifungua tawi la wakereketwa ya stendi ya Umalila Mbalizi, Mbeyajuzi,akiwa katika ziara ya kampeni ya kuweka mikakati yakuipatia CCM ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu,Oktoba 31, mwaka huu.
Mmoja wa walemavu akiwa miongoni mwa wafuasi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), wakiongoza msafara wa Mjumbe wa Kamati ya
Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete alipowasili Mbalizi, mkoaniMbeya kufanya mkutano wa kampeni za ndani za chama hicho, Mbalizi, mkoani Mbeya juzi

Wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiongoza msafara wa
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete alipowasili Mbalizi, mkoani Mbeya kufanya mkutano wa kampeni za ndani zachama hicho.

Msafara wa Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani Kikwete, ukilakiwa na maandamano ya wafuasi wa chama hichoMbalizi, Mbeya juzi, kufanya mkutano wa kampeni za ndani za chama hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. 1}jakaya 75%
    ii)lipumba 15%
    iii)slaa 9%
    iv)others 1%


    jakaya songa mbele

    ReplyDelete
  2. I can't believe we've reached so low....Huyu naye nani?? kama sio nyani?? Viongozi wamelewa madaraka nakujisahau hii sio nchi ya ufalme

    ReplyDelete
  3. Kidumu chama cha mapinduzi!
    Idumu siasa ya ujamaa na kujitegemea!
    Zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa CCM!

    ReplyDelete
  4. Lakini kikwete amejiachia sana, sijaona rais waliotangulia wakiingiza familia zao kwenye mambo kama haya

    ReplyDelete
  5. Katiba ya nhi inasemaje kuhusu public leaders kupokea zawadi? Leo kuku, kesho ng'ombe kesho kutwa sijui kiwanja...Ufisadi ndio hivi hivi zawadi zawadi

    Na utupe my comment Mungu anakuona

    ReplyDelete
  6. Anon wa pili acha ushamba, huyo naye katiba inamruhusu kushabikia chama cha siasa anachokitaka. Na kwa kuwa ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya CCM, ni mwanachama hai wa CCM ana haki ya kufanya kampeni bila kujali mahusiano aliyonayo na mgombea urais.

    Grow up na tembea uone, leo hii wameshindania nafasi ya Mwenyekiti wa chama kikubwa cha Labour nchini Uingereza ndugu wawili baba Ed na David Milliband, na wala haijasemwa ni usultani au ufalme, na mmojawapo ameibuka kuwa Mwenyekiti wa chama ambaye ndiye chama kikishinda uchaguzi atakuwa PM, cha ajabu kwa Ridhwani kushiriki siasa ni nini? Je ingekuwa ndio Bongo kaka wawili wanagombea hizo nafasi ingekuwaje?

    Kwa taarifa tu Ed Milliband amemshinda kaka yake David Milliband na kuwa mwenyekiti mpya wa Labour party na kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Gordon Brown. Ifike mahala tukue tuachane na wivu wa kijinga na watu waachwe washiriki siasa bila kubanwa eti ndugu zao ni nani na nani.

    Na haya mambo mbona vyama vingine vya siasa yapo tena huyu ndiye angekuwa ana uhusiano na viongozi wakubwa Chadema hata Ubunge angepewa bila hata kuchakarika au kufanya kazi yoyote kama walivyopeana ubunge wa viti maalum ndugu wa viongozi wa Chadema. Kwa hiyo toeni boriti kwenye macho yenu kwanza!

    ReplyDelete
  7. Poor Tanzanians,
    Yaani hawa vijana wamerubuniwa shauri ya umaskini walio nao. Ridhiwani anatembea na shangingi wao hata viatu hawana then wanampigia kampeni huyo mtoto wa rais? what a shame to my fellow poor tanzanians?
    Tufike mahali tujithamini utu na utanzania, tuache kuhongwa na hela ndogo.
    Afterall ccm inaendekeza umasikini na ujinga ili iwe rahisi kuwarubuni maskini wa vijijini.
    Mungu tuokoe na huu utumwa

    ReplyDelete
  8. we anonymous unayejifanya kujua mambo ya politics za uingereza, nani kakwambia mimi sipo huko, nimeishi miaka 30 hapa UK na sijaona huyo gordon brown , tony blair, david cameron au margreth thatcher akiingiza wanae kwenye mchakato wa siasa. hao akina miliband wako kwenye system tangu enzi na hakuna kati yao aliyekuwa anampigia debe mwenzake ashinde, kila mtu ni politician and they deserved, tofautisha nyoooooooooo

    ReplyDelete
  9. Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ina wajumbe kibao. Bado nashindwa kuelewa ni kipi ambacho huyu mtu amekifanya ambacho wajumbe wenzie hawajakifanya ambacho kinamfanya aandaliwe maandalizi mazito anapotembelea mikoani.
    Angalia mtoto wa Mzee Ruksa, Dk Mwinyi. Tumekuja kujua kwamba ni kijana wa mzee ruksa baada ya juhudi zake kumfikisha alipofika. Hata masuala ya mabomu mbagala tumeyasahau kwa sababu ni tabia yetu lakini hayakuzimwa kwa nguvu ya Mzee Ruksa.
    What has this guy done for the country so far? Something is not right.

    ReplyDelete
  10. Wewe uliyetukana mwisho wa kutoa maoni unaonyesha ni mfuasi wa chama cha matusi kilichoshindwa kutoa sera na badala yake kinaishia kutoa matusi. Umejibu ya UK mbona ya watu fulani kuweka mabinti na vimada wao kuwa wabunge wa viti maalum hujaweka? Tena aibu mpaka ya kupigana kwenye mabaraza yao.

    Haya natuone mimi na wewe mshamba nani, Bill Clinton alimfanyia mkewe kampeni mpaka dakika ya mwisho, na Mke wa Obama naye alimfanyia kampeni mumewe mpaka dakika ya mwisho. Sema na huo nao uwongo.

    DALILI YA MTU MWENYE KUSHINDWA NI KUTUKANA, maana mmeishiwa hoja sasa, eti nimekaa miaka 30 unaweza kukaa hata miaka 50 lakini ukawa unaishi kule kwa wenzio kule Eastenders! Ustaarabu hakunam utajuaje siasa za UK zinavyoendelea? Labda ungekuwa unaishi Central London au Zone 1 ndio ungejisifia hapa kuliko kujisifia kuishi kwenye nyumba ya council uliyokuwa unakaa bure!

    ReplyDelete
  11. Kwa ujinga huu wacha tu tuwe maskini na nasema wale wa vijijini endeleeni kuipigia CCM na msilalamike maisha magumu na dhambi ya kuichagua CCM iwatafune vizuri!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...