hii ni ming'oko aina ya mihogo asilia inayopatikana mikoa ya kusini ya lindi na mtwara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

 1. aise hii picha inanikumbusha Pwani kule Maneromango,Boga,Msanga,Kibuta malumbo kwa akina tambalizeni kule ni chakula tosha wanaita Mbao na shughuli ya kuchimba inawahusu sana wasichana na wanawake wazee.wenyewe wanakula na chachandu yaani pili pili na limao. Asante kwa kunikumbusha mbali lakini huku Arusha akuna vitu kama hivyo

  ReplyDelete
 2. nilisoma shule ya msingi ya Msinjaili Lindi miaka ya themanini. Asili yangu ni nyanda za juu kusini
  Asante kwa kunikumbusha Lindi. I miss you Lindi. It was fun. Kutoka kula vinyumbu mpaka kula ming'oko hahah

  ReplyDelete
 3. ukila hii ya kuchoma wakati wa kwenda kustarehe lazima uende na feni !!

  ReplyDelete
 4. KulembelaChaniOctober 21, 2010

  Michuzi, yaani hapa umenikumbusha mbaaaaaaaaaaaali, ming'oko kwa chumvi na pilipili, hii ndio candy-cane kijijini kwetu. Haipandwi mashambani bali ni kazi mzuri ya maulana, waliojaribu kuipanda walishindwa kwani inasadikika kwamba ming'oko uhama kutoka sehemu moja hadi nyingine.
  Wachimbaji wa ming'oko uchimba kwa kubahatisha wakiongozwa na machimbo ya nguruwe mwitu ambao ndio walaji na majiolojist wakubwa wa ming'oko, vile vile wachimbaji ugundua kuwapo kwa ming'oko kwa kutafuta aina fulani ya mimea (mikopo)inayojitokeza sehemu ambayo ming'oko ipo bila kuchimbwa kwa miaka kadhaa

  ReplyDelete
 5. umekosea kuandika mtwara! sio mtwara bali Ntwara

  ReplyDelete
 6. Jamani Ankal Michuzi vipi haya mambo??? Hata kanuni ndogo narahisi tu za uandishi huzingatii?!?!!! Herufi kubwa mwanzo wa sentensi na kwenye majina ya watu au mikoa!!!???

  ReplyDelete
 7. Nakumbuka miaka ya tisini nikiwa Mkonge sekondari, nimetokea Mbinga ambako kuna mboga maarufu kama hiyo inayoitwa KIKANDI. Michuzi endelea kutuletea vitu vya asili kama hivyo ili tukumbuke jadi yetu! big up michuzi!

  ReplyDelete
 8. Michuzi this is the best artical it reminds me kwetu Mnyambe na vinyumbu kwetu tunaita luvale.

  Kuna mtu yeyote ambae anaweza kujua botanical name ya min'goko na vinyumbu?

  It will be nice to know what benefits they have.

  ReplyDelete
 9. ankal hukuona upupu? hapa menyu haijakamilika! kwa wale walionielewa! he he heeee!

  ReplyDelete

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...