Mh. Lazaro Nyalandu CCM akishukuru baada ya kushinda Ubunge Singida Kaskazini kwa kwa kuzoa kura 41,102 (91%) na kumshinda Mgombea wa Chadema Bwana Rashidi Kimia aliyepata kura 3,544 sawa na asilimia 7.8.
Mh. Nyalandu alikuwa mgombea pekee wa ubunge
aliyetumia usafiri wa helikopta, ukiacha JK na Dk. Slaa waliogombea urais

Mh. Nyalandu na mai waifu wake Faraja Kota
wakiwasili mkutanoni kwa chopa
Mh. Nyalandu akihutubia mkutano wake wa
mwisho uliokuwa na nyomi ya maelfu ya watu wapatao 35,000




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Tatizo ni uadilifu....gharama za helikopta ni kutoka kwa nani? Kama kapata fedha kihalali hakuna shida, lakini kama ni fedha za ufisadi, tunahitaji maelezo takukuru wameshachukua hatua gani.

    ReplyDelete
  2. PESA ALZOTUMIA HAPO, ATAZIRUDISHAJE? KAMA SIO UFISADI

    ReplyDelete
  3. Sasa hakuna aliyemuuliza huyu Mheshimiwa wapi anakotoa mapesa ya kujirusha na helikopta wakati wapiga kura wake wengi hata baiskeli hawana.

    Hii haitii akili, kule wapigakura wake ni wadanganyika! Sasa umuhimu wa helikopta katika kijimbo kimoja ni nini? Ndiyo maana watu wataendelea kuidharau CCM kutokana na mbwe mbwe za waheshimiwa wa CCM kama huyu wenye mikogo wakati raia wengi wako katika dimbwi la umasikini, ambao hata mlo mmoja kwa siku ni matatizo.

    Naelewa wananchi bado wanashanga ni vitu kama helikopta na najua wengi katika huo muhadhara wake walikuja kushangaa hiyo helikopta, na wamempa ushindi wakifikiri jamaa yuko juu sana, lakini nawahidi kwamba hapo wameliwa.Miaka mitano hijayo itakuwa migumu kwao na hizi mbwe mbwe za helikopta ni kiini macho tu.

    ReplyDelete
  4. Ninavyowajua warangi na ushamba wao kweli walikwenda kuangalia helikopta. Jamaa amezoa kura kwa ajili ya helikopta tu na si maendeleo ama sera.

    ReplyDelete
  5. Ukioa Miss basi inabidi umfurahishe. Faraja Kota si nani furahia maisha ya ubunge lakini nawewe ulikuwa uvae KICCM.

    ReplyDelete
  6. Ukioa Miss basi inabidi umfurahishe. Faraja Kota si nani furahia maisha ya ubunge lakini nawewe ulikuwa uvae KICCM.

    ReplyDelete
  7. Hahaha Mhe. Nyalandu naona unawaua ma haters...PR yako si Mchezo!! Vijana wa USA naona hawataki kukusikia kabisa. Hongera kwa Ushindi.

    ReplyDelete
  8. naomba kuuliza swali jamani, hivi gharama ya kukodisha helikopta ni kiasi gani?

    ReplyDelete
  9. annon hapo juu kwa taarifa yako singida si kwa warangi hii inaonyesha jinsi ulivyo mtupu kwa uchache wa kuelewa na mvivu wa kujifunza, ustake usitake amini kuwa watu wamemkubali mhe nyalandu, hongera yake na ww ndio walewale waosha vinywa

    ReplyDelete
  10. Namna hii na mimi itabidi nitafute mume mbunge jamani, hivi kuna single aliebaki

    ReplyDelete
  11. Nilikuwa nataka kumjibu jamaa aliyeuliza hapo kwamba gharama ya kukodisha helucopter ni sh ngapi. Ghearama ni $25,000 kwa masaa 11 kutokana na kwamba sheria za anga Tanzania aziruhusu kusafiri kwa helicopter nyakati za giza.Makao makuu yetu yako Nairobi na tunapokea malipo kwa $ au whatever reflects the $ rate at that particular day.Tuna record nzuri ya usalama. Shukran.

    ReplyDelete
  12. Basi Michuzi unafurahia kichizi kuandika hayo matokeo, naona umekolezea kabisa eti jamaa yako Nyalandu amepata 91% na mzalendo wa CHADEMA kapata 7.8%. Ama kweli Bongo inawenyewe na wanaoihodhi mnaifaidi kichizi.

    ReplyDelete
  13. nikusaidie best unayeuliza wabunge ma 'single', try Joseph Mbilinyi..a.k.a sugu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...