Naibu Mkurugenzi Idara ya Usalama wa Taifa Bw. Jacky Mugendi Zoka akizungumza na waandishi wa habari leo katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar wakati alipotoa taarifa ya kupinga madai ya Dk Willbrod Slaa Mgombea urais wa CHADEMA kuwa idara hiyo imeshiriki katika kuchakachua Kura za mgombea huyo wa urais.
Naibu Mkurugenzi huyo amesema wananchi wampuuze Dk Slaa kwa kauli yake kwani madai yake hayana ukweli wowote na ameongeza kwamba idara yake haijajihusisha kabisa na masuala ya uchaguzi hivyo madai hayo ni ya kuipaka matope idara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. HAWA JAMAA WA CHADEMA SASA WANAANZA KUTUTIA WASI WASI! JUZI SHIBUDA KAROPOKA MANENO HATA KABLA MATOKEO YA UBUNGE JIMBONI ALIKOGOMBEA HAYAJATANGAZWA, AKADAI KUNA UCHAKACHUAJI.
    LEO HII NA SLAA NAYE ANAROPOKA MANENO HAYA. WANATAKA KULIPELEKA WAPI TAIFA LETU?
    UBABAISHAJI MKUBWA KAMA HUU KUFANYWA NA VIONGOZI WA NGAZI KAMA YA SLAA NI HATARI SANA KWA SABABU UNAWEZA KULETA REACTION INAYOWEZA KULIINGIZA TAIFA KATIKA JANGA LA KUTISHA.
    KWA NINI KAMA WANA ISSUE ZINAZOHUSU MASUALA YA SHERIA, WASIYAPELEKE KUNAKOHUSIKA?
    NA KAMA WATASEMA HAWAVIAMINI VYOMBO VYA SHERIA, KWA NINI BASI WAKAINGIA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA UONGOZI?
    KWA MTAZAMO WANGU, MTU KAMA SLAA HAWAFAI KUWA VIONGOZI WA KIWANGO CHOCHOTE KTK TANZANIA YETU.
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  2. UNAYEJIITA MNDENGEREKO,
    WHAT IF IBAINIKE USALAMA WA TAIFA WALIHUSIKA? KWANINI UNADIKIRI KUSEMA MTU MBABAISHAJI WAKATI HUNA USHAHIDI? UNAKUWA UPENDE WA USALAMA WA TAIFA WAKATI HUJUI HATA UKWELI WAKE? HUONI HATA WATU WA USALAMA WENYEWE WATAKUSHANGAA, ENDAPO WALIZIFANYA HIZO TUHUMA?

    MIMI SIKO KWA SLAA, WALA KWA USALAAMA WA TAIFA, HADI PALE UKWELI UNAPOTHIBITIKA KWA USHAHIDI. SLAA PEKE YAKE HATOSHI KUWA KITHIBITISHO CHA ANAYODAI. VILEVILE, WATU WA USALAMA WA TAIFA, HAWAWEZI KUKANUSHA TU, IKATURIDHISHA KUWA NI UKWELI WAKATI HATUJUI.

    WEWE NDIO UNATAKA KUTULETEA BALAA KWA KUCHOCHEA BILA KUTUMIA BUSARA. MNDENGEREKO HUFAI KUWA HAKIMU AU JAJI, MAANA HUTUMII MAANTIKI KATIKA MAAMUZI YAKO.

    NAWASILISHA.

    ReplyDelete
  3. Slaa halopoki utakuwa unamkosea adamu mwenyekiti wa tume aliyekiri wazi kuwa madai la Slaa kuhusu matokeo ya Geita ni ya kweli na wanayafanyia marekebisho. Allow your mind to think achana na ulevi wa vyama vya siasa. Vyama vitatumaliza watanzania tusipokuwa makini maana viongozi wake wanaangalia Ikulu tu hawajali haki za watanzania

    ReplyDelete
  4. Maoni ya "MNDENGEREKO" yamekaa "KINDENGEREKO" hata kama yuko UKEREWE !!!

    ReplyDelete
  5. wewe mtoa waoni ya kwanza acha kuongea pumba ! ujihi unaloongea , ama utakuwa chizi kidogo.

    ReplyDelete
  6. KWA NINI UNAWAJIBU HAO? WEWE SLAA NA WENZIO ACHENI ULIMBUKENI WA SIASA WW UMEONA WAPI MTOTO ANAYETAMBAA AKAPEWA KITI AKAE? MNATAKIWA KUHESHIMU IDARA YA USALAMA NA SERIKALI ALAA.

    ReplyDelete
  7. godbless mchagaNovember 05, 2010

    mkiwachekea hao wataingia mpaka chini ya uvungu na kuitukana serikali,washughulikiwe ipasavyo.

    ReplyDelete
  8. ni ukosefu wa adabu kuikashifu idara.

    ReplyDelete
  9. Akiwa katika mkutano wake wa kampeni huko Mwembetogwa Iringa, Dr Slaa alitamka wazi kuwa Usalama wa Taifa wanaripoti kwake. Watu wakakaa kimya hawakuhoji hilo wala kukanusha. Walioona hatari yake wakalikemea mmoja wao ni Mjengwa kwenye blogu yake. Hapo ilikuwa wazi kabisa ana kitu huyo Dr Slaa anakiandaa na hicho ndicho kimeonekana.

    Cha ajabu tunauliza iweje vijana hawa wanaoripoti kwake wamhujumu? Kwenye mkutano mwengine alitamka pia anaiendesha serikali kwa rimoti, sasa hiyo rimoti yake imeshindwa kumpatia ushindi?

    Tena kuna maeneo kama Mtwara ambako JK amepata kura zaidi ya elfu 30, na Dr Slaa hakufanya kampeni kabisa atazitoa wapi hizo kura wamwibie?

    Chama chake hakina mashina vijijini, na wengine bado hawaaamini upinzani, wanaona kuwa unataka kuleta machafuko, Dr Slaa anataka kuwathibitishia watu kuwa kweli upinzani ni fujo.

    Mwisho Michuzi acha kuposti matusi makubwa yenye kudhalilisha utu wa mwanamke, huna unayemfaidisha kwa kuweka matusi ya nguoni. Nafikiri umesoma magazetini kesi ya Moshi ya
    matusi ya facebook na sasa ni mwendo mdundo tutawachukulia hatua za kisheria wachochezi wote na wenye kutumia lugha chafu ili heshima irudi mahala pake. Na nyie wenye blogs mna wajibu wa kuhakikisha hakuna lugha chafu za matusi kwenye blogs zenu maana zinasomwa mpaka na watoto.

    Namripoti kwako mtoa maoni wa Fri 03:07 Am. huyu yuko nje ya nchi na anafikiri kuwa mkono wa sheria mfupi. Kwa taarifa yako na wengineo hata huko mlipo kuna sheria kali kuhusu kutumia abusive language na tena nyie kuwapata ni rahisi sana kwa sababu IP address zenu zinaweza kuwapeleka mpaka majumbani mwenu tofauti na TZ ambako mfumo wa address bado!

    ReplyDelete
  10. MkandamizajiNovember 05, 2010

    I don't think usalama wa taifa needed to say anything. They shoulda just shut up, let the chaff separate itself from the grain.

    Michuzi, tunasoma blog yako kwa sababu humu huwa hatukuti matusi. Usitufukuze please, ondoa hayo matusi.

    ReplyDelete
  11. (b)Nyooooh, we mndengereko huna lolote unalolijua, utabaki hivyohivyo na mawazo yako mgando!.
    Wacha SLAA adhibitishe ukweli kwa kutoa ushahidi alionao juu ya usalama wa taifa na tume ya uchaguzi kuchakachua matokeo ya uchaguzi.
    Acha kuwa ulimbukeni wewe!(/b)

    ReplyDelete
  12. Mtoa maoni hapo juu umenifurahisha sana sijapendezewa na matusi yaliyoandikwa. Vijana wanajisahau wanataka kulazimisha ushindi. Chama hakina ofisi kwenye matawi hata wagombea waliweka 179 sasa mnataka kuchukua nchi kupitia magazeti hahahahahah imekula kwako

    ReplyDelete
  13. nashindwa kuamini kama nasoma matusi mazito ambayao hayajahakikiwa katika blog hii ya ustaarabu, iweje leo uncle umeruhusu uchafuzi wa huu wa hali ya hewa. au maoni kama haya sasa hivi huku nako yanaruhususiwa tuambie mapema tuchanje mbuga hii blog ya wastaarabu. Huyo slaa imekula kwake chama chake kimemkangaa sasa hivi akitaka kupasua bomu basi aitishe waandishi wa habari maana bungeni tena ndio kwishnehi, hivi ulifiki kule kijijini wanajua kama kuna Slaa sana sana ukiwauliza wanaweza wakakujibu hiyo panga au mkuki, watanzania tuwe makini jamani majina ni nafsi na yanaumba kama jina lake huyu ni silaa kweli na anataka itumike kivita.

    ReplyDelete
  14. ukweli ni kwamba uchaguzi haukuwa wa kweli na haki.matokeo yamecheleweshwa bila sababu kama si kuchakachua ni nini?hata wakaguzi wa ndani ya nchi wameliona hilo.

    ReplyDelete
  15. Inaelekea Michuzi husomi hata hizi comments...kuna mtu ametuma matusi ya nguoni katika hii topic ya usalama wa taifa na Slaa. Please iondoe. Sio maadili tafadhali. Next time, bora upitishe maoni 2 lakini uliyoyahakiki ndio maana ya kazi yako. Asante. kazi njema

    ReplyDelete
  16. Wewe anony wa Tarehe 05, 03:07:00 AM, usituchafulie hali ya hewa kwa kutumia lugha za matusi kwenye globu ya jamii..embu jifunze ustaarabu hata kidogo ...

    Ni hayo tu

    Maliaga

    ReplyDelete
  17. NYIE MALIMBUKENI WA SIASA MSILETE JAZBA NA KUMSINGIZIA MICHUZI ANAACHA MATUSI WAKATI NI UONGO NA WEWE UNAYEANDIKA NI MTU MMOJA.MWAMBIE HUYO MUME WAKO MABUNDUKI AIHESHIMU SERIKALI NA IDARA ZAKE HATISHWI MTU HAPA CCM KAMA KAWAIDA.

    ReplyDelete
  18. Kwenye jamii ambayo kuna demokrasia ya kweli, hata serikali inakosolewa. Hii ni pamoja na idara zake. Kwa mfano, U.S., police, FBI, na wengine hukosolewa wakifanya makosa, na KAMWE wananchi hawakamatwi kwa kuikosoa serikali. Sasa kama Dr. Slaa anaishutumu Intelligence Service kwa lolote kuhusiana na uchaguzi, hilo sio KOSA AU KUKOSA ADABU. Kumbukeni, serikali sio jengo au bunduki au gari, ni wanadamu kama mimi na wewe ambao wanaweza kutumia madaraka/mamlaka yao vibaya kuhujumu haki za wananchi. Hata Obama huwa anawekwa kiti moto na wananchi. Tatizo ninyi mnazo heshima za uoga/uongo. Mnaogopa mkifikiri mnaheshimu. Panukeni mawazo, pengine tembeeni muone na kujifunza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...