JK akiwa na Ali Kiba ambaye alitumbuiza katika uzinduzi wa kampuni mpya ya simu iliyonunua Zain ya Airtel usiku huu katika ukumbi wa Mlimani City Conference Centre jijini Dar
JK akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wakuu wastaafu Mzee John Malecela, Jaji Warioba Dk. Salim Ahmed Salim, Mama Anna Kilango-Malecela na viongozi wa juu wa Airtel

JK akiwa na watendaji wakuu wa Airtel
baada ya kuzindua kampuni hiyo



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Wadau,
    Naomba kufahamishwa, nini faida au hasara kwa taifa iwapo kampuni moja inabadili wamiliki wake na hasa kuhusu suala la kodi? Mfano mzuri ni Sheraton! Nauliza swali hili maana redio mbao mara nyingi zinadai kwamba Wadanganyika ndivyo tuibiwavyo. Je ni ya kweli? Ikiwa ni kweli, kwa nini Mheshimiwa anaitwa ku-grace take-over?

    ReplyDelete
  2. Hivi wadau huu mtandao unavyobadilisha badilisha majina sio mbinu ya kukwepa kodi kweli? Isijekuwa kama vile Sheratoni ilivyokuwa inafanya. Si mnaelewa wakibadilisha jina inaonekana kampuni mpya then wanapata tax holiday...Wasijewakawa wanafanya usanii hawa owners wa (Celtel, Zain,Airtel...)

    ReplyDelete
  3. I don't think kama wamebadili registered name, kilichobadilika ni jina la kibiashara.Hii maana yake ni kwamba jina la kampuni linawezakuwa ni Celtel tanzania Ltd lakini trading as Airtel. Kama nimekosea nisameheni kwa ufahamu wangu mdogo.

    ReplyDelete
  4. Naungana na Anoy 03:41
    jina la kampuni linabakia Celtel Tanzania Ltd, kinachobadilika ni jina la kibiashara.
    mfano, mie huwa nalipa hao waliokuwa zain na sasa airtel, lakini malipo yatakiwa kuwa kwa jina la Celtel Tanzania Ltd,

    ReplyDelete
  5. Anony wa Tue Nov 23, 03:41:00 AM.
    AIRTEL imebadili kila kitu, yaani license zote za kibiashara kule Brela.
    Lakini ilivyobadilishwa from Celtel to Zain ilikuwa ni changing ya trading name tu.

    Ila kwenye swala la kodinaomba wataalamu wenye ufahamu juu ya tax law watusaidie.

    ReplyDelete
  6. Mimi nitakufa na CELTEL,ZAIN,AIRTEL yani nazimia kinoma,what i understand is that the name everywer esp in the government registration stays the same which is CELTEL lakini ni brand name tuu which changes!like i usually pay them my bill na the cheque has to be CELTEL TZ LTD otherwise they refuse it!
    karibu AIRTEL

    ReplyDelete
  7. Suala la Msingi hapa ni kampuni kuuzwa, Je Sheria zetu zinasemaje kwa mmiliki mpya kutumia jina lilelile la Zamani

    ReplyDelete
  8. tungepata mjibu ya uhakika ingekkuwa swa lakini hapa waadau naaona tunalabdisha tuu

    ReplyDelete
  9. Huu ni uhujumu na ukwepaji kodi na inaonekana kuna viongozi wakubwa waliona na mokiono yao ktk kampuni hiyo. Kama kuna uwezekano ni kujaribu kufuatilia kama hii Airtel italipa kodi au watapewa likizo la kutolipa kodi. Kama JK ataendelea kuwabeba watu kama hawa basi CCM ijiandae kutoka madarakani 2015.

    ReplyDelete
  10. This time wamebadili na jina kabisa kutoka Celtel kwenda Airtel Tanzania lakini hakuna ukwepaji wa kodi (ni normal business sale kama mnavyoona huko majuu). Sheria za kodi zilibadilika tangu 2004 (New Income Tax Act 2004 which came into effect from 1 January 2005) na mambo ya tax holidays yaliondolewa kabisa na hayatakaa yarudi tena. Mwanasheria

    ReplyDelete
  11. Airtel have only aquired the assets and clients of Celtel/Zain. Hence there should be no re-registration processes.

    My question is why are there so many high ranking officials in this function??

    ReplyDelete
  12. Wadau hii ni tofauti na ilivyokuwa Celtel to ZAIN. Kipindi kile walibadilisha jina la biashara ( Brand name) lkn kipindi hiki kampuni imeuzwa rasmi kwa Airtel na kila kitu kitabadilika. Kuhusu Tax holiday inatolewa kwa new business tu na si kwa kununuliwa ama kubadilishwa jina.

    ReplyDelete
  13. Lolote ni possible, kampuni inaweza ikawa imesajiliwa upya kwa maana ya kuwa kumpani ya zamani inafutwa kwenye regista na kampani mpya ndiyo inaingizwa. Pia kampani inaweza ikuwa imebadilisha tu jina hivyo inasajidili tu jina. Anyway kama mtu anataka kujua kwa kina nini kimetokea awaone hao jamaa wa Airtel au aende kwa msajili wa makapuni kupata maelezo zaidi na kamili ya nini kimetokea.


    Hili ni swala la vyombo vya habari kufuatilia. Lakini Tanzania kuna tatizo kubwa la waandishi wa habari wa mambo ya biashara, wengi wamejikita zaidi kwenye siasa, na sijua ni kwa nini.

    ReplyDelete
  14. Jamani hawa tumewachoka,kila mara kampuni inauzwa, mara wanabadili jina,sasa shauri zenu nyie mnaotumia mtandao huo wa Airtel mtakuja uzwa nanyie muda sio mrefu.

    ReplyDelete
  15. Mi nafikiri wadau wengi hawaelewi mchezo huu. si kweli kwamba hawa jamaa wamebadili jina la kampuni tu. ukweli ni kwamba Zain imeuzwa kwa Airtel , na kwa sheria za kibiasahara (za nchi) panapofanyika mauzo lazima kodi ilipwe kwani kimsingi biashara inafanyika. Ninachojua makampuni makubwa yanapouzwa kodi lazima ilipwe, inaitwa 'capital gains tax' kwani yule aliyeuza(zain) ameongeza mtaji wake kwa kuuza kwa bei kubwa kuliko aliyonunulia.

    Nakumbuka mchezo huo walitaka kuufanya kenya, serikali ikagoma mpaka kodi stahili zitakapolipwa ndipo zain iuzwe. sna uhakika wamefikia wapi.

    Jamani tujitahidi kuwa wadadisi kidogo na si kukubali kila uongo tunaoambiwa.

    mfano mdogo: kama umewahi kununua gari kwa mtu halafu ukataka kubadilisha kadi ya gari ili iwe kwa jina lako, TRA lazima watakulipisha kodi kwani wanajua mmeuziana(biashara) kwa nini isiwe kwa hawa.

    ReplyDelete
  16. Si bure bendi za muziki wa dansi wa kweli zina wakati mgumu kama MsondoNgoma, Sikinde, Wazee Sugu Njenje n.k.

    Maana kampuni kubwa kama hii inaona bora kumlipa mwanamuziki mmoja wa kizazi kipya!

    Ila pengine bendi za muziki wa dansi pia zielekeze mbinu za kupiga miziki ya 'cover'(kuigiza nyimbo maarufu duniani) vizuri kama Inafrika, labda wataweza kupata tenda za makampuni makubwa.

    ReplyDelete
  17. Kuna mambo kadhaa yanategemeana na kwenye mkataba mzima wa acquisition. Kama hii ni independent subsidary ya kampuni ya airtel then lazima waregister jina upya na mambo kama hayo.

    Ni ngumu kuzungumza mpaka ufanikiwe kuona mkataba mzima wa ununuzi.

    Mdau wa USA

    ReplyDelete
  18. Wadau hapo juu, inakuwa vigumu mtua anayefahamu aanzie wapi kuelezea bila ya kupata upinzani mkali na kutukanwa na wadau. Mpaka hapo elimu ya chini ya msingi wa biashara, mfumo wa makampuni, umiliki hisa utakapoeleweka kwa wengi. Leo nina baa yangu hapa sinza inaitwa TopTop Bar nikaiuza kwa mtu mwingine je nimeuza Baa au nimeuza Nyumba? Na je kuuza huko kuna maana nimekwepa kodi au TRA hawawezi kunidai kodi ya huko njuma? Pia nnunuzi mpya hawezi akaibalisha jina kuwa Mama Mia Bar?

    Mmoja wa aamiliki wa Celtel wameuza share zao kwa wamiliki wapya na kampuni inaendelea kama kawaida bila kuvunjwa na kuanzishwa upya, mikataba yote ya celtel inaendelea na pamoja na hayo kodi zote za zamani na sasa ninaendelea, kila kitu kinaendelea bila dosari kisheria. Ila wamiliki wapya wametaka na jina libadirishwe na ni kawaida du. ELIMU ELIMU;;;; mimi Alex Bura

    ReplyDelete
  19. Ali Kiba kama function inahudhuriwa na Mr Rais au officials wengine usivae namna hiyo.

    Jifunzeni kuvaa kuendana na occassion jamani na hasa kama umeamua kuufanya muziki kuwa ni profession yako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...