Ankal Michuzi eeee...
Nasikia sheria ya tanzania hairuhusu mwanafunzi wa kike mwenye ujauzito kuendelea na elimu wakati mjamzito. Na kwamba serikali huwa inapata tabu sana kuwagundua wanafunzi wenye ujauzito wakati mimbazao zikiwa changa.

Mimi kama mdau ambaye napenda serikali isitumie gharama sana katika suala dogo kama hili sababu tuna mambo mengi sana yanayotakiwa yafanywe ili uchumi wetu ukue. Nashauri wachunguzi wa mimba za wanafunzi wangetumia picha hiyo ya embe hapo juu ili kuwagundua wanafunzi wenye ujauzito


Yaani, ichukuliwe embe kama ilivyo ktk picha kisha sichana atakaetemamate kwa sana basi itakua tayari kigezo cha kupelekwa hospitali kwa uchunguzi zaidi kuliko kuwapima wanafunzi wote.
Mdau BAB TID

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. Kwa hiyo unashauri kuwa turudi zama za kale. Isitoshe ,kwani serikali inampango gani baada ya kuwatambua wenye mimba zaidi ya kuwaachisha masomo?

    ReplyDelete
  2. baada ya hapo nini kifanyike? akikutwa na mimba afukuzwe shule halafu? BAB TID hongera kwa kuzaa watoto wa kiume tu.

    ReplyDelete
  3. Did you seek legal advise to see whether your comments are legitimate constitutionalwise,or you are just writing from your personal feeligs?

    ReplyDelete
  4. Mimi sikubaliani kabisa na hizo sheria za mwanafunzi wa kike aachishwe shule sababu ya ujawazito. Hii siyo fair kabisa kwa wasichana. Kwanza kabisa hiyo mimba aliipatia wapi? Maana it takes two to tangle sasa huyo aliyempa mimba yeye ndio aendelee na shule? Haki iko wapi hapo? Basi na wanaume waadhibiwe waachishwe shule. Cha muhimu ni kuwa na mafunzo ya kuzuia huo ujauzito na bahati mbaya mimba ikipatikane asifukuzwe shule . Mwache aingie darasani kwani anazuia nini kuwa humo darasani? na kama haiwezekani basi akajifungue arudi amalizie shule. Hayo ndio yangu. Lazima tuwe na haki . Tusiegemee upande mmoja tu.

    ReplyDelete
  5. wewe sijui hata nianzie wapi. Tunakuombea mungu akupe akili maana kwa sasa huna. Huelewi kuwa mtu yeyote awe na mimba au asiwe na mimba anaweza kuchuruzikwa na mate akiona embe mbichi. Pole kwa mawazo finyu na yasiyo ya kisayansi wala kiitikadi.

    ReplyDelete
  6. Mimi ndio maana huwa napinga mtu asiye na elimu kuweka maoni yake hapa. Sasa tunaona wenyewe, eti wale embe....ujinga kkweli kweli.

    Sijui mdau ameshasikia kuwa kuna hospitali siku hizi? Serikali ikiangalia mbali, itaona kuwa ni wajibu wa serikali na jumuia kumsaidia msichana ili mtoto wake akue na afya na pia aweze kujisaidia kuendesha maisha yake badala ya kumwachisha shule na kumpeleka katika umasikini maisha yake yote.

    Kama atawaidiwa basi ataweza kuendelea na elimu yake na kufanya kazi na kuendeleza familia yake. Kwa kuwa sisi tuna mawazo ya kale, basi naona mpaka mzungu aje, atuambie ndio tutafanya hivyo. Ila kwa sasa tutumie maembe kama huyu pumba anavyotaka. Maoni haya katika karne ya 21 yanaonyesha jinsi Watanzania tulivyo nyuma kielimu.

    ReplyDelete
  7. Ningekuwa karibu nawe ningekutandika viboko usahau jina lako. Kabisa uka kaa chini kuandika upuuzi. Suala la mimba ningekuwa mimi ningewashughulikia wanaowapa mimba na wala si wabeba mimba. Nashangaa sana wanaofukuzwa shule ni wasichana na wanaume wanaachiwa na hao wababa wakubwa wanajikausha majumbani kwao

    ReplyDelete
  8. sometimes tuwe tunaangalia tunachosema,nani kakudanganya embe inapendwa na wajawazito wote? unajua maana ya kubeba mimba? wapo watu wanakula hizo embe bila ya kuwa wajawazito, je na wanaume wanaozipenda? ndio nyie mnaowapitia mimba watoto wa watu halafu mnazikataa

    ReplyDelete
  9. mdau uloweka embe la pili pili mjinga sana mimi sina hata mimba wala sijulikani lini nitaipata kuliona tu nimeanza kutokwa na roho ya embe la pilipili rudi shuleni tena ukasome badala useme iwaache wasome kama wenzetu majuu huku amalize masomo wewe ndiyo umeenda kutafuta embe jing sana wewe.

    ReplyDelete
  10. hahahahah mdau ulikuwa unafikiria nn haswa maana hii ni kali mtu kutema mate si kipimo cha mimba

    ReplyDelete
  11. ndugu yangu uko juu kweli yaani hilo embe linatamanisha kweli na wajawazito wote mate yana dondoka wewe mgunduzi wa hali ya juu bigup wasamehe wote wanaoponda maana hawataki kushughulisha vichwa vyao

    ReplyDelete
  12. Haluu... wanajumuiya naona mmemchamba sana huyu mtoa mada.

    Hatahivyo inabidi aeleweshwe kwa kuwa si ajabu ni wengi wenye mawazo kama hayo.

    Inasikitisha ila inabidi nicheke... wadau mada zimeisha au? manake duh... hii kali. Ama kweli hii ni blogu ya jamii na kwenye jamii kuna kila aina ya watu.

    ReplyDelete
  13. Wanaobebe mimba waachiwe ili iweje??Yaani shuleni kuwe na mama na mtoto ndio mnavyotaka??Hiyo sheria ibaki kama ilivyo na iongezwe makali.Uhuru tunaotaka kuwapa watoto wetu wa kike utatutokea puani.huwezi kuacha mambo yawe holela tu.utaratibu uundwe wa kuwawajibisha pia wanaowapa mimba ili washee maumivu.Akitaka kusoma tena ajiendeleze,kuna QT siku hizi.

    ReplyDelete
  14. KUTOKWA NA MATE HAKUTOKANI NA MIMBA NI ENZYME YA MDOMONI INAYOITWA PTYALIN

    ReplyDelete
  15. Naona haka katoto kamewachemsha kweli kweli wazee.....Kameota usiku...kakaona kaitoe ndoto yake kama comment hapa......Anyway...mtoto wa kike akijifungua haipo sababu ya msingi ya kumfukuza shule....kama alikuwa boarding itabidi apate uhamisho wa shule ya day iliyopo karibu na anapoishi...this will never mean promotion ya uzazi mashuleni..kwanza hiyo kero atakayoipata hakuna atakayethubutu kumwigiza.....AENDELEE NA MASOMO NA ARUHUSIWE KWENYE KUNYONYESHA WAKATI WA BREAK......kufa hatakufa ila chamoto atakipata wakati wenzako wanacheza.....HAYA MAMA-MWANAFUNZI nenda kanyonyeshe!....kuwaachisha shule ni kupelekea taifa kujaza wapumbavu nnchini.....Ratiba mbili....MASOMO NA UZAZI...ATALISAIDIA TAIFA KUWATAHADHARISHA WENZAKE!

    ReplyDelete
  16. Ai, Aibu kweli hii Bab TID. Yaani katika karne hii ya Sayansi na Teknolojia bado kuna watu wanamitazamo finyu hivi!!! Embe kipimo cha mimba!!!????

    Mijitu mingine bwana, yaani kwa vile hii ni blog ya jamii basi hata pumba wanaandika tu. Basi watu kama hawa wanalaumu kweli wasipowekwa kwenye blog hata kama wameandika Udenda. Ooh Kaka Michuzi unanibania!! Hivi. Kwani lazima kuandika, si someni walioandika watu. Acha wenye za kuchemka wawasaidie kuwaelimisha watu.

    ReplyDelete
  17. I loved your solution to a serious problem, ie laugh about it, make jokes. But life is serious.Teenage pregnancy is a serious problem. What about suggesting serious sex education lessons, especially to those with little tails.Raw mangoes with pilipili,that is ok according to you, but did you think of what will happen when mangoes are out of season
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  18. Nimecheka !!!!! Sanaaa kwa kweli hii site ukiwa na vijimawazo tembelea michuzi utakutana tu na kichekesho ..!mdau ulolte ahii mad thnks .... Mungu atakulipa kwa kumake people laugh ili waongeze amaisha

    ReplyDelete
  19. Anon wa 1700 am nakuunga mkono na mguu.
    Ikiachiwa wasichana wanaopata mimba kurudi mashuleni nani hatapata. Hivi mmeona huku vyuo vikuu kunakoruhusiwa kuzaa kinachoendelea. Mimba ni fashion na mashindano kila mtu anashindana na mwenzie kubeba mimba, msiniambie wanaweza kuwahudumia hio sio issue, issue ni kwamba masomo haya na mimba na vitoto vichanga haviendi jamani.
    Hawa wa shule ya msingi na sekondari wakiruhusiwa mimba jamani itakuwaje? Sasa hawapati na wanafanya juhudi wasipate kwani wanajua watafukuzwa shule, ikiwa ruksa mtawafanyeje.
    Iendelee kukatazwa ila hao waliopata hiyo bahati mbaya basi atafutiwe alternative elimu.

    ReplyDelete
  20. Kwi,kwi kwi kwi, yaani wewe ulikuwa unataka watu wacheke tu, au kunamaneno uliyokuwa unataka kuongezea ukasahau,maana hata haviendani hivi ulivyoandika.

    ReplyDelete
  21. Ujinga mtupu??!! yaani umekaa na kuacha kufikiria mambo yamaana unaleta upuuzi huu.
    Dunia imebadirika UONEVU WA WANAWAKE UNAFIKIA KIKOMO. As far as I know msichana akipata mimba anaenda kuzaa na anaruhusiwa kuendelea na masomo baada ya kujifungua uamuzi niwake.
    ALIYE MTIA MIMBA JE ANAFANYWAJE? 'It takes two to tango' wewe uliye mbaka, wewe uliye mhonga na kum-seduce, wewe jibaba bingwa wa kudanganya vibinti ADHABU YAKO NINI???
    KAMA WASICHANA WANAPIMWA MIMBA NA WAVULANA WAPIMWE DNA WAFUKUZWE SHULE WOTE??? KAMA NI LIJIBABA LIMEMTIA MIMBA LIFUNGWE KWA KUBAKA.
    ....HAKI ZA BINAADAMU....

    ReplyDelete
  22. Kwa hiyo na binti yako akila embe dizain hiyo tayari ni kitumbo ndwii? au tuseme ndio mmoja wa wale wenye mimba, ungedhubutu kuleta huu upupu humu ndani? siku zote mkuki mtamu kwa kiti moto tu!

    ReplyDelete
  23. Naungana na Naibu Waziri wa Elimu kwamba wanafunzi wanaopata MIMBA washtakiwe. Wakijua kuna kesi mbele yao huku wana MIMBA basi hata kuzipata hawatopata labda kama alibakwa.
    Tunawaachia sana ndio maana nao wanajiachia sana kwa wanaume. Kuanzia sasa wasiwakubali wanaume kabisa hadi wamalize shule, au km vp basi waepuke siku zao za kushika mimba au watumie kinga.
    UKIKUTWA NA MIMBA NI MAHAKAMANI TU NA UTAFUNGWA-HIO NDO DAWA

    ReplyDelete
  24. KWANINI MISHIPA YA SHINGO INAWASIMAMA KWA HIYO ISSUE YA EMBE,JAMAAA AMETOA KAMA KICHEKESHO TU!! nASHANGAA WATU MNATOKWA NA MATE KWA KUONGEA ETI AENDE SHULE.....HAMTAKI WATU WACHANGAMSHE BARAZA..KHAAAH!!



    KIPUSA

    ReplyDelete
  25. wajamani everything has a purpose. mie nadhani mleta mada alikuwa na lengo la kutuchekesha kuliko kutuhamasisha. ameona tumenuna mno na tuko serious mno. lengo ni kuchekesha tu. tusimtoe macho bure!

    ReplyDelete
  26. mimi naona tanzania sheria ya kusimamisha watoto wa kike shule wakiwa wajawazito ni aina ya ujinga wa kimawazo, iwapo huyo mtoto wa kike huyo inabidi amlee mtoto wake na kwa vile elimu yake ni ndogo basi hata maisha yake yanakuwa magumu ...na ukiangalia ndiyo umaskini unavyoendelea kukuwa. Chakufanya nikumuuacha azae na akiwa tayari arudi shule kuendelea na masomo na iwekwe sheria ambayo itasababisha mtoto wa kiume aliyehusika kuhusishwa kwenye kumlea mtoto huyo aliyezaliwa kwa asilimia mia moja bila excuses ya aina yoyote

    ReplyDelete
  27. kabla sijatoa maoni yangu, naomba nieleweshwe ni kifungu gani cha sheria kinasema mwanafunzi afukuzwe shule akigundulika ana ujauzito. Msaada tutani jamani, naomba kueleweshwa na kujulishwa.

    ReplyDelete
  28. BAB TID MWISHOOOO NIMECHEKA SANA NA HAO WALIOKUJA KUKUJIBU NDIO WAMEFUNGA KAZI.

    ReplyDelete
  29. kuna barua ya masharti ya kujiunga na shule za sekondari ambayo inaeleza kwamba uzinzi hauruhusiwi.

    kuna kijana alifukuzwa shuleni kwetu baada ya Mwalimu Mkuu kugundua kwamba alilazwa hospitali akitibiwa ugonjwa wa zinaa.

    sheria za kuwabana wavulana wanaotia mimba zipo, labda hazitekelezwi tu.

    ReplyDelete
  30. Inaelekea wewe hujui kabisa undani wa ujauzito. Si wanawake wote wajawazito wanaotematema mate. Sijui kama umeshawahi kuchunguza hilo. Au ukiona mmoja anatema unadhani wote inawatokea. Na hata wale inao watokea si kwa sababu ya kuona vitu kama ulivyoonyesha hapo juu bali ni mabadiliko ya hormones kwenye mwili yanaweza kumletea mama hali kama hio na inatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Soma vizuri/fanya utafiti wa kutosha vitu kabla hujatoa hoja.

    ReplyDelete
  31. huyu mtoa mada anaonyesha AKILI ZAKE HAZINA AKILI... msimlaumu saana wajameni...

    mdau
    mji mpya kigamboni

    ReplyDelete
  32. KABLA YA KUZUNGUMZIA MIMBA TUKUMBUSHANE NA KUONYANA KUHUSU UZINZI NA UASHERATI.TUKIZISHIKA AMRI ZA MUNGU IPASAVYO, HATUTAZINI, WALA KUFANYA UASHERATI HADI MUDA WA KUOA AU KUOLEWA.KAMA NI HIVYO BASI,HATUTAKUWA NA MIMBA ZISIZO NA WENYEWE. MUNGU ATUSAIDIE TUACHE KABISA UZINZI NA UASHERATI. TUWAONE WAKINA DADA KAMA DADA ZETU...MUNGU UTUSAIDIE KUPAMBANA NA PEPO LA NGONO NA NGONO ZEMBE !!!!UBARIKIWE SANA UTAKAYENIUNGA MKONO.

    ReplyDelete
  33. Utabiri, mithili ya pweza wa Ujerumani!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...