Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi akiongea na wawakilishi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU) kilichopo nchini leo jijini Dar es salaam mara baada ya kufika Ofisi ya Waziri mkuu kueleza kero zao kufuatia maandamano ya wanafunzi hao yaliyofanyika jana kupinga ongezeko kubwa la ada na kuomba wapatiwe mikopo kama vyuo vingine pamoja na kupatiwa ufafanuzi juu ya hadhi na uhalali wa Chuo hicho katika kutoa mafunzo ya elimu ya juu hapa nchini.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU) wakitoa malalamiko kwa Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi juu ya matatizo mbalimbali wanayokabiliana nayo mara baada ya kukutana naye leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi akisisitiza jambo na kuwatoa hofu wawakilishi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU) kuhusu madai yao na kuwataka wawe watulivu wakati serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) na viongozi wa Chuo hicho watakapokutana nao wiki ijayo kutoa majibu ya matatizo yao.
Juu na chini ni wawakilishi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU) wakitoa malalamiko kwa Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi juu ya matatizo mbalimbali wanayokabiliana nayo mara baada ya kukutana naye leo jijini Dar es salaam.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Wadau naomba kuuliza , hicho chuo kipo dar alafu kwanini tena kinaitwa kampala - hapo u fake wa chuo ndounapo onekana.


    mdau china

    ReplyDelete
  2. Kwasabu chuo kina makao makuu Uganda na pale unanda ndio kilipo anzia pale kwa jina hilo la Kampala International University sasa chuo Kimekua kimeanzanisha Tawi hapa Nyumbani sio kama huo ni utapeli ila ni vyema tujue usajili wa chuo hicho na ubora wa elimu inayotolewa na kama walimu wapo n.k

    ReplyDelete
  3. We mdau uko China alafu unauliza swali kama hilo kweli. Kwani kwanini chuo kiko Tanzania au Nairobi alafu kinaitwa United State International University (USIU) au shule iko Arusha alafu inaitwa Moshi International? Chuo kinaweza kuwa na branch nyingi sehemu nyingi duniani maadamu wanavibali vyakufanya hivyo. Jina la chuo haliwezi ku-conclude uhalali wa chuo. However, comments zangu hazilengi kukitetea chuo maana sijafanya research yakusema ni fake or not lakini analysis yako imenishtua.

    ReplyDelete
  4. IFM, ......IFM,........IFM(Dar),.....au CHUO Cha Usimamizi wa Fedha...........mpo???.....Mnangoja nini? Kama wenzenu wanaandamana kutoka walikotoka, na nyie Ikulu iko hapo hapo. Mnasubiri mpaka lini? Hicho ni moja ya Vyuo vikongwe (Estab. 1972). Vingine vimeanza juzi na wanapata hadhi ya Vyuo Vikuu. Kila kitu mnacho. Mnasubiri nini? Au hamuoni umuhimu wa hicho chuo kuwa na hadhi ya Chuo Kikuu???

    Mdau,
    Ughaibuni

    ReplyDelete
  5. Msamehe jamaa bado yupo kwenye nchi ya kijamaa ambapo karibu vyuo vyote vinamilikiwa na serikali.

    ReplyDelete
  6. KUNA WATU WAPUUZI SANA HATA KUFIKIRIA KWAO TABU,YAANI MTU MZIMA NA AKILI YAKO UNAULIZA JINA LA CHUO KWANINI LINAITWA KAMPALA HAHAHAHA WATU WENGINE UNAWEZA KUWATIA VIBAO!!!YAANI KWA MAANA YAKE CHUO KIKITWA DODOMA WAKATI KIPO DAR NI UTAPELI HAHAHAH PUMBAVU KWELI HUYU JAMAA HAPA ISSUE SIO JINA JAMANI MFIKIRIE KWANZA HATA MTOTO WAKO AKIONA COMMENT YAKO ATAJUA BABA/MAMA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU.

    ReplyDelete
  7. Mie sikujua kama wabongo wamelowea China .. wakati wachina wenyewe wanakimbilia Dar kufanya umachinga

    ReplyDelete
  8. Hee hata mimi namsupport mchina kwa swali lake. Labda hamkumwelewa. Hiyo ndio mwanzo wa mtu akimaliza anaambiwa amemalizia shule Kampala international, Uganda kumbe ni hapo hapo Dar..Ukisoma shule katika nchi nyingine sio unaelimika tu darasani bali unajifunza mengi katika jamii pia. Unaelewa vitu vingi ambavyo usingevielewa kama ungekua tu hap Dar...Hivyo mtu atakayesomea kampala anakua na upeo mkubwa kuliko huyo atakayesomea hapao Dar kwenye chuo kinachoitwa jina la nchi nyingine...Je wakimaliza shule wataambiwa waligraduate from Dar es salaam au from Uganda?

    Mimi hapa chuo nilichosoma kina branch kibao lakini kila branch inatoa shahada ya masomo fulani. Hivyo kwa vile nilikua ninafanya double major ilibidi nilivyomaliza couse load ya major moja niende nikakae Chicago kwa mwaka mmoja kumalizia masomo ya major nyingine. Na cheti kinaonyesha nimepata kutoka katika chuo kimoja lakini kila shahada ipo katika miji tofauti...Lakini nilikwenda huko sikupewa tu na kuambiwa nimemalizia mahali fulani...Na ni hapa hapa US lakini nilijifunza mengi sana nilipokua naishi huko

    ReplyDelete
  9. Mh. Lukuvi na jopo lako hongera kwa kuwasikiliza wanachuo hawa, tafadhali endelleeni nao mpaka ukweli na uhalali wa chuo hiki - KIU ujulikane, wazazi tumeshaingiwa na wasiwasi tunajuta hata kupeleka watoto wetu hapo.

    ReplyDelete
  10. sio kichwa cha mwendawazimu...kichwa maji..

    ReplyDelete
  11. nimekumbuka mbali katika picha hiyo hapo juu ni mi Braison Charles kutoka kushoto,katikati ni Emmanuel Biloso mtu wa karatu huyo kwa Dr Slaa.na Alex aka Pinda nikishirikiana na hao vijana pamoja na paul peter,scolar na wengine tulifanikisha kukipatia chuo cha kampala international university hadhi ya constitute college na kushauriwa kuongeza kozi ya ualimu na medicine hadi natoka mwaka2012 niliacha wanachuo waluokuja nyuma yetu wametambuliwa bodi ya mkopo na hata kupata mikopo hiyo.Lakini nimeshangaa juzi kuona wanaandamana na kupigwa mabomu kitengo cha pharmacy,sasa inakuwaje wanaanza kuendesha masomo hayo bila kukidhi vigezo wakati kipindi kile tulipewa mwongozo wote ikiwa ni pamoja na kujenga hostel zenye ubora na kiwango cha kukidhi mahitaji ya wanachuo,kushusha karo na malipo kuwa katika sarafu ya kitanzania,na kutenganisha wanachuo wa open na distance learning na residential student ambao ni senior student toka advanced level kwa kufata kigezo cha GPA kama zilivyoainishwa na TCU GUIDE BOOK.naona haya ni makusudi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...