Othman Michuzi Jr aliyepiga taswira hizi
anasema jamaa wanakaba mpaka penati

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Hapo utakuta jamaa wana PhD zao. Wabongo mtu akiwa na cheti ya MS Word toka pale CC anataka aajiriwe na Daily News. Wengine wanaandamani eti bongo hakuna ajira.

    ReplyDelete
  2. mimi sioni tatizo ya hawa jamaa kuwepo nchini kwetu ! kama watanzania wenyewe ni wavivu , wanapenda ngono na stare TU! wabongo 24- 7 wanawaza ngono tu na stare . wakipewa kazi wanawaza kuiba . Bila kuelewa anapoiba kampuni ikifa anajiaribia mwenyewe!

    WACHINA OOOOOOOOOOOOOOOYE !!!!!!!!!!!!!!!!

    MDAU PARIS

    ReplyDelete
  3. Sijui ule mpango wa waziri mdogo wa wizara ya viwanda na biashara umefikia wapi kuhusu wawekezaji hawa?

    ReplyDelete
  4. HAWAJAMAA NI HATARI SANA LICHA YA KUKABA HATA PENATI WANAKABA MPAKA REFA NA WASAIDIZI WAKE

    ReplyDelete
  5. Bila kuchafua hali ya hewa,picha ya kwanza hapo sio kariakoo,mi nimezaliwa na kukulia kariakoo,naijua kila kona ya mitaa hiyo,lakini hapo sio

    ReplyDelete
  6. Uchochezi wa kibaguzi ndio huu wa kina Othman Michuzi. Watanzania wengi wako nje --Mpaka Zimbabwe wakiganga njaa zao. Hivi watajisikia vipi Othman Michuzi wa huko akiwatoa kwenye blog zao? Leteni hoja zenye mantiki, sio za kibaguzi. China ni nchi inayoendelea kama yetu na wachina wengi tu wana kipato sawa na mtanzania wa kawaida! Wakijitafutia kama hivi kwa nini tunaona wivu?

    ReplyDelete
  7. Wabongo kazi kupiga domo tu wakiona wengine wanaangaika 24/7!

    Wanasema ukimuasha aliye lala ....... ! Sasa kama tunaona jamaa wanajituma hivo kwanini tusiamke kuiga mfano huo? Tuone aibu na tujiulize: jamaa hao wametoka kote kwao mpk Tz na wameona nafasi za kazi , inakuwaje sisi atukuziona na tunapiga domo badala ya kuamka?

    Huo ndio ushindani, kama wanafuata taratibu za uamiaji akuna ttz. Tukumbuke Watanzania kibao wapo nje ya nchi, je wakitendewa hivo tunavyo wafanyia jamaa hawa tutajisikiaje???

    Tujifunze kutoka kwao na tufanye kazi,
    Well done Wachina

    ReplyDelete
  8. Haina kulemba iyo,.mie nataka jua aliyewapa vibali alitumia vigezo gani?njoo zanzibar kwa mchina tambi, ndo utajua hawa jamaa wapo serious kwenye game.

    ReplyDelete
  9. jamani tembeeni muone nyie mnaosema ni ubaguzi nendeni china muone kama mtaishi kwa raha mustarehe wazungu wachina na wengineo ni wabaguzi hasa kwa weusi, msifikiri wa tz walio ulaya america na asia wanaishi kwa kuaribishwa mikono miwili kama sisi tunavyofanya, hawa wachina wakuja kwa njia ya uwekezaji kwa kufungua makampuni makubwa badala yake wanaishia kuuza maduka na biashara ndogondogo.
    na hanjuwi uhalifu wanao fanya wa chinichini wa biashara haramu.
    je mnakumbuka container la wachina lililoanguka baharini likiwa kwenye harakati ka kupakizwa kwenye meli? yale madhahabu na menoya tembo vifaru na ngozi za chui imeishia wapi?

    amkeni toka kwa usingizi mzito nendeni rwanda mkajifunze.

    ReplyDelete
  10. Hi Ancle Michuzi!!

    Mie mnaona junior kafanya la maana sana kutuletea kitu kama hiki katika libeneke hili. Nafikiri mawazo tutakuwa tunatofautiana ial nia yetu wote ni moja.Tukumbuke kuwa maisha ni jinsi wewe unavyoytengeneza na hayajalishi katika nchi ganila muhimu ni kujua mabo matatu tu muhimu:
    1.Kwa nini unafanya au kuamua kutenda jambo au kazi.
    2.Unafanya ili iwe nini.
    3.Kwa sababu gani na kwa ajili ya nani unafanya.

    Mtu yeyote akipata kwanza majibu ya hayo maswali matatu basi huweza kustahimili chochote kile na mahali popote pale. Hii ina Maana kuwa kama Wachina au Wageni wa kutoka nchi yoyote wapo TZ kwa mujibu wa sheria na masharti ya Serikali yetu , basi tuelewe tunatimiza kanuni na sheria za binadamu kimataifa na hatuna haja ya kuwalaumu kwa kujijengea maisha yao kadiri wanavyoweza ili mradi hawamnyanysi mwenyeji wao au kuvunja sheria walizowekewa na serikali yetu. Mimi pia ni mdau niliyopo hapa Europe kama miaka zaidi ya 20 ambaye nimeona jinsi watu wa chi za socialist za zamani kamam , Romania,Bulgaria,Poland nk jinsi walivyokuwa duni kabla ya kuingia kwenye umoja wa Ulaya(EU), lakini walipokuwa wakija huku Ujerumani au tuseme West countries walikuwa radhi kufanya kazi za aina yoyote ile kwa mshahara wa 3,50euro kwa saa, na wenyeji waliwakubali na kuwawajibisha, hatimaye hali ya uchumi ilipoanza kudedea wenyeji wakaamuka na kuanza kuwalalamikia wageni ati wanachukua nafsi zao za kazi,lakini serikali ilipokea malalamikon hayo bila kuwafukuza wageni isipokuwa kwa kuwalazimisha wananchi wao kujitolea kufanya kazi kama hizo hata kwa mshahara mdogo na pia kupitisha kiwango cha chini cha kila aina ya kazi ili kusiweko na tofauti za mishahara kwa kazi ya aina ile ile. Ukitaka kuyaona haya nisemayo kama ni kweli basi angalieni jinsi Ujerumani ilivyoweza kuushangaza Ulimwengu kwa kudumisha uchumi wake kwa muda mfupi kwa kuondokana na world economic crises!
    Kwa ndugu zangu wote Watanzania tusione kila mara wageni ndio wenye kuchukua nafasi zetu za kazi bali nasi tukae chini na tuanze kushirikiana nao ili kuweza kupata pia ujuzi na akili zao kibiashara ,kiakili, kimawazo na kiufanisi, hatuwezi kusema kwamba nchi yetu haiwezi kutegemea misaada kutoka nje wakati sisi wenyewe hatujitolei katika kufanya kazi, kujiwekea malengo na mishahara ya kima cha chini kwa kila aina ya kazi mtu aifanyayo ili imsaidie kimaisha, lawama peke yake haitatufikisha mbali.Tujue moja Uchumi na maendeleo ya nchi yanaendelea kwa Ulimwengu wa sasa kwa mfumo wa kushirikiana kati ya nchi na nchi, wageni na wenyeji,demokrasia ya usawa wa haki za binadamu na sheria za nchi na sasa ni wakati wetu kujua Uhuru wetu tuliupata 1961 lakini kujitegemea wenyewe hatuwezi bado tunahitaji ushirikiano nwa wageni watakao kuishi nchini kwetu.

    Pia tusisahau kuwa TZ ni nchi ya Amani na utulivu, yenye asilimali za asili nyingi sana kama Gold, Diamond, natural Gas,and etc, wakati kuna nchi nyingine hata huku Ughaibuni hazina rasilimali asili hata moja, mfano Ujerumani wao asilimali kuwa walionayo ni Know how(Ujuzi na Uvumbuzi) ambayo sio asilimali ya asili ila ni ya kujifunza kwa bidii na kuwa very creative (Creative country)katika sekta mbalimbali.Nafikiri wanauchumi wataungana nami kuwa Germany inaongoza kwa Uchumi wake duniani kwa kupitia export ya bidhaa zao kwa uimara wake(Made in Germany was created after the second worl war 1945) na sisi tuanza kubadilika kimawazo, tusiwaangalie tu hao wachina ila tuige na kuyachukua mazuri yote wanayofanya kwa faida yetu sio wao tu. Mabadiliko huletwa na wananchi si tunaona yanayowasibu Tunisi na sasa Egypt(Misri)lakini sisi tunahitaji tubadilishe attitude(dhamira ) zetu kuhusu Kazi na ajira, Urafiki na unafiki, Starehe na uvivu, utapeli na Uaminifu, Juhudi na ufanisi na mengine mengi tutakaribia kile kisemwacho maisha bora kwa kila mtu.

    Maneno matupu hayavunji mfupa!!! Haya ni Maoni tu mazuri yachukuliwe na mabaya niachieni mwenyewe!

    Mdau toka Germany

    PS Uncle naomkba usinibanie hili! Asante na kazi njema.

    ReplyDelete
  11. kila nchi jamani inasheria zake., sio swala tu la wageni kukimbilia bila sababu, ilo swala la watanzania wengine wako nchi za watu, wanafata sheria. na sheria ni msumeno, na hao wageni wazibitiwe wafwate sheria za nchi ya Tanzania, ikionekana hawajafata sheria ni khaki kwa taifa la Tanzania, kuwatimua warudi makwao, ni hivyo tu ndugu zanguni kwani na watanzani wengi wanasumbuka kuishi chi za watu bila sheria.Na hao watanzania wanaoishi nchi za watu bila shiria bila shaka nadhani wanangaika sana. jinsi ya kuishi ugenini.

    ReplyDelete
  12. Acheni wachina wanyakue kazi zote kubwa na ndogo ndogo maana Watanzania kazi yetu midomo na starehe kwa wingi,kila siku Mango garden,Leaders club,Billicanas,Ulevi na ngono kwa saana,muda wa kujituma ni mdogo sana kuliko starehe !!Haya ndiyo maisha yetu Watanzania,kazi yetu kulalamikia kila jambo.Kwa mtaji huu Umaskini,ujinga,magonjwa km. ukimwi nk.havitaisha,na Wachina watatajirikia ktk nchi yetu na kutuacha tukistarehe huku tukilalamika !!! !!!
    Mtoa maoni Dar.

    ReplyDelete
  13. Kuhusu Wachina, tuzungumze mengine na la ngono tuliache kando. Mnafikiri wanavyozaana kwa wingi hizo mimba zinatoka kwa 'roho mtakatifu', kiasi kwamba wamewekeana sheria ya kutozaa mtoto zaidi ya mmoja!!! Sasa hivi idadi yao inakaribia bilioni 1.5!!!

    ReplyDelete
  14. wewe mtoa mada ulisema hizo picha sio kariakoo, kumbe ni za wapi chumbani kwako ? hio picha ya chini ni kariakoo tena msimbazi karibu na police station , na ya juu bado sijapaelewa, any way mada ni WACHINA na sio mtaa gani ... wabongo bana ...bichwa zero

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...