Katibu Mkuu wa Chama cha (Tanzania Association of Managers nad Owners of Non -Government Schools and Colleges) ndugu Benjamin Nkonya kushoto na kulia ni Mwenyekiti wa Chama hicho ndugu Jerry Nyabululu wakizungumza na Waandishi wa Habari ambao hawapo kwenye picha ,kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam leo kuhusu matoke ya kidato cha nne mwaka 2010 yafutwe, na Mitihani isahihishwe upya , kwani utaratibu wa usahishaji wa mitihani hiyo ulichukua muda mfupi kwa sababu ya Bajeti ya Baraza la Mitihani kuwa finyu kwani vyanzo vya mapato vimepungua ni baada ya Serikali kuondoa Ada ya Mitihani kwa Shule za Serikali,hivyo kufanya Baraza kuwa na uwezo mdogo wa kusimamia kazi ngumu ya kusahihisha Mitihani ya Nchi nzima.Picha na Anna Itenda -Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Mnawanyonga walimu kwa mishahara midogo huku sehemu kubwa ya pesa mnatia mifukoni kwenu,hivyo mnategemea miujiza itokea kuwafaulisha wanafunzi.

    ReplyDelete
  2. Mlikuwa wapi kukataa Mtihani wa Form two ulipokuwa unaondolewa?
    Leo hii matokeo mabaya mnakuja juu?
    Mlikuwa wapi Kipindi cha waaliu kudai Maslahi?

    ReplyDelete
  3. Mh sasa Tanzania tunaelekea kubaya, tunamhitaji Mungu wetu kuliko kawaida, sijawahi kuona matokeo mabaya ya mtihani kama mwaka huu, wanafunzi waliopata Div 0 idadi yao ni kubwa kuliko waliopata Div 1-4? Hii ni hatari sana. Kama inawezekana kurudia kusahihisha hiyo mitihani sawa ila kama haiwezekani basi wafanye utaratibu wa kurekebisha haya matokeo. Yanatisha. Halafu kitu kingine mara nyingi watu wanasingizia mishahara kuwa midogo kwa walimu, jamani mimi ninaamini kwamba mwalimu anayeshindwa kufundisha mtoto eti kwa vile analipwa sh 100,000/= hata ukimpa million (1,000,000/=) bado hataweza kufundisha. watu wamekuwa na visingizio tu vya pesa mishahara kidogo, usitegemee utendaji kazi kuwa bora kwa kuwa pesa imeongezwa, haiendi hivyo. Lazima watu wajifunze kuheshimu kazi na kuacha kuiba mishahara kwa kutokufanya kazi zao, kama mshahara mdogo si mtu aache kazi atafute inayolipa vizuri. Kama unakubali kufanya fanya kwa moyo. UALIMU ni wito ila siku hizi tunazoa kila kilichosalia ndio hao wanakuwa waalimu. Tubadilike.

    ReplyDelete
  4. WIZARA YA ELIMU IPEWE HAKI SAWA NA WIZARA NYINGINE,WALIMU WANAPATA SHIDA MNO MNO.UTAKUTA MWALIMU ANATOKA KUFUATILIA MSHAHARA WAKE WILAYANI HATA SIKU 2 JE MNATARAJIA NINI?MSHAHARA WENYEWE KIDOGO MNO UNAPOKEA SIKU HIYO HIYO UNALIPA MADENI UNABAKIA MTUPU,UKIRUDI KAZINI BADALA KUFUNDISHA KWA HAMU,UNAKUWA UNAWAZA UTAISHIJE BILA PESA NA MAHITAJI MENGINE.JE?UNATARAJIA MTU KAMA HUYU AWAFUNDISHE WATOTO WAFAULU?
    BASI WAKUBWA WA SECTOR HII WAKAWAFUNDISHE WANAFUNZI NYIE WENYEWE ILI WAFAULU.MDAU LONDON.

    ReplyDelete
  5. Hawa jamaa wanachekesha sana, baada ya kutafakari nini kimesababisha wanafunzi wao wafeli wao wanataka mitihani isahishwe upya kwani hata akija malaika kusaisha hiyo motihani ndo atampa maksi mtu aliyejibu 2+2=7. Poor Management na ndo mana shule zenu zimefeli pumbavu...! Pangeni strategies za kurekebisha makosa next year sio mnaleta longolongo kutetea madudu. NECTA oyeeeeeee na Mama Ndelichako Juuu Juuuu zaidi. Hii ndio shida ya kuchanganya Siasa na Mambo ya Msingi

    ReplyDelete
  6. Du hii kali ya mwaka nilipokuwa shule ya sekondari kulikuwa na usemi
    Usemao Division ngumu kupata level ya form four ni Zero na One na ilikuwa kweli so
    How come Zero zimekuwa nyingi hivyo!! Mi na wewe hatujuhi na wasika
    Nao Hawajuhi?Pumbavu watoe sababu zinazoeleweka ndani ya Siku
    Saba za kazi kosheria.

    ReplyDelete
  7. Kikubwa hapa tunatakiwa tuanzie chini kabisa kwani kinachotatiza ni lugha. Mtu anasoma KISWAHILI miaka saba(7) halafu anaanza kusoma masomo kwa ENGLISH miaka nne(4) atawezaje kuelewa? Na kule hawafundishi kizungu isipokuwa masomo ndo yanafundishwa kwa kizungu,sasa hapo hatuoni kuwa ni tatizo! Somo la KISWAHILI libaki kuwa hivyo isipokuwa masomo yote yafundishwe kwa kizungu.

    ReplyDelete
  8. Hawa wanaopendekeza mitihani isahihishwe upya wana elimu gani vichwani mwao?? Wangetuambia kama wana tuhuma zozote kwa waliosahihisha mitihani, hapo tungelifanyia kazi hilo, na tungependekeza wasahihishaji wengine.
    Lakini hata mitihani ikisahihishwa mara kumi, ni vigumu na ni hatari kwa msahihishaji kumpa mwanafunzi alama ya kupata wakati amekosa.
    Hawa jamaa wangepewa fursa ya kusahihisha wao, mwanafunzi aliyeandika 2+2= 7 wangempa maksi 20 ili mwanafunzi huyo asifeli mtihani na kulitia aibu taifa hili lenye mafisadi wengi kuliko Wazalendo.

    Abiola Jr, Mikanjuni Tanga

    ReplyDelete
  9. Wee anonymous hapo juu hujui unachosema ndio maana unasema. Wee nenda kapokee huo mshahara wa laki moja halafu ufundishe watoto kwa juhudi zote...Na msahara wenyewe unaufuata mkoani kila mwezi baada ya week mbili kuchelewa. Na bado unafamilia na kazi ya ualimu inahitaji dedication and preparation. Hawana muda kwa vile muda wao wote ni kufuatilia mishahara yao na kukaanga mandazi kusuppliment mishahara isiyotosha...

    Tanzania tunatakiwa tujifunze bila walimu hakuna elimu. Na elimu ya awali ndio foundation ya mtu yeyote...Nyie mnaoweza kusomesha watoto kwenye shule nzuri na kuangalia nje ya dirisha na kusema huyo sio mtoto wangu aliyefell basi kwa taarifa yenu hao watoto ndio taifa la kesho. In one way or another mwanao atakuja kuishi, kufanya kazi na hata kuoa au kuolewa na huyo unayemchungulia tu wa dirisha..We need to wake up...Watoto wakiwa hawana akili basi na taifa letu litakua, taifa gani? Just imagine rais mwenye div zero namake hao watoto wa wenye zao kesho wataondoka na kupelekwa nje watakao baki hapa ni hao hao waliofell....

    ReplyDelete
  10. "Lazima watu wajifunze kuheshimu kazi na kuacha kuiba mishahara kwa kutokufanya kazi zao, kama mshahara mdogo si mtu aache kazi atafute inayolipa vizuri."

    Hii hoja ni nzuri sana kama itawahusisha watendaji wote wa serikali - kuanzia kwa rais hadi kwa katibu kata, pamoja na waheshimiwa wabunge. Kama ni kuiba mishahara kwa kutofanya kazi ninafikiri tuanzie na Ikulu, tushuke hadi wizarani, hadi halmashauri za wilaya na miji. Ninakuunga mkono.

    ReplyDelete
  11. mtihani utungwe ndani ya silabas na si vinginevyo. masomo yenye silabus nyingi yafanyiwe mtihani kwa awamu. silabus zigawanywe mara mbili then watoto wafanye mitihani awamu mbili.
    system nzima ya mitihani inabidi ibadilishwe, including marking scheme

    ReplyDelete
  12. Hivi akifeli mwanafunzi, wa kulaumiwa nani? Serikali, mtoto, wazee walimu au shule. Maana mchango wa wadau wote hawa ndio wanaochangia ufahamu na ufaulu wa mwanafunzi. Kuna mwanafunzi anasoma Marian Secondari, nimemsikia akisema kwamba jina la shule hiyo linakuzwa na wanafunzi na sio waalimu wala shule yenyewe ila ni wanafunzi wenyewe ndio wenye jitihada. Wanasena wala hawana walimu wazuri ila wenyewe wanasoma kweli of course katika mazingira ya utawa na wao wana muda mwingi wa kujisomea na kupumzikia. Wanajitafutia past papers wao wenyewe na kusaidiana kuzisolve wao wenyewe. Hawa Marian wanachukua wasichana waliofaulu kiwango cha juu na wanaofanya mtihani wao wa kuingia form I ni wengi sana wanafikia 2000 lakini wanachukua 70 kama sikosei, ina maana wengine wamefeli? Sifikiri.

    Lakini tukiliangalia upya suala hili, tangu kaingia huyu mama Ndalichako Baraza la Mitihani kiwango cha kufeli kimekuwa kikipungua kila siku na sasa kimefikia kikomo, sasa ni Wizara, Shule, Baraza Walimu, wanafunzi. Wao wanatakiwa watoe changanua la kina kueleza wapi pana weakness katika uelewa wa wanafunzi, katika kujibu masuala mitihani. Au ndio njama tu za kusingizia serikali ambazo zenyewe zina shule za vipaji na miaka yote huwa wanatoa matokeo mazuri ghafla zidondoke kwa sababu eti mishahara, vile vile private schools zipo nyingi na wao vile vile wanachukua 'CREAM' inafaulu nyingine hazifaulu zinazongoza kufaulu ni seminari, HAPA IPO NAMNA LAKINI IKO SIKU SIRI ITAVUJA.

    ReplyDelete
  13. hawa wamechemsha tu. hoja ya msingi haipo. wanaopinga mishahara ya walimu kwa ni chanzo cha matokeo mabaya wanatatanisha ufahamu wao. mishahara kuwa midogo inasababisha walimu wasiconcetrate na kazi na badala watafute mapato mbadala, walimu wananingia kama kawaida ila hawana hamasa ya kufundisha.
    kuna haja ya shule pia kuwa na mazingira bora, sidhani kama mtu anaweza kufanya vyema katika hali ya maisha ya shule zetu. no maabara, umeme hakuna.n.k shule inahitaji concentration kwa vijana kusoma kweli na walimu kuwafundisha kweli.
    lakini tusitafute mchawi ukweli ni kwamba elimu tumeicha katika mikono ya wachache na serikali kutoitilia mkazo ndo matokeo yake hayo. kwanini shule nyingi za private matokeo yanaridhisha kuliko za serikali?

    ReplyDelete
  14. Mtoto wa CoastFebruary 02, 2011

    Sababu iliyotolewa na Chama haijitoshelezi:
    Wangesema kuwa wana ushahidi wa Mitihani kutosahihishwa vyema au kuwepo tuhuma za upendeleo au kutotenda haki na si tu suala la muda, maana unaweza kuwa na muda mrefu bado pia ukasahihisha mtihani vibaya! hapo wapo?

    Aidha kwa nini tulikuwa hatujasikia toka kwa WALIOSAHIHISHA MITIHANI hiyo mmoja mmoja au kwa pamoja wakilalamika juu ya kutokuwa na muda wa kutosha ktk kazi hiyo, mpaka matokeo yametokea? Je yangekuwa mazuri bado Chama hiki kingeshauri kufuta matokeo hayo kwa sababu wanazozitoa hapa?
    Je wanataka kushauri kuwa kwa kukosa muda Wasahihishaji walikuwa wanaamua kuwafelisha watahiniwa bila kusahihisha? Kama ni hivyo hili si tu la kufuta mtihani bali linakuwa la kuwafuta kazi hao Wasahihishaji na hata kuwafikisha mahakamani kutokana na walichokifanya kama ndivyo mnamaanisha?

    ReplyDelete
  15. Siri ya kufaulu mitihani ni displine wadau…… angalia shule zote za top ten bora kila group utaona wanashea on common siri displine. from head masters to wapishi hata kama mishahara wanalipwa late majuma mawili. I happen to be in one of those shules enzi hizoo. wadau mateacher wabovu kiaina na rushwa huku ni kwenda mbele vibosile wote wanahonga kila mwaka wanao kwenda huko. startegy ni half vichwa nature bright alafu wengine mlango wa nyuma. just look closer you will know the secret. wadau na wenye inchi wanajua siri they just keep for their kids to take over were they left. raia wema wanajionea hawafai kwavile walipata divison zero. Ebwanaa wee tume be set up. wakifix system nafasi zao wanao hawatachukua kina jamaa wakijiweni pia watapigania. Ndio maana jamaa wakijiweni wataka apate zero alafu kinanahii wanajijua wanapata fulsa zote, falsa za kuongoza kama kawaida na hizo division za daraja la kwanza. Alafu tunasema elimu sawa kwa wote hapo kuna usawa kweli au double standards of high quality. vitu vingi bongo haviopareti kama vinavyotakiwa kuopare. Nikama karata tatu kamali. unawini round ya kwanza unalooose round nyingine zote. Tunaingizwa mkenge kila siku. Leo nitaishia hapo.
    Wasalaaam,
    Window Watcher,.
    somewhere on earth.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...