Hapa ni katika eneo la kuondokea abiria uwanja wa ndege wa kimataija wa Julius Nyerere jijini Dar. Hebu cheki huko juu kulivyomeguka. Wananchi wengi wanajiuliza nini kazi ya mapato yanayopatikana uwanjani hapa ikiwa ni pamoja na pesa kibao zinazotokana na kuingia na kupaki magari, kodi kibao za uwanjani na kadhalika. Uongozi wa uwanja huu muhimu mpoooo??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. Watu mnaona kweli, yaani mimi napita hapo mara kibao lakini sijawahi kutizama juu kukoje, Hongera sana endelea kukagua sehemu nyingine maana tunaaibika ukizingatia hiyo ndio njia ya wageni wetu wote wanaoingia na kutoka nje ya Tanzania.

    ReplyDelete
  2. hio roof iko hivyo siku nyingi sana, mbona wasafiri wameshajizoelea, napenda kuamini labda kuna sababu za kitaalamu kwanini halijazibwa, "ventilation" or sina uhakika

    ReplyDelete
  3. Hatuna viongozi wala watawala, hii kazi kweli sijui ni nani aliyetuloga tukawa wapamabvu kiasi hiki. Ubabaishaji mtupu.

    No leadership, no managerial skills, is a perfect storm for backwardness and primitive ways of living. Its a shame that people in positions of power never change for good. Damn corruption is destroying this country. Nobody gives a damn anymore. I'm just about to wash-off my hands on this country.

    ReplyDelete
  4. ISSUE ZA AINA HII KWA BONGO UTAPATA KICHAA UKIFUATILIA. SIKU UKIONA SEHEMU IMEKAA SWAFI HAPO NDO PA KUSHANGAA ILA HALI KAMA HII NI YA KAWAIDA KABISA KWA UZOEFU WANGU MDOGO NILIONAO JUU YA BONGO.

    ReplyDelete
  5. it is squarely lack of leadership skills.

    ReplyDelete
  6. WAACHE KUJIENDELEZA KWA MANUFAA YAO WAJE WAKATENGENEZE AIRPORT,UNACHEZA NINI NA VIONGOZI WETU WANAPITA HAPO HAPO KUSAFIRI KWENDA NJE KWA RAHA ZAO LAKINI MASWALA KAMA HAYA HAYAWAHUSU,WAO WAJINUFAISHE NA WATOTO WAO WAKASOME NJE WANASHIDA GANI KAZI KWENU MASIKINI ILA TUMEFUNGUKA MACHOOOOO,NCHI HII SHIDA TUPUU KILA KITU TABU MAISHA MAGUMU INANIUMA BASI TUUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  7. Nimepaona hapo Juzi tu na nikaamua niwe mpole. Nchi yooote imesinzia kuanzia Ikulu hadi uwanja wa ndege. Kila mtu anaangalia la kwake...shame on Tanzania Government

    ReplyDelete
  8. Muulize Lyimo na Chawene wanajua kakarabati choo tu milion 7 lakini cjui hapo utaambiwa tzs ngapi kaka wezi wakubwa

    ReplyDelete
  9. Sasa wewe ulitegemea vipi? Wafanyakazi wa serikali wanapata mishahara midogo, lakini matumizi yao makubwa. Hizo pesa zinatoka wapi? Tena hao sheria hawagusi maana wanajua kula na wenzao.

    ReplyDelete
  10. Wewe anony wa saa 11.28 unapita mara kwa mara ukienda wapi? Nitakuumbua shauri yako!

    ReplyDelete
  11. KWA KWELI NI KITU CHA KUFADHAISHA TAIFA LA TANZANIA KUSHINDWA KUZIBA SEHEMU KAMA HIYO AU NDIO TUNASUBIRI MFADHILI PIA AU MWEKEZAJI KWA SEHEMU HIYO NDOGO AMKENI JAMANI,HIZO SUTI MNAZOVAA NA HAYO MAGARI MNAYOENDESHA MAZURI NA MAJUMBA MAZURI MNAYOISHI NA ELIMUNZURI MNAZO WAPA WATOTO WENU ZINATOKA HAPO KWA HIYO MUWAJIBIKE.

    ReplyDelete
  12. MIMI NINGEONELEA LINGEJENGWA BANDA KUBWA LA MAKUTI KUUUBWA ILI TUWE HATA WANANCHI TUNGEWEZA KUCHANGIA KULETA MAKUTI WAKATI LIKIVUJA HILO BANDA NA PIA INGESAIDIA KWA HALI YA HEWA MAANA HAPO SEHEMU JOTO LAKE SI MCHEZO NA VIYOYOZI MARUFUKU HAPO KWENYE SEHEMU YA KUCHUKUA B.PASS,ASANTE

    ReplyDelete
  13. Jamani BONGO kaazi kwei kwei.sasa kodi za hapo uwanjani zinaendaga wapi?safari bado ndefu mnooo,mimi binafsi nina kila sababu ya kutokuwa na mzuka na hii Nchi khaaa!!!

    ReplyDelete
  14. Nguvu ya uma inahitajika sasa pasi kusita kabisa!

    ReplyDelete
  15. Mh, Mi nadhani panya wengi, labda wameweka wazi makusudi ili iwe kivutio kimojawapo kwa wageni wanapoziona zikipitapita juu,nawapongeza sana,maana niwabunifu wazuri.

    ReplyDelete
  16. Michuzi, unakumumbuka tulipokuwa tunakwenda Airport 'assignment' wakati Airport bado jipya. Enzi zile ulikuwa unaweza hata kwenda juu (balcony) kuangalia ndege zikiruka/watu wakishuka kwenye ndege. Ilikuwa 1987 na airport bado iko vile vile....HAKUNA MAINTENANCE! Wanajenga halafu basi tena sijui mpaka ianguke.

    ReplyDelete
  17. Nani kasema Viongozi wanapesa hapo labda Viongozi hao wabunge Serikali wanapita Geti jengine kama sio Airport ya zamani.... kama mdau alivyosema ukikaa bongo unaona kawaida na ukipita sehemu safi unaona maajabu. Ni tabia tu ambazo zimetukalia muda mwengine tusisubiri kufanyiwa ni wenyewe tu kuamuwa sawa na Nyumbani mbele ya geti mtu anaona sio pake kwa kusafisha mazingira.

    ReplyDelete
  18. Hizo pieces zinazoning'inia juu ni health and safety hazard to start with.Hata hao wafanyakazi walitakiwa wasikae hapo karibu. Ni aibu na kusikitisha. hakuna anewajibika. Viongozi kula na kunenepa nchi inateketea.

    ReplyDelete
  19. Michuzi usibanie hii, wewe unamuuliza nani hili swali wakati wewe unauwezo wa kwenda hadi kwa wahusika na kuwauliza wanfikiria nini? Sasa wakiweka kiwanja vizuri, misaada haitakuja, inabidi watowa misaada waanze kuona ubovu kuanzia wanpoteremka kwenye ndege. Sasa unafikiria chukuwa chako mapema kitapatoikanaje kama kama pesa itakwenda kutengeneza uwanja wa ndege ambao watu wanpita tu hakuna kulala. Hongera umegunduwa hilo. Hilo tatizo ni sawa na tone la maji kwenye bahari. Matatizo yetu ukiyalinganisha ni sawa na bahari ya hidi hujui uanzie wapi uishie wapi. Hakuna anejali zaidi ya kujali matumbo yao.

    ReplyDelete
  20. Wamekaa kwa maofisi tu na matumbo yao vile makubwa,kazi ndogo tu kama hiyo mpaka wasukumwe. Pumbafuuuuuuuuuu sana!

    ReplyDelete
  21. SASA HIYO NDIO INTERNATINAL EIRPOART, KWELI NYINYI WAFRICA AKILI ZENU MKIAMBIWA KIDOGO MSKATAE, NINI HII SASA, HAPO NDIO GATE WAY KWENDA SEHEMU MBALIMBALI ZA ULIMWENGU TEANA ZILIZOENDELEA, SI MNACHEKWA IOI AIBU WEEE.HAHAHA....

    ReplyDelete
  22. Kwa kweli hiyo hata haistaili kuitwa Air Port, hivi kweli serikali haiwezi kuwa na vision kila mwaka inatenga badget ya kujenga uwanjwa mpya wa kisasa? Ukienda katika phases?
    Hii ni karne ya 21, lazima tuwe na miundo mbinu ya maana kuweza kukompete na wenzetu, la sivyo tuaachiliwa mbali.

    ReplyDelete
  23. Dah!! Mungu ibariki Tanzania, tunaimba karibu kila siku,ila kamwe mungu hawezi kutubariki kama sisi wenyewe hatuonyeshi kutaka kubarikiwa!
    embu tuseme ukweli ndugu zangu, kama hiki ndicho kiwanja kikubwa cha kimataifa chenye heshima ya marehemu baba wa taifa kipo hivi, vp kuhusu hivyo vingine huko?embu tujiulize kwa kutafakari kwa ukweli kabisa,NI WAPI AMBAPO KAMA MTANZANIA UNAWEZA KUJIVUNIA MIMI NI MTANZANIA UKIWA KIFUA MBELE!yaani kila kona ni matatizo tu!
    Mungu tuokoe kwenye haya mabalaa
    AMIN

    ReplyDelete
  24. Tanzania mwendelee kutembea mwendo wa pole, wenzenu wanatumua mbio...aibu tupu..hebu jaribu kupita airport za wenzetu..hakuna uchafu hata kidogo....nashangaa Tz...eti..mwalimu JK Nyerere int airport...me naona waondoe hilo jina wanamdhalilisha baba wa taifa, yeye hakuwa corrupt hivi. Viongzi wanakula tu hela ya walipa kodi hebu jiulize mapato yote hayo yanakwenda wapi..hata ukarabati mdogo haupo. Aibu tupu, juzi tu baada ya kushuka kwenye ndege abiria pamoja na uchovu wote tumesubirishwa saa moja hadi kuchukua mizigo yetu,hamu yote ya kuonana na wapendwa wanaokusubiri wakupokee inakuwa imeisha. Wafanyakazi wenyewe wako veeeeery slow...Tz hadi ipite fagio ya chuma ndo watu watashika adabu..hapo sasa tujiulize nani atakayeweza kupitisha fagio hilo. Hivi mawaziri na viongozi hawapiti hii aiport wajionee. nyanja zote tuko hoi Tz..why?..lini tutajaribu hata kuiga tu vya wenzetu?..AIBU KABISA

    ReplyDelete
  25. Wewe anym wa Feb 18,03;52:00 pm. Niumbue tu ndugu yangu, ruksa kwani siku hizi kila mtu anauhuru wa kusema alichonacho moyoni kwake. Napita mara kwa mara kwaajili ya kufuatilia mambo ya utafiti wa masomo yangu.

    ReplyDelete
  26. dah wananchi mimi nilikuwa nje miaka zaidi ya mitano na mara nyingi nikiangaliaga facebook naona watu wameng'aaa nikajua watu na nchi kuna maendeleo,dah siku niliyotua airport umeme ulikuwa umekatika,kulikuwa na jotoo balaa,afu gizaaaa du,jamani hata zile toroli chafu sana,jamani eeh jiungeni www.pamojasms.com mlio nje ili muwaambie wenzenu,kusema ukweli kunatia huruma saana tena saana.

    ReplyDelete
  27. ni mabomu yalofanya hivo....

    ReplyDelete
  28. Hio sehemu yote iko mbioni kufanyiwa ukarabati mkubwa sana. Fedha ziko tayari na michoro ipo ila ugumu upo jinsi gani kuufanya ukarabati huo bila kuathiri shughuli za kila siku za sehemu hio. Kwa sasa sehemu hio inahudumia watu zaidi ya uwezo wake kutokana na wingi wa ndege kwahio sehemu ya departure ikifungwa itapunguza zaidi uwezo wa kuhudumia abiria. Ukarabati huo utaanza siku za karibuni sambamba na ujenzi wa terminal 3.

    ReplyDelete
  29. ACHENI UJINGA.. MABOMU YAMEFANYA HIVYO.. MIMI NAPITA SANA HAPO KWENDA MAREKANI.. NYIE MNAONGEA HATA PASSPORT HAMNA.. EMBU KAPANDE BAJAJI..
    NDIO CHOO KINACOST .. NA BADO.. TUTACHUNA SANA.. WE LALA HUKO KEKO SISI TUPO MIKOCHENI NA MAJUMBA MBEZI.. KAA CHONJO..LOL
    KIONGOZI WA WABEBA MABOKSI
    CALIFORNIA MAREKANI
    KARIBU NA MUNGU

    ReplyDelete
  30. wewe mdau wa CALIFORNIA marekani...sasa nani kakuuliza kama unapita kila siku hapo...eti hamna passport una uhakika gani kama waliochangia hapa hawana passport.acha hizo wewe kama uko uko MAREKANI mbona poa sio ishu sana wewe kuwa huko!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...