Ankal akiwa na mtangazaji mwandamizi wa Voice of America Bi. Khadija Riyami aliyeongozana naye White House jijini Washington DC leo tayari kuanza kazi ya kuripoti kutokea Ikulu hiyo ya Marekani, akijaza nafasi iliyoachwa wazi na Mh. Juma Nkamia, ambaye sasa ni Mbunge wa Kondoa.
Ankal ameiambia Globu ya Jamii usiku huu kwamba wadau wake wala wasiwe na hofu kwani libeneke litaendelea kama kawa kwani kaacha timu kubwa ya kuendeleza libeneke na wakati huo huo atakuwa akileta mambo moja kwa moja toka sebuleni kwa Obama. VOA wamekuwa wakimzengea sana Ankal ili akafanye kazi kwenye idhaa hiyo ya Kiswahili upande wa habari za mtandaoni.
Ankal ameiambia Globu ya Jamii usiku huu kwamba wadau wake wala wasiwe na hofu kwani libeneke litaendelea kama kawa kwani kaacha timu kubwa ya kuendeleza libeneke na wakati huo huo atakuwa akileta mambo moja kwa moja toka sebuleni kwa Obama. VOA wamekuwa wakimzengea sana Ankal ili akafanye kazi kwenye idhaa hiyo ya Kiswahili upande wa habari za mtandaoni.
Ankal akielezea mambo ya libeneke kwenye ukumbi wa mkutano wa White House baada ya waandishi wa White House na wa nchi mbalimbali kumuomba aelezee jinsi tasnia ya habari ilivyo Bongo kwa hivi sasa, hususan swala la kuibuka kwa 'vikombe' karibu kila kona ya nchi. Ankal aliwaambia kwamba ni kweli kumezuka watoa dozi sehemu kadhaa lakini hadi sasa Babu wa Loliondo ndiye anayetamba kuliko wengineo wote. Ankal alipata wakati mgumu sana kuelezea ni namna gani kikombe kimeshika hatamu Bongo.
Ankal akivinjari kwenye viunga vya White House
jijini Washington DC baada ya kutoa mada ya vikombe
Ankal akiwa ofisi za masuala ya nje ya Marekani (State Department) ambako ndiko ziliko ofisi za Bi. Hilarly Clinton. Kazi yake ya kuripoti habari za Ikulu ya Marekani huhusika na ofisi hii pia. Ameiambia Globu ya Jamii kwamba anamshukuru Mungu kwa 'kudakwa' na VOA na hivi sasa anajiandaa kupigana vikumbo na wanahabari wa dunia. Kasema ana uhakika kwamba endapo kama mambo hayatokua mswano ataingia mtaani kubeba boxi.
jijini Washington DC baada ya kutoa mada ya vikombe
Ankal akiwa ofisi za masuala ya nje ya Marekani (State Department) ambako ndiko ziliko ofisi za Bi. Hilarly Clinton. Kazi yake ya kuripoti habari za Ikulu ya Marekani huhusika na ofisi hii pia. Ameiambia Globu ya Jamii kwamba anamshukuru Mungu kwa 'kudakwa' na VOA na hivi sasa anajiandaa kupigana vikumbo na wanahabari wa dunia. Kasema ana uhakika kwamba endapo kama mambo hayatokua mswano ataingia mtaani kubeba boxi.
April 1st == fools' day !!
ReplyDeletemichu sikuwezi....kila mwaka kwenye fools day lazima ulete kitu kipya..sawa bwana ha hah a ha ha aha aha
ReplyDeleteHII IMEKAA KI APRIL FOOLS DAY ZAIDI...!!! poleni woote mliouvaa mkengezz
ReplyDeletemdau canada
Hongera sana uncle yetu, Mungu azidi kukufungulia, ukipata wewe na sie tumepata! tumefurahia sana mafanikia yako!!
ReplyDeleteNANA
Kila la kheir, umeweza ngazi ya moja utaiweza na nyengine - Amin.
ReplyDeleteUnatuwakilisha kwa hivo tutafata nyayo zako.
Anko ulikwenda kwa Loliondooooo nini?
Asante
Hongera kwa kuwapata watu na APRIL FOOL HII!!!... :D hahahaha
ReplyDeleteWadau leo ni sikukuu ya wajinga isije ikawa Ankal anatudanganya??????
ReplyDeleteHappy April Fools Day Uncle Michuzi.
ReplyDelete...April Fools day. Dah, umewapata wengi sana leo
ReplyDeleteSikujua kuwa Ankal ni mwandishi wa habari wa ku report. Nilikuwa naelewa kuwa yeye ni photo journalist, mwanahabari zaidi katika picha. Hongera zako Mkuu, tutakuwa tunapishana kwenye corridor za White House maana wengine huko ndipo kibarua chetu cha u Jack Bauer. Mwezi Machi naona umepita haraka sana, kumbe leo ni tarehe 1 April?
ReplyDeleteTAARIFA MUHIMU KWA WADAU WA LONDON na UK - KUANZIA LEO JIONI (SAA 12 JIONI) PASTOR KIJIKO WA SEVEN SISTERS ALIYETUNUKIWA NA ROHO SAFI KUFANYA SHUGHULI YA KUTOA TIBA, ATAANZA KUGAWA KIKOMBE (£0.50p only)KWA WATU WENYE MATATIZO NA MARADHI MBALI MBALI. TAFADHALI WASILIANA NAYE: BONGO BAR, 65-67 BROAD LANE, LONDON N15 4DJ.
ReplyDeleteHUU NI UWEZO WA MWENYEZI MUNGU TUU.
Siku ya wajinga nadhani umeshawatia changa la macho wajinga big up.
ReplyDeleteHappy Fool's Day kaka.
ReplyDeletewap michuzi haya mambo ya cku ya wajinga cyo,,,we mkal kaka,,,kwan nkamia kashaacha kaz mda mrefu mpaka leo wamekuchukua wewe????????kwel kaka we noma umewashika wajinga
ReplyDeletehongera kk mungu akupe wepesi
ReplyDeleteApril fool nyinyi
ReplyDeletepambaf
THE END JUSTIFIES THE MEANS...ANKAL....HONGERA SANA BROH...!!
ReplyDeletejeffmsando@yahoo.com
Ongera kaka
ReplyDeleteMimi hujanipata, happy April fools day!
ReplyDeleteYa mwaka huu kali lakini naona wengi wameamini!
ReplyDeleteHii imekaa kama vile story ya April 1, ujue sisi ni watu wazima kuanza kutuimbisha nyimbo za fools day, ohoooooo!!!
ReplyDeleteHa ha ha, hamna kitu mIchuzi, unatuzingua! APRIL FOOLS!
ReplyDeleteLeo sio siku ya wajinga kweli?nadhani anatania hapa
ReplyDeleteIs it april fool day or not, any way congraturation
ReplyDeleteAnko umewapata wajinga kibao
ReplyDeletelol, ckukuu njema
april fools day
ReplyDeletei reserve my comment mpaka siku ya wajinga iishe!
ReplyDeleteApril fools day umewakamata
ReplyDeletehongera mzee Michux
ReplyDeletemwambie Obama uje nae kwetu aje kutuletea angalau maendeleo
ila nafikiri hii umeitoa bcz of foolday mmh
kweli au april fools day!!!!
ReplyDeleteHii ni kwel ankal au ndio ya mambo ya leo tarehe 1 aprili
ReplyDeleteMichuzi!!! Leo ni siku ya wajinga
ReplyDeleteAnkal, leo siku ya wajinga...humpati mtu!
ReplyDeletehv leo si ni cku ya wajinga au????????
ReplyDeleteHongera Ankali ila naona utawapat wengi april fools day. ila mie nakuombea one day yes upate nafasi kama hiyo
ReplyDeleteApril fool!
ReplyDeleteFools Day!
ReplyDeleteHappy April Fool Day!
ReplyDeleteany other day i would believe it, but on april fools day...i don't believe it... let us wait and see
ReplyDeleteleo si siku ya wajinga jamani......
ReplyDeleteAnkal, kama huu si utani wa April Fools' Day, [maana naona hiyo posting ni ya 1 April], basi nami naungana na wadau wengine hapa juu kukupa pongezi zangu za dhati na kumuomba Muumba wetu awape wewe na wanafamilia wako kila la heri. J. Mwaipopo.
ReplyDeleteHAHAHAA...Bro Ankal MIE NAKUPA HONGERA YA KUWEZA KUWASHIKA WENGI,
ReplyDeleteNaona hata wewe ukianzisha kikombe utapata mamluki,
Kweli cku ya wajinga!!!
April fools day. Umewapata uncle.
ReplyDeleteHongera bro. Tunakutakia mema zaidi. Hata hivyo natumai kuwa utaendeleza libeneke na tutaendelea kupata blogspot yetu ya jamii ambayo ndiyo blogspot namaba moja ya kitanzania kila siku. Be blessed.
ReplyDeleteApril Fools day kweli umewapata wengi uncle michuuz
ReplyDeleteHongera sana mkuu, ila japo naona hizo pcha lakini habari hii umeitoa siku ya "wajinga" sasa kidogo inautata, hebu kesho tuwekee mkazo ili tukupongeze vizuri.
ReplyDeletePicha ya pili inaonekana kama alishawahi kuitoa siku za nyuma jamani. Thikukuu ya wajinga,… thidanganyiki!
ReplyDeletei hope its not April fool!!!
ReplyDeleteAnkal naona umewapata sana watu leo...ha ha ha ha....Najua tutakutana soon pale Break Point. Happy fools day
ReplyDeleteHa, ha, ha, LEO NI SIKU YA WAJINGA DUNIANI!
ReplyDeleteumewapata wengi, siku ya wajinga duniani!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteKAKA LKN HAYA SIO MAMBO YA APRIL FOOL?!MAANA HIZI PICHA NAONA KM ZILE ZA KIPINDI KILE UMEANDAMANA MHE RAIS!
ReplyDeleteWajinga ndio waliwao...(April Fool's Day)...
ReplyDeletemmmhhh Ankal?
ReplyDeletehii sio fools' day special kwa wadau???
kama sio, hongera!Mungu akuzidishie!
AHHHHH......WAIT A MINUTE????
ReplyDeleteKwani leo siku gani???? Michuzi aache Bongo, now way. Kwenda zako, mi sihamini leo Aprili moja bwana..this sounds waaay good to be true
AHAHHAHAH APRIL FOOLSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS
ReplyDeleteHE GOT YOUUUUUUUUUUUUU!!
ila leo ni siku ya wajinga kumbukeni jamani
ReplyDeleteYaani nyote nyie hapo juu mmeingizwa mjini na ankal? leo ni siku ya wajinga, na nyinyi ni wajinga waliwao. taarifa za kuaminika, ankal yupo loliondo kwa babu kaweka hema akisubiri zamu ya kikombe, na sio marekani..wabngo bwana, maneno tu..ina maana angesema leo anatoa kikombe uwanja wa taifa, basi nyie mgeeenda..april 1st, siku ya wajinga na vihiyo..
ReplyDeletehngera ankala kwa kuivuta hii vilivyo..
Ya kweli au sikuku ya ... Maana leo tarehe 01-04
ReplyDeleteApril fooooooooooooooooooooooooooool people
ReplyDeleteHongera on the APRIL FOOLS..............ahahhaaaaa
ReplyDeleteApril fools dayyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyyy.Hizi ni picha za zamani wakati Jk alipokuja USA.
ReplyDeleteHongera sana Muhidi! Hakika unastahili kufika ulipofika! Hakika!
ReplyDeleteHa ha ha ha ha...kaka leo kweli umetupata...HAPPY FOOLS DAY!
ReplyDeletemmmhh nina mashaka siku ya wajinga leo hahahhahahahahaa
ReplyDeleteuncle kawapata
Leo siku ya wajinga duniani ankal tunaye bongo hapa haendi popote poleni mliokuwa mnamsubiria kwa hamu ughaibuni
ReplyDeleteAsalaam aleikum, Ankal napenda kuchukua fursa hii kukupa pongezi zangu za dhati kwa kufanikiwa kufika huko maana najua ni kwa juhudi binafsi na kudra za mwenyezi Mungu. Napenda kuungana na wadau wengine kukutakia mafanikio mema zaidi na zaidi, Kwani hata mimi katika nyanja za blog nimekuwa nikipata mwelekeo toka kwako, waweza itembelea Blog yangu ya www.mtandaowawatanzania.blogspot.com.
ReplyDeleteahsante!
kweli uncle umewapata weeengi kwenye sikukuu ya leo ya wajinga.....wamekupa hongera ni wenngi.
ReplyDeletehongera kwa kuwaingiza wachache mjini!!!
ReplyDeleteAPRIL FOOOOOOOOOOOOOOOL!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
CU nxt yr 01.April
Hongera sana. Tunakuomba tu ukifika huko usije ukaanza nawewe kutuandikia vingerza hapa kwenye blog yako kama akina mashaka. Vingerza vyenyewe ni vya kuunganisha na selotepu/gundi.
ReplyDeletelingine tusije tukakusikia baada ya miaka 2 eti ooh nataka nigombee ubunge. Tutaacha kusoma hii blog yako kwani tunajua ww ni kijani na njano, rangi ambazo zimeshachuja. tunahitaji jezzy zingine nazo kwenye ulingo wa siasa tuone zinakuja na lipi.
ankal acha uongo!hata mimi nilitaka kupatikana ila umenikosa
ReplyDeletesiku wajinga leo
ReplyDeleteHongera kaka, sasa umetumbukia kubeba box.lol
ReplyDeleteHongera sana ankal Mungu akutangulie katika kazi hiyo, na akupe afya njema. Kikombe ulipataaa????
ReplyDeleteAnksl isije ikawa April Fools Day ...
ReplyDeleteOtherwise nikupe hongera sana naamini katika juhudi na maarifa. Na hivi ndio vimekufikisha hapo ulipo.
Ila kama ni April Fools Day utawapata wengi ..
Dommy
Hongera sana ankal lakini kumbuka white house dressing code si ze fulana lol
ReplyDeleteall ze best
kaka nimekukamata siku ya wajinga leo..hahahahahahahaha.hizi picha zako za kitambo ulivyoenda..poleni wajinga
ReplyDeleteuncle i hope hujatufanya fools leo, but kama kweli hongera sana
ReplyDeleteWote mliotoa comments kalakabahu. Hivi hamjamgundua leo ni siku ya wajinga, Ankal kawachakachueni eti na nyie mmechakachuka. Kweli MJINI SHULE. Popleni na hongera ankal kwaa kuwapata wajinga wengi kiasi hicho... lol
ReplyDeleteAPRIL MOSI 2011
ReplyDeleteHONGERA KAKA MICHUZI TUNAKUTAKIA KILA KHERY KATIKA KAZI NA DHAMANA MPYA ULIYO TUNUKIWA NASI TUNAOMBA USILIACHE JAMVI LETU NYUMA ....BIG UP...........MDAU...DOHA
ReplyDeleteTarehe 1 leo mwezi wa nne, ni sikikuu ya wajinga. Hongera kwa kuwakamata wengi.
ReplyDeleteApril Fools dayyyyyyyyyyyy got a lot of people. Ukiangalia hizi picha vizuri utagundua zina zaidi ya mwaka. Michuzi hapa anaonekana kijana tofauti na post moja ya mwanzoni mwa wiki hii ambayo inayonyesha ana mvi kichwani
ReplyDeleteMbigiri
leo ni april fool, usiwe unatudanganya ankal, hahaha
ReplyDeleteHongera kwa bonge la April fool
ReplyDeleteHaya yasije kuwa , mambo ya april fools lakini. Nasubiria kesho nitoe pongezi.
ReplyDeleteapril fool dude
ReplyDeleteHongera mkuu!but naona km fix vile coz leo ni siku ya wajinga!!
ReplyDeletefrm manto.
Happy fools day!
ReplyDeleteapril fools day!
ReplyDeleteSio mambo ya tarehe 1 April kweli! Manake habari yenyewe imetoka siku ambayo sio!
ReplyDeletekaka mbona maoni mengine una minyia?
ReplyDelete1st of april
ReplyDeleteBIG UP ANKAL!!
ReplyDeleteAnkal hiyo ni kweli au mambo ya siku ya wajinga...Binafsi naomba iwe kweli ule bata huko ughaibuni.Inshallah
ReplyDeleteHA-HA-HA-HA HAPPY FOOL!....Mdau USA!~
ReplyDeleteAPRIL FOOLS! Hizi picha nakumbuka kama kipindi kile ulivyoeenda na JK Nyumba Nyeupe( White House)
ReplyDeletesikukuu ya wajinga. Naona umewapata wengi kweli
ReplyDeleteHah hah Hah! leo uko unaripoti VOA! kesho tarehe 02 April unarudi kupambana na joto na foleni za Dar Es Salaam.
ReplyDeleteKesho tutakuna Rose garden kama kawaida na kuporojoa kungojea jam ipungue kabla ya kurejea makwetu.
Libeneke kuendelea kutokea Dar na siyo Washington DC. Fools Day I guess.
kaka mbona haieleweki eleweki au imekaa ki 1st april? mwandishi mpiga picha, wanabadilishana na mtangazaji?
ReplyDeleteUNCLER MICHUZI. KAMA LEO NI SIKU YA WAJINGA VILEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
ReplyDeleteIRENE MZIGURA
Jamani leo ni 1st of April, naona amewapata haswa
ReplyDeleteUtani Mwingine bana...
ReplyDeleteNAOMBA ANKOO UJIITEE ANKOO WA MANKOO
ReplyDeleteMichuzi tunaomab uthibitishe kauli yako usiku huu.
ReplyDeleteShabashii! Wapiiiii!!!!!! hiyo nafasi ameipata saa ngapi! Huyo ni Ndanda boy ktk siku ya Foooooooooooooooools!!!! Day.
ReplyDeletemzee wa pajazzzzz na titizzzzzz nikumbukwe pia ankal!
ReplyDeleteankal hongera lakini mbona umevaa suti tatu kwa siku moja au na wewe ushakuwa super star?
ReplyDeletesawa mimi nakwambia karibu nyumbani
NASHUKURU WADAU WOTE MLIOTOA NA MSIOTOA MAONI. UKWELI NI KWAMBA ANKAL ALITANGAZA HIVYO KAMA KUENDELEZA LIBENEKE LA APRIL FOOL'S DAY. HIVYO HABARI HIYO SI YA KWELI BALI NI YA KUFURAHISHA BARAZA TU. ASANTENI KWA KUENDELEA KUNISAPOTI KATIKA LIBENEKE NAMI NAWAAHIDI WEMBE NI ULE ULE, HAKUNA KULALA
ReplyDeleteApril Fool - Hukmu Ya Kushiriki Kuongopa Kwa Mzaha
ReplyDeleteNasiha Za Minasaba Mbalimbali
Kufanya utani wa kusema uongo siku ya tarehe 1 Aprili limekuwa ni jambo la kawaida kwa baadhi ya Waislamu, jambo ambalo limeharamishwa katika Shari’ah ya Kiislamu
عن ابن عمر رضي الله عنهما قال : قال صلى الله عليه وسلم: ((إني لأمزح ولا أقول إلا حقّا)) رواه الطبراني في المعجم الكبير - " وصححه الشيخ الألباني
Kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu ‘anhuma) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika mimi sifanyi mzaha wala sisemi ila tu yaliyo ya kweli)) [At-Twabaraaniy katika Al-Mu’ujam Al-Kabiyr na ni Swahiyh kwa mujibu wa Shaykh Al-Albaaniy]