wataalamu wa upimaji barabara wako bize hivi sasa jijini Dar wakiandaa njia za kupita mabasi yaendayo kasi .Hapa ni barabara ya Azikiwe avenue
 Upimaji ukiendelea.
 Kwa jicho la kawaida ni ngumu kuwaelewa
 Kwa vile ni siku ya kazi zoezi hilo linakuwa gumu ukizingatia watu na magari yanakatisha kila dakika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2011

    Kaka michuzi hii hadithi ya hawa jamaa nadhani itaaminika tukiona utekelezaji otherwise mimi binafsi siamini kama kuna kwenda kasi wala nini.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2011

    Jamani jamani! Huu upimaji utachukua muda gani? Maana huu mpango ulikuwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005. Na JK alituahidi kuwa mwaka 2006 mabasi ya mwanzo yangeanza kufanya kazi. Lakini sasa miaka 5 baadaye bado zoezi la upimaji linaendelea. Haya mabasi hayaji ng'o labda hapo daladala zote za wakubwa zitakapochoka na kushindwa kufanya kazi. Na hii inawezekana tu kama mamlaka huska zitaacha sasa kusajili magari madogo ili yatumike kama daladala.

    Msongamano Dar na majiji mengine hautokani na ufinyu wa barabara tu bali ni kwa sababu ya vipanya na DCM kutumika kusafirisha abiria. Kama yangetumika mabasi makubwa, badala ya vipanya 200 kutahitajika mabasi kama 30 tu. Sasa huoni kuwa hapo msongamano utapungua. Pili usafiri utakapokuwa mzuri watu hawataenda na magari binafsi makazini, maana ni gharama kubwa sana kuendesha gari binafsi. Sasa huoni kuwa foleni itapungua kwa sana.

    Kwa hiyo mimi sioni kuwa msongamano utaondelewa kwa kuongeza barabara za mabasi. Ningefurahi kama hizo barabara zinazoongezwa zingekuwa za waenda kwa baiskeli. Sasa hivi Tanzania hatuendi na baiskeli kazini maana hakuna njia za waenda kwa baiskeli.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 10, 2011

    kaka michu, hawa jamaa sio wadau wa uclass wanapiga assignment

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 10, 2011

    mimi cdhani kama ni sahihi kupitisha hayo mabasi ya kasi na hata ya sasa sababu yanasababisha msongamano mkubwa sana wangeplan vizuri mabasi yangepita pembeni ya jiji na watu tungeweza shuka na kuingia kati ya jiji !
    Mzushi

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 10, 2011

    natamani sana uanze maana ni kama ndogo mafuta yanatuumiza sana maana sasa elfu kumi kwa siku du

    ReplyDelete
  6. wabongo kwa mbwembwe hatujambo hayo mabasi yatakua yanaenda kwa kasi kuelekea wapi? na yatasimama wapi na wapi? kwa miundombinu ipi? madereva hawa hawa au watakua wazungu!!! na reckless driving yetu hayo mabasi watu wengi watakua disabled hapo mjini kama wale wa piki piki za mchina Muhimbili pale wanaweza tusaidia kuthibitisha idadi ya disabled/vilema au kufa kwa ajali hapo hatujasema ajali za vipanya na ma dcm,sijui fuso!!.

    Suluhisho la foleni dar ni pamoja na kuhamisha hayo mawizara..wizara ya kilimo na mifugo ipo dar wakulima wako Iringa, Mbeya..wafugaji shinyanga, Mwanza, Mara.

    Hayo mabasi hata waweke bend bus, au show case haitasaidia kwa miundo mbinu tuliyokua nayo kama wapo serious wajenge fly over kwenye makutano ya bara bara zilizo bize kama morogoro road maeneo kama ubungo,magomeni,fire, kwingineko lkn nahofia uzembe wa madereva wetu hio fly over zitakua ajali usiku na mchana kila siku.

    Pia wapige marufuku gari ina mtu mmoja inaenda mjini?? chukua mfano mama ana gari yake, watoto,vijana wakazi (house boys,shop keepers,wafanya kazi wa ndani siku hz wengine wana drive (house girls),wanafunzi pia wengine wana drive foleni itakosa? familia za wafanya biashara ndio kabisa (baba, mama,mtoto,vijana wakazi) mnagombea parkin moja pale kariakoo na sehemu nyingine kwanini wasitumie gari moja?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...