MKAZI wa kijiji cha Ntendo, Zakaria Lusambo akimshukuru, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye baada ya kukabidhiwa baiskeli ya miguu mitatu pamoja na wenzake wanne wenye ulemavu wa miguu, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jana, kwenye Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga. Baiskeli hizo zimetolewa na Mbunge wa Sumbawanga, Aeshi Hilary

Waliokuwa wanachama wa CHADEMA wakimpa kadi zao, Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, katika mkutano wa hadhara uliofanyika, jana, katika Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga. Zaidi ya wanachama 50 wa CHADEMA walirudisha kadi zao na kujiunga na CCM

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga, jana, siku ya kwanza ya ziara yake na Mjumbe wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba, mkoani Rukwa.

KATIBU wa NEC, Uchumi na Fedha CCM, Nchemba Mwigulu akikabidhi kwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kadi za wanachama kutoka vyama vya upinzani ambazo wanachama wa vyama hivyo walimkabidhi baada ya kutangaza kuhama vyama vyao na kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana, katika Uwanja wa Mandela, mjini Sumbawanga. Mbali na CUF na NCCR-Mageuzi, Chadema pekee walihama 51.


KATIBU wa NEC CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara baada ya mapokezi ya msafara wake na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Nchemba Mwigulu, kuwasili kwenye uwanja wa Laela A, Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa

VIjana wakimzunguka Nape baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Naela, Sumbawanga mkoa wa Rukwa.

Waendesha pikipiki zaidi ya 50, wakisubiri kuusindikiza msafara wa Nape na Mwigulu, baada ya kuwasili nje kidogo ya mji wa Sumgawanga mkoani Rukwa

Nape akiteta jambo na Mbunge wa zamani wa jimbo la Nkwela, Chrisant Mzindakaya, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Naela A, Sumbawanga mkoani Rukwa.

Nape akishiriki katika ngoma ya kina mama wa Naelea mkoani Rukwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Well done Nape, nasi tunatakiwa tufanye hivi. tunakanyaga wao walipopita tunasafisha wao walipochafua tunaweka sawa wao walipopotosha. Naomba Chama chetu kiwawezeshe mzunguke kote walikotia doa muweke hali ya mambo sawa. Kwa kasi hii na ari zaidi nina hakika tutayarudisha majimbo. CCM Juu...

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2011

    mh nape hii hasa ndio dawa pekee ukizingatia uwezo upo nguvu ipo na wasomi wapo wengi tu wapo nyuma yenu hata wananchi bado wanaimani na ccm kwa kiasi kikubwa mbali na propoganda chuki na jaziba ukijumlisha na uongo wa watu wazima wenyeakili zao timamu wenyelengo baya na nchi yetu kwa ajili ya uroho na tamaa zao mungu akubariki sana ni chama kisichokuwa na ubaguzi wala upendeleo chenye wabunge wa makabila yote na dini zote nchini mungu awe nanyi amin

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2011

    cha msingi tuepuke uchakachuaji.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 01, 2011

    Hao watoto watakuwa wamefikisha miaka 18 kuweza kupiga kura 2015?Hao ndio watawang'oa kwa taarifa yako bwana NAPE(Tanzania brotherhood!!).Ila CCM mna bahati nyie....kungekuwa na....mngeipata....basi tu hatuna jinsi inabidi tuwakubali(nadhani mnanielewa ninachomaanisha)

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...