Washiriki wa Miss Excellence OUT mwaka huu wataochuana leo viwanja vya
Chuo Kikuu Huria Kinondon Biafra, jijini Dar es salaam




WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Benard Membe atakuwa mgeni rasmi katika mashindano ya urembo ya kumsaka mrembo wa Chuo Kikuu Huria yaliyopangwa kufanyika leo kwenye ukumbi wa chuoni hapo Kinondoni Biafra, jijini Dar es salaam.

Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 11 kutoka matawi mbali mbali ya chuo kikuu huria kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano, Albert Memba.

Memba alisema kuwa Waziri Membe amethibitisha kuwepo kaika mashindano hao ambayo yatapambwa na bendi ya Mapacha Watatu na msanii wa bongo fleva, Linah.

Aliwataja warembo ambao watachuana leo kuwania nafasi ya kushiriki katika mashindano ya Miss Tanzania kuwa ni Grace Dominic, Weirungu David, Bella Edward, Nemesia Simon, Jemima Maole, Magdalena Assey, Neema  Mtitu, Sophia Chacha na Valentine Uwonga.

Warembo hao walikuwa kambini hotel ya Chichi iliyopo Kinondoni chini ya mkufunzi wao ambaye ni miss chuo kikuu huria wa mwaka 2009, Shine Mkali.

“Tunatarajia kuwa na shindano kali ambalo litatao warembo bora ambao tunaamini watashinda katika mashindano ya Vodacom Miss Tanzania mwaka huu na kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Dunia, Miss World,” alisema Memba.

Washindi watatu wa mashindano hayo watapata fursa ya kupambana katika mashindano ya Miss Tanzania yaliyopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...