Waziri Mkuu wa zamani,Edward Lowassa(Kushot0)akimkabidhi Bahasha yenye Tsh. milioni 13, Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu,Issa Shaaban bin Simba,kwa ajili ya kusaidia shule ya sekondari la Edward Lowassa iliyopo Kigamboni,Dar es Salaam.Kwa mujibu wa Mufti ambaye ni mlezi wa shule hiyo, Shule hiyo inatarajiwa kufunguliwa rasmi mwakani kwa kuanzia na wanafunzi 200 wa kidato cha kwanza, na kwamba fedha hizo zitatumika kukamilisha baadhi ya mambo ya shule hiyo ikiwemo kujenga bweni la watoto 30, choo cha shule, kisima cha maji na shule itajihusisha zaidi kusomesha yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Kulia ni aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Alfred Tibaigana ambaye pia ni mlezi wa shule hiyo.
Edward Lowassa(kulia)akimsindikiza Mufti wakati akiondoka baada ya hafla ya kumkabidhi fedha hizo,iliyofanyika Ofisini kwake,Mikocheni, Dar es Salaam.
Wakiagana baada ya shughuli hiyo.Picha na Mdau Bashir Nkromo
harooo hiro rimjamaa ringine katikati ya rishekhe na rirowasa sirifahamu muraaaa hebu ritamburishee nadhani ni rimtu maarufu muraa
ReplyDeleteGo Lowassa!! Our next President!!
ReplyDeleteThis is nice watanzania mna ushirikiano sawa Mbarikiwe!Allah akuzidisheni!
ReplyDeleteRais wa ukweli 2015, wabaya wako watakufa kwa kiwewe very soon. A very visionary leader, we need you!!!
ReplyDelete