Bosi wa zamani wa Benki ya Dunia  Dominique Strauss-Kahn ameachiwa huru baada ya Mahakama ya Manhattan, New York, nchini Marekani  kufuta kesi yake ya kubaka baada ya waendesha mashitaka kuomba kesi hiyo  ifutwe kile kilichodaiwa ushahidi hafifu na uwongo wa mshtaki  mfanyakazi wa hoteli Nafissatou Diallo. Waandamanaji kibao walifika mahakamani hapo kushinikiza afungwe kwa kitendo hicho, lakini ndio hivyo tena mahakama imemuachia na amekuwa huru kurudi nyumbani kwake Ufaransa ambako wachunguzi wa mambo wanasema anaweza kusimama kugombea Urais wa nchi hiyo katika uchaguzi ujao.

Mwanamke huyo wa Afrika Magharibi mwenye umri wa miaka 33 alidai Strauss-Kahn (62) alimshambulia kingono katika hoteli ya Sofitel kitongojini Manhattan mnamo Mei 14, mwaka huu. Bosi huyo wa zamani wa Benki Kuu alikamatwa ndani ya ndege ya Air France alipokuwa akijaribu kutoroka Marekani. Pichani anaonekana Strauss-Kahn na mkewe  Anne-Sinclair pamoja na wakili wake wakitoka mahakamani baada ya kuachiwa huru. Uchunguzi w DNA ulithibitisha kwamba Strauss Kahn alifanya ngono na mwanamke huyo lakini hiyo haikutosha kuthibitisha kwamba kitendo hicho kilikuwa kwa kulazimishwa au la.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. hii inasikitisha sana manake huyu mzee ana tabia ya kupenda wanawake ni alimshika kweli yule mwanamke ila tu pesa ndio imefanya vitu vyake hapo.... atabaka tena mwingine huyu manake anajua ni atatolewa tu kwa pesa yake. how sad. na angekuwa mtu mweusi hapo ni angeenda tu jela lakini sababu ni mweupe anaachiwa HURU.... vitu vingine ni vya kijina manake kama yule mchezaji wa mpira MICHAEL VICK kaenda jela sababu ya kupiganisha mbwa huyu kabaka kweli na anachiliwa, kwa kweli inaudhi alichokosa tu ni kazi yake nzuri la sivyo ataendelea kuishi kifahari mstzzz

    ReplyDelete
  2. ANGELIKUWA MZUNGU INGETHIBITIKA KABAKWA NA HASA BAADA YA HIVYO VIPIMO VYA DNA KUTHIBITIKA LAKINI NI MUAFRIKA IMESHAPAMBWA KUWA ALITAKA MWENYEWE EH MOLA TUEPUSHE WAAFRIKA NA MABALAA HAYA HASA TUISHIO UGHAIBUNI

    ReplyDelete
  3. Kesi umeshinda , kimbembe nyumbani angalia mama alivyo na usongo mkifika home! pambaf

    ReplyDelete
  4. Bosi wa zamani wa "Benki ya Dunia" na "Benki Kuu?" Au wa Fuko la Kimataifa la Fedha (IMF)?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...