Aliyekuwa mkurugenzi Mkuu wa TBC Tido Mhando (shoto) akimpa maelezo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seth Kamuhanda alipotembelea studio za TBC wakati Tido akiwa bado kazini na kabla ya kumalizika mkataba wake.

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Bw. Dunstan Tido Mhando, hajachukuliwa na Al Jazeera, kituo cha habari   cha kimataifa chenye makao yake mkuu jijini Doha, Qatar, Globu ya Jamii inaweza kuthibitisha.

Uchunguzi wetu wa kina kufuatia habari hizo kuchapishwa katika mitandao ya jamii kwa muda wa wiki mbili sasa unaonesha Al Jazeera sio tu hawajamchukua Tido bali pia yeye mwenyewe hajaomba kushika wadhifa huo. 

Vyanzo vyetu vya habari vilivyo karibu kabisa na Tido vinasema yeye mwenyewe ameshangazwa na uvumi huo ulioanzishwa na mtandao wa Jackal  News wa nchini Kenya kwamba Tido Mhando na Joseph Warungu, maveterani wa BBC, wamehamia Al Jazeera.

Vyanzo hivyo vimehoji kwamba Al Jazeera kikiwa ni chombo makini cha kimataifa kisingekuwa na haja kutangaza hadharani nafasi za kazi kadhaa ikiwamo hiyo ya Ukurugenzi wa idhaa yake mpya ya Kiswahili katika Afrika Mashariki endapo kama wangekuwa wameshampata Tido.

Vimesema vyanzo hivyo kwamba hivi sasa Tido yuko mbioni kufungua kampuni yake binafsi na wala hana mpango wowote wa kwenda Al Jazeera ama chombo kingine chochote.

"Endapo kama vyombo vilivyovumisha mambo haya vingekuwa makini vingemfuata Tido mwenyewe kujua ukweli wa mambo," vimesema vyanzo vyetu vya habari.

Tido, ambaye alimaliza mkataba wake na kuondoka TBC mwishoni mwa mwaka jana, amekuwa hasikiki na mara ya mwisho kuonekana hadharani ilikuwa wiki mbili zilizopita kwenye msiba wa mke wa Mzee Mikidadi Mahmoud. Juhudi za wanahabari kutaka aongee siku hiyo hazikuzaa matunda.

Leo Globu ya Jamii imeweza kuongea na Tido Mhando, naye kathibitisha kwamba yuko njia moja kufungua kampuni yake binfasi, ambayo hakuitaja jina wala kutoa tarehe za kuanza kazi na kazi aina gani. Naye alionesha kushangazwa habari zinazomhusu yeye kuhamia Al Jazeera na kukataa kuongelea kitu alichokiita uvumi usio na ukweli.

Globu ya Jamii pia ilizungumza na mratibu wa nafasi za kazi zilizotangazwa kwa idhaa yake mpya ya Swahili Service, naye kaoneshwa kushangazwa nan habari hizo, akisisitiza kwamba si rahisi wao kutangaza nafasi ambayo keshapewa mtu. 


Ila amekiri kupokea mombi mengi sana toka wanahabari wa Afrika Mashariki na kusisitiza kuwa hawezi kusema kuwa jina la Tido limo ama la kwani muda wa kuchambua maombi bado haujatimia.  "Muda utapowadia mtatangaziwa kila kitu", alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Habari wadau? Mimi ninashauri kuwa habari ichujwe vyema kabla ya kurushwa. Mini habari ya kwanza ilinistusha na kumuombea Tido kazi mpya njema kumbe si kweli. Hii inanichanganya!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...