Mwakilishi wa Emmanuel Televisheni na Kanisa la The Synagogue Church Of All Nations Bi. Martha Harvey akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jumla ya shilingi milioni ishirini na tano 25,000,000/- kwaajili ya wahanga wa ajali ya Meli ya MV Spice Islander iliyozama katika mkondo wa Nungwi huko Unguja na kusababisha vifo vya watu wengi hivi karibuni. Mchango huo uliokabidhiwa leo ikulu jijini Dar es Salaam umetolewa na Kiongozi wa Kanisa hilo Nabii Themitope Balogun Joshua ambaye anaishi katika MAKao makuu ya Kanisa hilo jijini Lagos Nigeria.
Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.
NAOMBA KUULIZA SI KWA UBAYA , MBONA WATHAMINI WENGINE NILINA WALIKUWA WANATO AMCHANGO WAO KWA YULE KIONGOZI WA ZENCHI INAKUWAJE HAWA WANATO DIRECT KWA RAISI WA BARA ? NAOMBENI JIBU JAMANI.
ReplyDeleteMDAU PARIS
Wewe muuliza swali wa kwanza hapo juu. Yaani pamoja na kuishi Paris Ufaransa bado hufahamu kuwa Rais Kikwete ndiye kiongozi wa Tanzania yaana Bara na Visiwani? Ukimpatia Rais kikwete pesa itafika kwa wahusika.
ReplyDeleteMchungaji Dar es salaam
Nimependa staili ya hilo kanisa katika jinsi utunzaji wa pesa, badala kushika minoti kama makaratasi ya kufungia maandazi
ReplyDelete