MKURUGENZI wa Uchaguzi jimbo la Igunga Magayane Protace (kulia) akimkabidhi fomu za kuwania ubunge wa jimbo hilo, mgombea mteule wa CCM Dk. Dalally Kafumu , jana. Wengine ni Katibu wa CCM wilaya ya Igunga Neema Adamu na Msimamizi wa masuala ya uchaguzi wa CCM, Matson Chiz
MGOMBEA mteule wa CCM jimbo la Igunga Dk. Dalally Kafumu (kushoto) na Mratibu wa Uchaguzi wa CCM jimboni humo, Katibu wa NEC ya CCM, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba wakiwa katika huzuni kwenye hospitali ya wilaya ya Igunga ambako walisaidia kupeleka mwili wa mtoto Peter Ezekiel ambaye alifariki papo hapo baada ya kugongwa na lori la mizigo katika barabara ya Igunga-Singida akijarbu kuvuka barabara akiwa na mamia ya wananchi wa jimbo hilo waliokuwa wakimsubiri Kafumu na msafara wake, jana. Kulia ni ndugu wa mtoto huo.

MGOMBEA mteule wa CCM jimbo la Igunga Dk. Dalally Kafumu (kushoto) na Mratibu wa Uchaguzi wa CCM jimboni humo, Katibu wa NEC ya CCM, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba wakimfariji Kulwa Mpina baada ya kufika kwenye chumba cha kuhifadhi maiti mwili wa mtoto Peter Ezekiel ambaye alifariki papo hapo baada ya kugongwa na lori la mizigo katika barabara ya Igunga-Singida akijarbu kuvuka barabara akiwa na mamia ya wananchi wa jimbo hilo waliokuwa wakimsubiri Kafumu na msafara wake jana. Picha na mdau Bashir Nkoromo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

 1. Safi sana Kafumu. Igunga ni jimbo letu hata waoshe vinywa namna gani hawatafurukuta. Wangekuwa ndio wanapiga kura tungepata wasiwasi. Lakini kwa vile wapiga kura wanatuunga mkono, basi hatuna shaka na uchaguzi huo.

  CCM oyee!

  ReplyDelete
 2. jamani na mie nalia

  ReplyDelete
 3. Tunachohitaji hapo ni uchaguzi wa HAKI tu basi.Mambo ya ujanja ujanja kwenye chaguzi tunaomba ukome mara moja manake unaweza kuitumbukiza nchi yetu nzuri kwenye matatizo(Kinachoendelea kwingineko duniani tunakishuhudia wenyewe..uwongo jamani?).Ile dhana kwamba haa Tanzania 'hiki kitu' hakiwezi kutokea ondoeni vichwani mwenu kabisaaa..tusisahau kwamba kuna vijana wanakua.Tume ya uchaguzi ndiyo yenye jukumu la kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani na HAKI..Kuna watu wanatumia vibaya vyeo vyao serikalini na kuamrisha Tume ya uchaguzi kufanya 'wanavyotaka'..Ipo siku watakuja kujuta..Nchi kuchafuka ni sekunde tu..Maamuzi mabovu ya mtu mmoja yanaweza kuitumbukiza nchi katika matatizo makubwa.MICHUZI TEAM msibane comment yangu..bado tunahitaji amani nchini na ili amani iwepo kunahitajika demokrasia ya ukweli na HAKI..HAKI HAKI ITENDEKE.TANZANIA nakupenda kwa Moyo wote.

  Ni mimi

  David V

  ReplyDelete
 4. Wanaigunga msituangushe. Tunaamini maendeleo aliowaletea Rostam yatakuwa kichocheo kwenu ninyi kuipa CCM ushindi katika jimbo hilo. Msimuangushe mbunge wenu aliyeamua kujiuzulu japo kwa kashfa kwani alikuwa anahakikisha anarejesha nyumbani japo kidogo alichopata huko alikokwenda kutafuta. Si sawa na ambao hawaleti kabisa. Mkono mtupu haulambwi.

  ReplyDelete
 5. Natoa pole kwa Mama Kulwa Mpina kufiwa na mtoto wake. Mungu ampe nguvu katika kipindi hiki kigumu.

  Nimeshuhudia watoto wadogo na ata wakubwa wakigongwa na magari, malori, Tanzania hasa kwa vile hawaangalii kabla ya kuvuka barabara au walikuwa wamelewa. Huyo mtoto sijui details, labda alikuwa anajaribu kuwahi wenzake waliokwisha vuka. Habari ya huyo mtoto inasikitisha mno.

  Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. AMEN.

  ReplyDelete
 6. inatia huruma unakwenda kwenye sherehe na mtoto wako anafarii kwa kugongwa na gari,lakini pia kina mama tuangalie tusiwe washabiki wa vyama tunafuata sherehe tunawacha watoto masafa ya mita 100,pole dada ndio kazi ya mungu

  ReplyDelete
 7. Kaka Nchemba naona vile vi digrii vyetu sasa vimekuwa politics kabisa. Kula kuku mwanangu

  ReplyDelete
 8. KWA NINI WATANZANIA HATUELEWI? HIVI MTUMIA BARABARA KWA MIGUU AMEENDA SHULE GANI KUSOMEA KUVUKA BARABARA?

  Kwa hali yoyote inapokuwa dereva kama mtaalamu aliyesomea kuendesha chombo cha moto wakati anapita kwenye eneo lenye makazi halafu akagonga mtu ni kosa la dereva. Kwa sababu alitakiwa kuchukua tahadhari na kupunguza mwendo.

  Sasa mtoto wa watu anagongwa halafu tunasema haaangalia kushoto/kulia sasa huyo dereva alikuwa anaangalia wapi?

  Inasikitisha sana. Naomba uumbe huu uende kwa watu wote wanaotumia vyombo vya barabarani au wanaojiita madereva. Udereva ni kuwa makini kuepusha ajali barabarani.

  Poleni wafiwa na Mungu ailaze roho ya marehemumahala pema peponi.

  ReplyDelete

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...