
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Maiti zilizopatikana hadi sasa ni 192 na watu 601 wameokolewa wakiwa hai katika eneo la Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja kati ya watu 760 waliosajiliwa kusafiri na meli ya MV Spice Islander iliyokuwa ikielekea kisiwani Pemba juzi usiku wa Septemba 9, 2011.
Baadhi ya Abiria walionusurika walisema kuwa abiria walijaa kupita kiasi katika Meli hiyo kongwe ya MV Spice Islander iliyokuwa ikielekea Pemba.
MV Spice Islander ilianzia safari yake kwenye Bandari ya Dar es Salaam ambapo iliondoka mchana wa Septemba 9, 2011 ikielekea Pemba kupitia Zanzibar.
Ingawa haijafahamika maramoja kuwa Dar es salaam iliondoka ikiwa na abiria wangapi na mizigo yenye tani ngapi, lakini meli hiyo ilitia nanga kwenye Bandari ya Zanzibar na kuondoka kuelekea Pemba usiku wa kuamkia Septemba 10, 2011 ikiwa na abiria 670 waliosajiriwa.
Mnamo majira ya saa 7.30 usiku meli hiyo ikiwa katika eneo la Nungwi mkoa wa kaskazini Unguja ilianza kupinduka polepole na hadi ilipofika saa 9.00 usiku meli hiyo ilipinduka na hatimaye kuzama kabisa kwa kuelemewa na mizigo pamoja na abiria.
Baadhi ya wananchi wameitupia lawama malka ya bandari na Sumatra kwa kushindwa kudhibiti uchukuzi wa abiria na mizigo kupita kiasi.
Kazi ya utafutaji wa watu walio hai na uopoaji wa maiti bado unaendelea na vikosi vya Jeshi la Polisi wanamaji, KMKM na JKU wanaendelea na kazi hiyo.
Jeshi la Polisi limetuma timu ya wataalamu wa Upelelezi na Madaktaji pamoja na Meli moja ya uokoaji MV Mamba ikiwa na boti nyingine ndogondogo ziendazo kasi za msaada majiuni.
Serikali ya Zanzibar na ile ya Muungano kupitia marais JK na Dk. Shein wametangaza siku tatu za maombolezo kuanzia kesho Septemba 11, 2011 na bendera zote zitapepea nuzu mlingoti.
Hakutakuwa na sherehe zozote ama mikusanyiko yenye kuonyesha buurudani na michezo.
Mh. Zito Kabwe, yeye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Waziri Kivuli wa Fedha, alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa vyama vya Siasa waliofika katika viwanja vya Maisala mjini Zanzibar na kutoa Pole kwa wafiwa na kusema Chama chake kimesitisha kwa muda shughuli za kampeni katika jimbo la Igunga mkoani Tabora kutokana na msiba huo mzito.
Hiyo ni meli ya pili kuzama baharini ikiwa safarini kuelekea Pemba. Meli ya kwanza ilikuwa ni MV Fatahi iliyozama mwaka jana ikiwa Bandari ya Zanzibar ikielekea Pemba.
Meli nyingine mbili ziliungua moto zikiwa bandarini Zanzibar na meli nyingine ya MV El- Salaam ilizama Baharini ikiwa na bidhaa mbalimbali ikielekea Songosongo Kilwa kwenye utafiti wa mafuta.
Hakika poleni ndugu na Jamaa wa Abiria wote waiosafiri na Chombo hicho kwa Vifo vya raia wa Tanzania wasionahatia. Hakika ajali hii inasikitisha sana hasa ukizingatia kuwa Serikali yetu ina Taasisi mbalimbali zinazoshughulikia suala zima la usafiri. Je ndugu zetu wataendelea kupoteza maisha hadi lini, Mv Bukoba, Mv Fatahi na sasa MV Spice Islander. Ni ukweli usiofichika kuwa Rushwa na kutowajibika (Uzalendo wa nchi) haupo hivi sasa.
ReplyDeleteHebu jiulize, tu hata hawa waandishi wa habari wanashindwa kuandika habari kwa umakini na kutoa figure sahihi Mara meli ilikuwa na watu 601, 650,wamekufa watu 192 je meli ilibea watu wangapi? nivyema mkatoa idadi ya watu waliopatikana hai na wanaoendelea upatikana wakiwa wafu ili mwisho wa siku tuwe na takwimu sahihi juu ya suala hili.
Naungana na watanzania wote katika kipindi hiki kigumu kwani huu ni Msiba wetu sote Mungu azilaze Roho za Marehemu mahali pema peponi.na awarejesheshee afya njema majeruhi wote wa ajali hiyo mbaya.AMINA
Kwa kweli habari ya kustusha sana. tuzimdi kumuomba Mungu ili kuepusha majanga zaidi.
ReplyDeleteInshallah Mungu atupe subira.
Jaliath, DSM.
Poleni sana wafiwa wote, Mungu awatie nguvu.
ReplyDeleteKwa kweli ni msiba mkubwa na wakusikitisha sana. Tunaiomba serikali kupitia mamlaka husika kuwa makini na kiwango cha abiria sio tu kwenye meli bali hata vyombo vingine kama daladala n.k. Inasikitisha kuona chombo chenye ubovu ambacho kingeweza kubeba watu 300 kimebeba watu 2000 na kuruhusiwa kusafiri. Sumatra mko wapi?, Askari wa usalama mko wapi? serikali tunaomba mfanye kazi angalieni jinsi yatima wanavyoongezeka tunaenda wapi? Mtukufu Rais tunaomba mamlaka yako ifanye kazi na tahadhari ziwekwe kila sekta.
ReplyDeletePoleni sana ndugu zangu mliokumbwa na msiba huo mzito tuko pamoja.
Jast DSM
jaman polen watanzania wote kwaujumla hilo ni pigo letu sote kutokana na uzembe wa watu wachache.hiv tanzania tutaelimika lini na kuwa waelewa lini hivi meli inabeba watu kazaa kwa nini wazidi?na ni jukumu la nani kujua hii meli watu wametosha?na sisi watanzania wewe umeona gari au meli imejaa we unataka kwenda ilimradi ufike sasa yana tukumbumba kama hayo.mungu ailaze roho za marehemu peponi amina!!!!...
ReplyDeleteSifuni: dar es salaam
ReplyDeletePoleni watanzania wote mlipoteza ndugu na jamaa katika ajali hii mbaya na ya kusikitisha sana. Huu ni msiba wetu wote kama watanzania, tupo pamoja katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, Naomba Mungu awafariji wafiwa wote, Poleni sana.
hili kweli ni janga kubwa kwa taifa kwa kupoteza ndugu na jamaa ambao ni muhimu sana katika ujenzi wa taifa kwa uzembe wa watu wachache. naomba watanzania hasa wamiliki wa vyombo vya usafiri wasije wakataka kujifunza baada ya kutokea jambo hali wakijua nini kitatokea baada ya kutenda/kuruhusu watu kujaa kisa tu cha kuangalia pesa kuliko maisha ya watu ambao ni muhhimu sana katik ujenzi wa taifa letu. poleni sana watanzania wenzangu. Mungu azilaze roho za marehemu. Amina!
ReplyDeleteInnocent Mtegwa
Huu ni uzembe ulio kithiri kwa mamlaka husika kama sumatra ambao waliacha inapakiza mzigo kkupita kias,na pia kwa kikos cha wokovu ambacho kilizubaa tangu meli inaanza kuzama saa7:30-9:00 haliyakuwa wana taarifa. Serikali inapaswa kuwashuhulikia.
ReplyDeleteKOBA DSM
Poleni sana ndugu zetu mliopatwa na janga hili moja kwa moja pamoja na ndugu na jamaa zenu, na watanzania wote kwa ujumla.
ReplyDeletePamoja na kuwa si wakati sahihi sana wa kuyasema haya, imefika mahala tuangalie mambo haya kwa marefu na mapana. serikali ichukue nafasi yake kama mlinzi wa watu na mali zao, mtunga sheria na msimamizi wake ili haya mambo yawe hadithi kuliko kila siku tunazembea halafu badala ya kuweka juhudi katika kuzuia maafa, tunakuwa wa kwanza kutoa pole yanapotoea. Ajali kwa dunia ya leo zina kinga, tukisimamia mambo yetu sawasawa kutokea itakuwa kwa nadra sana na hata namna ya kukabiliana itakuwa ya ufanisi zaidi kuliko hivi sana. Naamini, kuna mtu/ watu wamelala usingizi, hawatimizi wajibu wao. Mungu tunusuru waja wako.
kwakeli inaskitisha sna kuskia habari nzito kam hizi inshallah mungu atawaafu wote waliojeruhiwa na aliotangulia mbele ya haki mungu atawalaza mahali pema peponi ameeen, ila mie ningeomba serikali wawemakini sna katika maswala haya kma ilishatokea mara kadhaa bac pia wajitahidi waweza kuzicontrol rushwa ninazotendwa na wananchi wenzetu ili kupunguza ajali kutokea tena. assalam alaykum! Munira Nassir Abdul-rahman. kutoka Malaysia
ReplyDelete