Naibu Katibu Mkuu wa sekretarieti ya Hay- Atul Ulamaa Tanzania,Sheikh Mohammad Issa (kulia) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo wakati umoja huo ulipotoa tamko lao la pamoja kuhusu kitendo cha Chama cha CHADEMA kutoomba radhi kwa waislamu kufuatia kitendo cha udhalilishaji wa kumvua hijjab Mkuu wa Wilaya ya Igiunga, mkoani Tabora, Mama Fatma Kimario. Kushoto kwake ni Katibu wa sekretarieti ya Hay- Atul Ulamaa Sheikh Sherally Hussein.
Katibu wa sekretarieti ya Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (Hay- Atul Ulamaa) Sheikh Sherally Huseein (kulia) akitoa tamko kwa waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo kuhusu wafuasi wa Chama cha CHADEMA kukaidi kuomba radhi kwa umma wa Kiislamu kufuatia tukio la udhalilishaji kwa kumvua Hijjab Mkuu wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Mama Fatma Kimario hapo septemba 15 mwaka huu. Katikati ni Naibu Mwenyekiti wa Umoja huo, Sheikh Abdallah Bawazir na kushoto ni Sheikh Manzi Said Manzi wa taasisi ya MWINYI MKUU.
Picha ya pamoja ya viongozi wa umoja wa wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (Hay- Atul Ulamaa).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Jamani ndugu zangu na viongozi wangu wa dini toka lini siasa zikaingizwa kwenye dini maana kama kweli mnazingatia dini huyu mama kaolewa na mkristo je nindoa gani imefungwa je inarusiwa.Tusikurupuke matokeo yake tunaambiwa wachochezi

    ReplyDelete
  2. Jamani ndugu zangu waislam Tusikubali kutumiwa kwenye mambo ya siasa viongozi kama nyie mnaposhutumu chama fulani kipindi hiki cha kukaribia uchaguzi ni sawa na kuwaambia waislam wa igunga wasichague Chadema.Chakujiuliza yule mkuu wa mkoa alivuliwa kweli hijabu!! au mtandio ndio Hijabu!! Halafu masuala yako mahakamani kwa nini mnayazungumzia, hatukawii kusema viongozi wetu sasa mnatumiwa na chama Tawala. subirini watu wachaguane tar 2 ndio muanze kushutumu chadema, kuishutumu sasa hivi ni sawa na kuambia jamii yetu ya kiislamu isichague Chadema.

    ReplyDelete
  3. Wakati waislam tunaongelea kitendo cha Muislam aliyeolewa na Mkristo kuvuliwa "mtandio" tunaacha kuzungumzi mambo ambayo ni muhimu zaid kuyazungumzia ili kuokoa jamii zetu

    Mfano mzuri ni wanaharakati wa TGNP kudai haki sawa kwa MASHOGA na kuwaleta kwenye hadhara na kuwalipia gharama zote na kuwapa nafasi ya kuutangaza USHOGA hadharani bila kificho

    Hili ni jambo ambalo tunapaswa kulipa kipaumbele kikubwa zaidi ila simaanishi kwamba na hili liachwe lakini tayari hatua zimeshachukuliwa hatuna haja ya kulizungumzia tena lakini hili la USHOGA hakuna yeyote aliyelikemea.

    WanaDINI tuamke sote maana hakuna dini inayomtambua MUNGU ikakubali USHOGA

    ReplyDelete
  4. yeah hata mimi nawasupoti viongozi wa dini na nawasaidia kuiasa jamii isiwachague kabisa chadema sababu ni chama kinachowabagua waislamu na ukabila,ukanda,ubepari ndio sera zao.

    ReplyDelete
  5. dini na siasa wapi na wapi na je msituhumu tu kwamba chadema imemvua nguo huyo mwana mama but je huyo mama kwenda kupiga kampani ilikuwa haki au kuhusu hili mi naona chama cha CCM kinawatumia hawa waislamu kutaka kuwaj hawaengea picha mbaya chadema kwa waislamu ili wasiwapigie kura chadema mi nawashauri hawa wazee wa kiislamu watumie busara hekima wasikurupuke tu kuituhumu chadema WAISLAMU MPAKA LINI ELIMIKENI JAMANI KITU KIDOGO VIKAO VISIVYO NA MAANA MBONA HAMKAI KUJIULIZA UCHUMI INAENDAJE MAISHA YAMEPANDA NI MUDA MUAFAKA SASA KWA WAISLAMU KUELIMIKA MTAISHIA KULALAMIKA MPAKA LINI AMKA MWISLAMU.

    ReplyDelete
  6. Ignorance is a bliss!.. you can not cure it!!

    ReplyDelete
  7. Kwanza Naungana Mkono na waliochangia hapo juu wote wawili! Mimi naongezea tu kidogo! Ni kwamba kama kweli hao wanasuoni wanauchungu sana na Dini ya Kiislamu, Kuna Mambo mangapi wanafanyiwa waislamu na wala sijawahi kuwasikia wakikemea au kujitokeza hivyo? Kwa ufupi wapo kisiasa zaidi, Na DINI + SIASA = VIFO chonde chonde Ushabiki wa siasa katika dini ni NOMAAA.

    ReplyDelete
  8. Njaa mbaya jamaniii!!!!

    Yule mama ni Mkatoliki na ana mashamba kibao ya nguruwe na yeye ni miongoni mwa wasambazaji wa kubwa wa nyama ya nguruwe jijini Dar!!!!

    Kweli waislamu tunamtetea mtu kama huyo???? Mi si shabiki wa CHADEMA ila kwa hili kwa Waislamu wenzangu nalipinga kabisaaaaaaa!!!! Hata kama tumekosa shule kiasi gani na kutumiwa na vyama vya siasa lakini si kiasi cha kutetea watu kama hao!!!! Tutumie busara kidogo tunajidhalilisha

    Waislamu twendeni shule kwa kweli tunakoelekea ni kubaya

    ReplyDelete
  9. unapoenda sokoni hawaulizi kama una hijabu au la, ukipeleka mtoto shule, ukiwa bna hijabu hupunguziwi bei..... watanzania wa leo sio wa jana wa kupelekeshwa pelekeshwa....

    ReplyDelete
  10. Sina haja ya KUGOMBANA na ndugu zetu waislam, bali natoa angalizo kwa hawa wachache wanaotumia "kivuli cha uislamu". Binafsi natafsiri kuwa huu ni utafutaji shwari na uchonganishi usiokuwa wa lazima. Dini ni upendo, Dini ni uvumilivu, Dini ni maelewano, sijaona kitabu cha Dini kinachohimiza kisasi, hii ilikuwa enzi za Agano la Kale baada ya Agano jipya hamna ulipizaji kisasi.Ninashangaa hawa wakina Shehe Hussein na wenzake wanatangaza kupambana na wale wote wanaopinga Uislamu, this is ridiculous haisaidii kupambana na wanaopinga vita UISLAM kwani haitatoa funzo, ninaamini kama kuna yeyote anayepinga Uislam asaidiwe kwa kuelimishwa kwa upole na uvumilivu ili aweze kuuelewa uisalamu na aone anachofanya (upigaji vita Uislam) si jambo jema.
    Unapoamua kupambana naye wewe unayejihita Muislam utakuwa umetenda dhambi ya kulipiza kisasi. Hata kilichofanywa na CHADEMA was based solely on DC misconduct and not religious aspect. CHADEMA hawakuwa na muda wa kujiuliza huyu DC ni muislamu au ni Mkristo? Walipoletewa taharifa za ghafla zilizopelekwa na wapenzi wa CHADEMA kwamba kuna illegal meeting, CHADEMA wali take impromptu action ya kumfuata na kumtoa kwenye mkutano, hakuna hata mmoja aliyefikiria swala la Dini. Zaidi ya hayo tunaambiwa DC ni Mkristo alibadili baada ya kuolewa na mkristo, na huko kwenye nyumba yao Mbezi DSM wanafuka nguruwe, sasa hawa wanaojiita wanatetea Uislamu nani aliwaambia kuwa Dc ni mwislamu? Tuache kuingiza mambo ya Dini kwenye Siasa,tuache kukurupuka, tutafute sababu za msingi na wala sio utengenezaji wa sababu zisizokuwa na mashiko. Tuache kutumiwa na wanasiasa, cha kushangaza hawa wanaojihita wanapigania kuzalilishwa kwa uislamu iliwachukua siku kadhaa kabla ya ku react, walikuwa wanasubiri nini siku hizo zote? Kama sio kutengeneza kesi ya kupika?

    Kimbache Benedict

    ReplyDelete
  11. Waislamu wamenyanyasika katika nchi hii tangu kuhasisiwa kwa TANU,CCM,CHADEMA na kadhalika.Waislamu walikuwa salama ndani ya TAA pekee.Sio kweli kuwa waislam hawana elimu kwani hii ni hulka iliyopikwa hata ndani ya wazee wetu wakahasisi chama cha siasa baada ya tabu zote akaja mtu hajui hata kuvaa suruale ikasemwa kuwa huyu elimu yake ndiyo sawa.Waislam wasiposema basi kwa UNYANYAPAA huu kila siku watakuwa dhalili.Suala ya huyo mama ni kuwa mwanamke amedhalilishwa lakini hajuwa amevaa hijabu labda kutokana na kukithiri kwa uovu dhidi ya waislam ndipo masheikh wangu wakalichukuliwa kwa nguvu kubwa.Kuna watu wanasema dini ni upendo mbona dhuluma dhidi ya waislamu hawasemi ni upendo upi usio na haki?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...