Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Joel Bendera (kulia) akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bw. Emmanuel Humba (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko huo, Ally Kiwenge (wa pili kushoto) baada ya kufungua kongamano la saba la mwaka la wahariri wa habari na waandishi waandamizi la kujadili taarifa za utafiti wa huduma za NHIF nchini. Kongamano hilo la siku mbili lilianza jana mjini Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia), akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari,baada ya kufungua kongamano la saba la mwaka la wahariri wa habari na waandishi waandamizi la kujadili taarifa za utafiti wa huduma za NHIF nchini. Kongamano hilo la siku mbili lilianza mjini Morogoro.Jennifer Sumi wa gazeti la Mwananchi na Scolastica Mazula wa Redio Times FM, wakiwa katika kongamano hilo

Said Mmanga kutoka gazeti la Changamoto, akitoa taari ya utafiti kuhusu upatikanaji wa huduma za afya vijijini walioufanya na Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, George Marato katika Mkoa wa Mara.

Beda Msimbe wa magazeti ya Serikali ya Daily News na Habari Leo, akitoa taarifa ya utafiti wa huduma zitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), katika Mkoa wa Ruvuma.

Mwandishi wa habari mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Grace Michael akitoa taarifa ya utafiti wa huduma za afya zilitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), katika Mkoa wa Kigoma.Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia), akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari,baada ya kufungua kongamano la saba la mwaka la wahariri wa habari na waandishi waandamizi la kujadili taarifa za utafiti wa huduma za NHIF nchini. Kongamano hilo la siku mbili lilianza mjini Morogoro.


Baadhi ya wahariri wa habari na waandishi waandamizi wakiwa katika kongamano la saba la mwaka la kujadili taarifa za utafiti wa huduma za NHIF nchini, lililoanza jana mjini Morogoro.

Wachora vibonzo Nathan Mpangala (kulia) na King Kinya wakisikiliza kwa makini wakati wa kongamano likiendelea.Baadhi ya wahariri wa habari na waandishi waandamizi wakiwa katika kongamano la saba lamwaka la kujadili taarifa za utafiti wa huduma za NHIF nchini, lililoanza jana mjini Morogoro.

Picha zote na Kamanda Richard Mwaikenda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...