Kijana anaejishughulisha na biashara ndogo ya uuzaji wa Mihogo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja akigeuza mihogo hiyo mchana wa leo kama alivyokutwa na kamera man wa Globu ya Jamii.Vijana wengi wa jijini Dar hawapendi kujishughulisha namna hii hali inayowapelekea wengine kujiingiza katika uizi na wengine kutumia madawa ya kulevya.Hivyo Globu ya Jamii inawapongeza vijana wa namna hii na kuwataka wale wengine kuiga mifano ya namna hii ili kuendelea kujenga Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Enzi zile za IFM, ndio ilikuwa lunch hio Uncle. Tulikuwa tunaita Pizza.

    ReplyDelete
  2. Hiyo ni lunch kwa wafanyakazi wengi wa mjini na hasa ikikaribia mwisho wa mwezi.

    Umenikumbusha wimbo mmoja nimeusahau kidogo ulikuwa unaanza 'tarehe 15 mwisho wa mwezi....'

    Uliimbwa na Mkenya mmoja (wao huwa wanapata mshahara kila baada ya wiki mbili)

    ReplyDelete
  3. Jamani kiswahili kigumu? sio UIZI ni Wizi...

    ReplyDelete
  4. Nafurahishwa mno kwa wito uliotolewa kwa vijana kujishughulisha na kazi. Kazi kama hii humwezesha mtu kujikimu kimaisha. Wanao kusomeshwa na hata kupata chakula muda wowote.
    Mimi ninaloshamba la Mihogo na limesheheni chakula hicho. Nakaribisha wanunuzi kuichukua shambani Morogoro, Bigwa (0715 368052).

    ReplyDelete
  5. tatizo hatuna mipango madhubuti ya kuwawezesha vijana wa namna hii kufanya kazi kwa utulivu na kujiamini. hapo alipo anatazama huku na kule maana wakati wowote watakuja mgambo wa jiji watamzoa na toroli lake jamani. sasa vijana tufanyeje? tuibe? tule wapi? mbona hivi jamani? kwani kuna anayependa maisha ya kuiba wakati akijua wazi kwamba wakati wowote kifo kibaya kinamsubiri? hatupendi, tunalazimika.

    ReplyDelete
  6. Jitihada ya kijana kwa kujishughulisha kuchoma mohogo ni dira ,msaada kwa jamii ya walio chini kupata angalau mlo wa lunch kazini, na mfano mwema...tujitahidi kuwapa fursa zaidi kwa maendeleo yetu na sio tena kuwatumia Mgambo wa Manispaa kuwakwamisha!

    ReplyDelete
  7. Utamu wa hiyo mihogo mchomaji awe na mafua makali yanayochuruzika!!!

    ReplyDelete
  8. E bwana wee unakumbushia mbaaalii!Kuna babu mmoja alikuwa akiuza mihogo ya kuchoma bei poa kweli na wakati mwingine watu walikua wakimwibia waziwazi lakini yeye atii neno, siku ya siku siri yake ikapatikana polisi wakaja wakamkuta na mafurushi kiba ya misokoto ya bangi.

    ReplyDelete
  9. Heehhe, heeeh, mitamu hiyo imenikumbusha mbali sana, enzi hiyo tuliita CHIPS DUME!!!!!. Maana ukila asubuhi na chai mchana unaweza pita bila kusikia njaa. Hapa majuu si mitamu kama ya Africa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...