Kaka,

Ni mara kadhaa nimeshaona humu kwenye Bulogi yako majadiliano ya diskasheni juu ya baada ya kuinunua na kuivaa suti, zile Lebo zinazobandikwa Sutini, kwenye mikono kwa nje, zing’olewe au zising’olewe?

Sasa Kaka hivi karibuni na mimi nilibahatika kwenda Dubai, nikapita kwenye duka la Shoping Mol, nikanunua shati la JINZ (hilo linaloonekana hapo pichani) ambalo kwa kawaida wakati wa kuvaliwa huwa halichomekewi ndani ya suruali.

Sasa chini kabisa baada ya kumaliza vifungo kuna hiyo ze lebozzzzz ambayo kwa kuwa hapo ilipo hakuna kifungo na shati halichomekewi basi nikilivaa ze lebozz inaonekana.

Swali langu ni kwamba Je na Ze lebozzzz hizi kwenye mashati haya ya JINZ zinapaswa kung’olewa wakati wa kulivaa au niiache hapo nilivae hivyohivyo?

Naomba msaada wako na wa Wajuzi wa haya mambo ili nisije nikalivaa hivyohivyo nikachekwa na Waosha Vinywa.

Nawasilisha.

Mdau, Perez

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Tehtehteh Leo nimecheka sina mbavu Mkuu bora umeuliza umetusaidia wengi na mie ninalo shati la Lebozzz tehtehteh.

    ReplyDelete
  2. Hilo shati ulilijaribia kabla ya kulinunua?

    ReplyDelete
  3. ulaya mbona watu wanavaa jamani, shida ni nini wabongo? mbona tuna kuwa washamba, tunajali vitu visivyokuwa na msingi??? ebooo!
    Lebo haing'olewi

    ReplyDelete
  4. hata msemeje kwenye suti ni nooo full stop!

    ReplyDelete
  5. Kwa kifupi, label zinazotakiwa kutolewa utaona zimeshikizwa tu kwa uzi na sio kushonewa kabisa. Kwa wale wavaa suti, label za mikononi japo pia umezinunua lakini ni za kutoa. Ushamba upo hata ulaya hivyo cha kutoa ni cha kutoa tu. Label ya mshikaji kwenye shati la jeans, hiyo haikukusudiwa kutolewa japo watu wengine huamua kuitoa ili wasijulikane wamenunua kwa designer gani, hasa kama ni cheap designer. Maamuzi ya mwisho ni ya mvaaji na jinsi anavyojisikia lakini label ni za kutoa. Amen.
    Mdau Allen.

    ReplyDelete
  6. teh tehe teh,me napita tu

    ReplyDelete
  7. Lebo kama hapom unaiachaa tuu. Kwenye suti ndiyo yaku toa

    ReplyDelete
  8. WEWE MDAU WA HUKO AFRICA TOA TONGO TONGO MACHONI HIO NI NEMBO YA BIASHARA YAKE HUYO DESEGNER , KWANINI MNAVAA NIKE; ADIDAS; GEORGIO ARMANI? AU WEWE UNAWEZA KUNYWA COCACOLA ISIOKUWA NA LABEL?

    SASA KWA NINI ULIKWENDA NUNUA DUBAI ?WHY NOT HAPO BONGO? NA WEWE NENDA CHINA KASHONESHE NGUO ZAKO NA UWEKE NEMBO YAKO HAKUNA ATAKAE KUJA NA KIPINGAMIZI ATAKAETAKA NUNUA ATANUNUA; SIO BAADA YA KUNUNUA NDIO UANZE COMPLAIN HII NDIYO DUNIA YA MIAKA ELFU MBILI BAADA YA YESU!

    MDAU LONDON

    ReplyDelete
  9. Nafikiri lebo kuwepo au la siyo big deal hapa, vaa pendeza endelea na mambo yako ! ni vitu vidogo sana hivyo wabongo na hakuna sheria iliyowekwa juu ya hilo.

    ReplyDelete
  10. HILO SHATI KAMA LINAVYOONEKANA NI (V) LA KUCHOMEA SIO LA NJE NA KUONYESHA LEBO NI UTASHI WA MTU, MAANA KILA MMOJA NA UTASHI WAKE. LAKINI KUZIONYESHA LEBO NI USHARUBARO WA MTU KUJIONYESHA KUWA NI BAAB KUBWA!!!NI KUZINGO'A TUU.
    HASA ZA SUTI INABIDI UZISOME KABLA HUJAUZA SURA.

    ReplyDelete
  11. http://www.youtube.com/watch?v=JGEljQFUx6E

    Mambo ya Kopi endi Pastiii haya hapa.

    ReplyDelete
  12. Lebo ziachwe zisitolewe. Zinatoa amelezo ya nguo kufuliwa, kupasiwa ama la nk.
    Exksept lebo zilizoshikizwa na uzi tu unaweza kutoa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...