Na. John Kitime.


Kuanzia album ya kwanza ya Tancut Almasi Orchestra , bendi iliendelea kutoa vibao vilivyoweza kudumu katika kumbukumbu za wote waliovizisikia kuanzia enzi hizo, album ya kwanza ilikuwa na nyimbo kama vile, Nimemkaribisha nyoka(Kasaloo Kyanga), Kashasha(Kyanga Songa), Tutasele (Kasaloo), Mtaulage(John Kitime), Big Four(Utunzi wa wimbo huu ulileta utata kwani ulianza kwa ugomvi kwa Mamado Kanjanika kudai kuwa aliutunga yeye wakati akina Kasaloo na Kyanga wakidai wameutunga wao.


 Lakini hatimae akina Kasaloo waliacha ugomvi huo na Mamado hutajwa kama mtunzi wa wimbo huu. Hebu angalia mambo yalivyokuwa wakati Kashasha likipigwa. Niko hapo na miwani kubwa nikiungurumisha rhythm guitar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. namuona kawelee enzi za ujana wake,sio mchezo, Tancut walitisha enzi hizo,sijui lini tena muziki kama huo utarudi tena. Big up Kitime kwakutudondoshea hiyo,tunangoja kama utatudondoshea mtaulage. Mdau London.

    ReplyDelete
  2. Ahsante sana kitime, naomba utundondoshee SAFARI SIO KIFO,machozi hunitoka sana, kuna siku ulimpa nafasi kasoloo pale msasani mkiwa na njenje ilinikumbusha mbali sana.

    ReplyDelete
  3. Naona Bro Kitime ulikuwa staili ya pekee ya kucheza....Mapacha wakaona wakufunike!!!!...anyway,..welldone.

    ReplyDelete
  4. Bro Kitime wanikumbusha mbali sana, kwani nalikuwa natoroka hata prep time pale Lugalo sec.school siku za hao jammaa na wewe. Club ya tancut niliipenda sababu yenu ingawa ni dent
    la nguvu. Sasa nipo huku kwa OBAMA, je hiyo album nitaipataje? tuwasiliane kwa e-mail hii kipen_84@yahoo.com. Asante sana mzee.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...