hebu angalia gari jinsi linavyoonekana,yaani hata haliyofautiani na hizo takataka zinazobegwa na gari hilo.
yaani limechoka mpaka linatia huruma
tairi zake ni vipara ile mbaya,yaani zimeishaaaa......
hivi ndivyo linavyoonekana kwa mbele.
huu ni mlango wa dereva na kuna stika safiii inayotoa ujumbe mwanana.
Takataka inabeba taka
ReplyDeleteHILI GARI NILAKUTUPA JALALANI LAKINI WAKULAUMIWA HASA NI SEREKALI YETU HAINA MFUMO WA MAGARI MABOVU KUYAPIGA MAFUKU KUONEKANA BARABARANI KUNA MAGARI YA ABIRIA DALADALA YAMECHOKA KAMA HILI GARI LATAKA
ReplyDeleteyaani lenyewe tu ni takataka tosha halafu bado linabeba takataka.
ReplyDeletelenyewe ni taka kisha linaendelea kudondosha taka mitaa yoote
ReplyDeleteMbona gari lenyewe ni TAKATAKA
ReplyDeleteHuwezi amini linaoa taka maeneo ya msasani na mitaa ya karibu karibu na masaki!
ReplyDeleteHivi Watanzania tutaelimika lini? Tukipigania vyama vingi walioko madarakani hawataki kuachia ngazi. Ivi kweli serikali hailioni hili jamani? Alafu tena daa uso wa tz! aibu kubwa acheni wazungu watucheke upunguani tunao sijui tumelaaniwa na nani. Gari ni uchafu tosha kuliko takataka lilizozibeba. Asante sn Michuzi kwa kulimulika hili.Ndio yanaleta ajali haya.
ReplyDeleteMdau USA
Lenyewe tu ni takatakaa
ReplyDeletehilo gari lenyewe takataka,sasa sijui tunapunguza uchafu au tunaongeza..mawazo tu hayo
ReplyDelete"Kwa pamoja tutauboresha utumishi wa umma" Shame on you na vipeperushi vyenu! Mnaboresha au mnabomoa? Gari gani hili la taka linaloeneza magonjwa barabarani? Serikali yetu inapoelekea si pema. Kila mahali ni noma kwa sasa. Mashuleni watoto wanakalia kanga madawati hakuna, hosp kitanda kimoja watu watatu, maji umeme, mafuta juu. Tutaponea wapi jamani?. Miaka 50 ya uhuru!!!? Michuzi usibanie ujumbe wangu.
ReplyDeleteMimi nakataa hiyo siyo Tanzania. Hii picha imepigwa sehemu nyingine na kubandikiwa stika ya Tanzania. Nakataaaaa.....Huu ni mwaka 2011, mwaka wa hamsini toka tupate uhuru. Hatuna magari ya umma kama hayo. Bongo ni tambarare...acheni kutupaka matope namna hiyo.
ReplyDeleteTakataka namba moja ni gari lenyewe
ReplyDeletelenyewe takataka
ReplyDeleteHilo gari linabidi kupelekwa kwenye makumbusho ya Taifa.
ReplyDeleteweldone mtoa habari na picha!, do your part.
ReplyDeletePamoja tutafika!
Wameshindwa kuliweka gari vizuri hata kama ni lakusombea takataka walau gari lingekuwa katika hali nzuri gari limechakaa uchavu namna hii kweli hapo watakumbuka kuwajibika katika kuondoa uchafu katika maeneo usika gari lenyewe ni kama takataka
ReplyDeleteYaani jamani hii gari yenyewe ni takataka,inachafua mazingira.kweli tutafika?mdau wa lincoln.
ReplyDeletehalafu lina stika ya wiki ya kwenda kwa usalama kuonyesha kwamba limekaguliwa na linafaa kutembea barabarani
ReplyDeleteTunaweza kubinafsisha hii sekta kama Saudi Arabia. Saudi walikuwa na hili tatizo na wengi wao hawakutakana kufanya hii kazi.Wakawapa contract kampuni ya marekani wamarekani Waste Management na jamaa wakashusha vitendea kazi vya kisasa na miji yao iko safi kabisa.
ReplyDeleteAliesema TZ ni nchi ya ajabu sana duniani hakukosea :) Yaani nimecheka hapa.
Acheni kelele nyinyi watu wa ughaibuni. Sasa unataka serikali inunue gari la mamilioni la taka wakati magari ya kubebea wagonjwa hakuna. Vijijini huko hata zahanati hakuna, eti wanataka magari mepya ya TAKA. Kama mnataka magari mazuri lipeni kodi ya kutosha. UKerewe kodi ya kila nyumba kwa mwaka ni £1200, ndio maana wana magari mazuri. UKerewe mpaka TV inailipia kodi. Wenzenu vijijini hata hiyo barabara hakuna, usafiri wa punda.
ReplyDeleteNi gari la serikali au binafsi.Kweli kama ni la umma huu ni ufisadi na ni aibu wanakataa magari ya Uk yaliyozidi miaka 10 na kutoza ushuru mkubwa.Hili gari sitaki lipite mtaani kwangu litanichafulia hewa.
ReplyDeletemithupu ungempiga picha na dereva wake tumuone bana!
ReplyDeleteTAKATAKA HUBEBWA NA MAGARI TAKATAKA.
ReplyDeleteHIVYO HUCHANGIA SANA KUENEZA MAGONJWA KWANI BAADHI YA TAKA HUDONDOKA SANA NJIANI WAKATI ZIKIPELEKWA DAMPO NA PIA WANAOZIPAKIA HAWANA MAVAZI MAALUMU WALA ELIMU YA AFYA KWANI HUJA KULA ULAIANI KWA MAMA NITILE BILA HATA KUBADILI MAVAZI WALA KUOGA NA KUJIPULIZIA DAWA MAALUMU.TUTAKUFA SANA.
kamw wengine walivyosema, gari lenyewe ni takataka. je wanaopaswa kusimamia hizo sheria ni akina nani na wamiliki wa hivyo vyombo au hizo kampuni za kuzoa uchafu ni akina nani. utakuwa wanaosimamia sheria hizo ndio wamiliki au wenye hisa kubwa kwenye hayo makampuni.
ReplyDeletenani asiyejua kwamba asilimia kubwa ya break down ambazo ni mbovu pia zinamilikiwa kwa asilimia kubwa na polisi. ajali inapotokea na polisi kuja kupima, basi utakuwa/utaona yeye ndie anampigia mtu wa break down aje kuvuta gari.
Tatizo sio gari, mnalaumu kitu hakina akili!!!!!!!!? gari linakufa ki sabuni.
ReplyDeleteGari yenyewe ni takataka tosha. Sasa tungufunguwe macho na akili jnsi nchi ilivyo na ufisadi mtu akipeleka gari bongo atapigwa ushuru mkubwa mpaka akome na kuulizwa MOT ya gari na kadhalika. Je hayo yaliyo ya kwao kama hili lina MOT kweli au yanafanyiwa MOT magari ya bongo au kwa yanayo ingizwa tu ili kukukomoa kwa uhasidi. Fanyeni haki kwa kila mtu, ile mtu kuwa aghaibuni ni kutafuta maisha ili asaidie nyumbani sio kukomoana
ReplyDeleteRUSHWA...inanuka hapa kwa mazingira jinsi Mkandarasi huyu wa kuzoa taka alivyoipata kandarasi hii.
ReplyDeletehalafu likiua watu... tunasema ni ajali.. tunasema bahati mbaya, ajali wapi... wakati ni maksudi.
ReplyDeleteIssue si uchafu, issue ni hatari kwa maisha ya binadamu. Ndio maana magari yanakaguliwa. Sasa hili limepita kigezo chochote cha usalama?
sisi ni wajinga..
Nilipokuwa Dar es Salaam mwaka huu, niliwaona wazoa takataka ambao wanazunguka na magari ya aina hiyo. Hawana vitendea kazi kwa ajili ya kazi yao hatarishi. Hata viatu hawakuwa navyo. Wanakanyaga hizo takataka wakiwa peku peku, na wanazipakia kwa mikono peku peku. Hawajavaa chochote usoni cha kuzuia wasivute vumbi na hewa chafu. Nilishtuka sana, nakahofia afya zao. Na kweli, hawawezi kuwa ni wazima kiafya. Papo hapo, ukiangalia magari ya fahari yanayokatiza humo mitaani, utaona wazi kuwa Tanzania haishindwi kununua magari bora ya kuzolea takataka. Utaona wazi kuwa Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu.
ReplyDeletembona mchuma bado upo bomba kabisa unaweza kupiga kazi mpaka mwaka 2020
ReplyDeleteWAKUBWA WANASOMA HIZI?????
ReplyDeleteAnyways, naomba msimamizi wa gari hii aitunze zaidi.... siku Yule waziri mkuu wa Ukerewe akija, ndiyo limo ya kumpokelea pale Airport...Halafu aelezwe "hivi ndivyo tunavyoyapenda mawazo yako." ..Nakubali - gari halina kosa....._______________.