Mbunge wa Mafia, mkoani Pwani, Abdulkarim Shah, akiwa kwenye boti aliyoikodi kwa ajili kusaidia kuokoa wananchi wa maeneo ya Jangwani jijini Dar es salaam leo,  akitoa maelekezo kwa nahodha ni sehemu gani ya kupita wakati alipokuwa akishiriki katika kuwaokoa baadhi ya wananchi  waliokumbwa na mafuriko. 


Msongamano wa magari eneo la Daraja la Selander, pande zote mbili za barabara zilikuwa zinaruhusu magari kutoka mjini ili kupunuza adha jijini, baada ya barabara nyingi kufungwa kutokana ma mafuriko.

Wananchi wakitembea kwa miguu baada ya kukosa usafiri eneo la Daraja la Selander, Dar es Salaam

Wananchi wakiangalia mafuriko eneo la Vingunguti

Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah, akimpokea mtoto aliyekuwa amehifadhiwa juu ya paa la nyumba, pamoja na msichana mmoja wa nje ya nchi, aliyejitambulisha kwa jina la Janne Borold, aliyekuwa naye sambamba katika kusaidia kuwaokoa wananchi hao. 
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo, wakiwa wamejikusanya kusubiri boti iwaokoe eneo la Spenco Vingunguti. 

Baadhi ya vijana wakijitolea kuwaokoa watoto wa maeneo ya Spenco Vingunguti.Gari likipita kwenye mafuriko likitokea Ubalozi wa India, Dar es Salaam.


Sehemu ya Daraja la Selander, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Dar es Salaam, ikiwa imebomoka kutokana na mafuriko. 

Hali ilivyokuwa katika daraja la Jangwani. Mawasiliano ya usafiri yalikatika katika eneo hilo kwa kuhofia magari kuzama. Picha na Richard Mwaikenda


Gari la Serikali namba STK 3316 likiwa limetumbukia kwenye daraja lililobomoka kutoka na mvua iliyonyesha leo eneo la Makondeni kwa Mahita, Mbezi, Dar es Salaam. Dereva na abiria waliokuwemo walinusurika kwenye ajali hiyo. 


KWA PICHA ZAIDI,BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 45 mpaka sasa

 1. jamani m'mungu atunusuru, mlipuko wa vipindu pindu

  ReplyDelete
 2. Ewe Mola wasaidie ndugu zetu hawa na uwakinge na milipuko ya maradhi. Lakini ningependa kuwakumbusha ndugu zangu Watanzania tumuogope Mungu Jamani, hii ni kuonyesha kua tukiendelea na mwenendo wetu wa maasi i.e. Ulevi, starehe, uzinzi, ufisadi na kadhalika basi tujue huu ni mwanzo tu.
  Maana kila siku ukiangalia habari za Bongo watu wanazidi kumsahau Mwenyezi Mungu na kujikita katika ulimwengu kama vile hakuna mwisho. Tujue ya kwamba inapokuja adhabu ya Muumba kwenye Taifa lilojikita katika maasi haijali wazee, watoto, wake kwa waume au wacha mungu. Kwani wacha mungu wamekua kimya kukemea maasi katika jamii.

  ReplyDelete
 3. Huu ndio mfano wa kiongozi wa kuigwa. Jiulize all the way from Mafia na kuokoa watu wenye mahitaji.
  Majimbo mawili tofauti haya. Jiulize wa Kinondoni alikuwa wapi kuokoa wapi, ama ndio alikuwa anafanya ziara ya kuangalia maafa.
  Welldone mbunge, wastahili kuitwa Mheshimiwa

  ReplyDelete
 4. ndugu asante kwa picha,sie tulio nje ya TZ tupate kuona hali halisi,kuna sehem nimesoma mvua kama hiyo haijawahi kutokea miaka 57 iliyopita.ni hatari sana,haswa hao walio juu ya paa nyumba ina weza kubomoka.pole ndugu zetu.

  ReplyDelete
 5. tuwekee picha zaidi,hata video pia.tuna shukuru kwa picha

  ReplyDelete
 6. Mko wapi viongozi wa Dar es salaam, nahisi ni Aibu nyie hamuonekani but mbunge wa mafia anajitoa muhanga kusaidia wapiga kura wenu

  ReplyDelete
 7. Where is Disaster Recovery Strategy?

  ReplyDelete
 8. Achilia mbali kipindupindu, hili lenyewe ni janga la kipekee.

  ReplyDelete
 9. Yaani nawaangalia Watanzania wenzangu walio hapo juu ya msikiti. Wanacheka wenyewe utafikiri hamna tatizo lolote lililo wapata. Kwanini Mungu asiwasaidie. Watanzania ni watu waliobarikiwa sana kuwa na mioyo ya furaha muda wote. Ndio maana pamoja na mazuri yote ya kwingine nasubiri tarehe ya kurudi nyumbani Tanzania na hata ingekuwa ni leo nsingeahirisha fright yangu. Mungu tunakuomba usitishe iyo mvua.Amen

  ReplyDelete
 10. that sucks I hope that your families are safe and you can find peace soon.

  ReplyDelete
 11. poleni sana ndugu zetu!mungu yupo nanyi.huyo mbunge wa mafia anastahili sifa sana na watu wote waliojitolea kusaidia.nb miundo mbinu 0 hzo barabara zinaonekana kabisa wamelipua. mitaro hakuna then barabara za juu muhimu. sio posho za wabunge

  ReplyDelete
 12. Mheshiwa Makinda uliyedai posho za wabunge kwa visingizio vya Mheshimiwa Shibuda sasa tumuombe Rais asaini ili posho hizo zisaidie waathirika wa mafuriko ambao hawana income, roof on their head, and daily bread. How about that?

  ReplyDelete
 13. Kwa umaskini uliokithikiri kiasi hichi, hivi kweli bado kuna mbunge anayefikiria posho?

  ReplyDelete
 14. Helcopters zilionekana nyingi sana kipindi cha mafuriko ya wanasiasa pale Igunga, vipi mafuriko ya walala hoi Dar zipo helcopters mbili tu za vyama vya siasa POLISI na JWTZ? Vyama vya CCM, Chadema, NCCR, CUF, na vingine utitiri helcopters zenu ziko wapi???????

  ReplyDelete
 15. Majengo mengi marefu na mafupi yanaongezeka kwa kasi Dar. Lakini sewage system bado ni ile ya mkoloni.Mvua iliyonyesha ni kubwa sana lakani maji yalitakiwa kufuata sewage system ili kuazaa kupungua na siyo kutegemea jua kukauka. Poleni ndugu zangu, Mungu awasaidie ili siku hizi za mihangaiko ziwe historia.

  ReplyDelete
 16. Isa nyumbani ni nyumbani,nilifikiri ungefurahi kurudi ili usaidie katika uokoaji?

  ReplyDelete
 17. Poleni kwa maafa!

  Maafa hayana jinsi pasitafutwe mchawi , ohh serikali,ohh chama!.

  Mfano wewe ndio Raisi au Mbunge ungeweza kuzuia majanga ya asili kama mafuriko na mvua kubwa ambazo hupangwa na Mungu yasitokee?

  Mungu atunusuru!

  ReplyDelete
 18. Poleni kwa maafa!

  Maafa hayana jinsi pasitafutwe mchawi , ohh serikali,ohh chama!.

  Mfano wewe ndio Raisi au Mbunge ungeweza kuzuia majanga ya asili kama mafuriko na mvua kubwa ambazo hupangwa na Mungu yasitokee?

  Mungu atunusuru!

  ReplyDelete
 19. Hahahaha Mdau wa 14 hapo juu Helikopta zipo 2 tu za Chama cha POLISI na JWTZ kwa sababu za vyama kama CCM ,CHADEMA, na CUF ninakutaarifu kwa dharura na kwa masikitiko makubwa kuwa zipo gereji huko nchini KENYA zinapokodiwa zinafanyiwa matengenezo!

  ReplyDelete
 20. Mbunge wa Mafia unastahili pongeze kwa jinsi ulivyojitolea. ni aibu sana kwa wabunge wote wa Dar Es Salaam sijui wako wapi kwa sasa, pengine nje ya dar kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka. nafikiri umefika wakati wa kuchagua viongozi wanaoongoza kwa mifano na kuachana na viongozi wanaoongoza kwa kushindana kuvaa suti nzuri na kuendesha magari mazuri bila kujali wananchi wao.

  ReplyDelete
 21. mungu wajalie wenzetu hata tukiwalaumu ni bureeeeee, haya tuje kwenye hizi barabara na madaraja jinsi gani serikali inavyochakachua kweli kama wangejenga kitu imara yangebomoka??? tujue jinsi gani hawa makandarasi wanalipuaaaaaaa tena serikali mjenge haraka sana hayo madaraja na barabara,kitu ambacho nimeshangaa sana barabara ya namanga eti wamemaliza kujenga ile ni barabara au rafu jaman nchi hii imeoza na inanuka viongozi bure kabisa,ilibidi niulize nikaambiwa ndio barabara ya namanga imesiha hivyooooooo

  ReplyDelete
 22. Boti zenyewe zimeozaaaaaaa tanzania tanzania nakupenda kwa moyo wote X2 upuuzi huu nchi hii haifai kwishnei,haya hizo posho saidieni watu sasa waone

  ReplyDelete
 23. Siasa zinajiri katika maoni yetu,,,kiasi cha maafa kinaonyesha wazi hadi maji yanafika ktk madirisha ya nyumba na kukaribia mapaa ya nyumba, lakini analaumiwa Raisi wa nchi Miundo mbinu hafifu na Serikali!!!.

  Jamani mfano Je, Raisi au Serikali anaweza sababisha kiasi hicho cha mvua kubwa na mafuriko?

  Jamani Je, Raisi au Serikali anaweza zuia kiasi hicho kwa hali inayoonekana cha hali ya majanga hayo isitokee?

  ReplyDelete
 24. Mungu Atubariki Watanzania. Mungu atusamehe makosa yetu, Mungu atuepushe na kikombe hiki. Tunaomba hayo yote tukiwa na unyenyekevu mkubwa. Amen

  ReplyDelete
 25. Kwa kweli inasikitisha sana kwa hali inavyoonekana na kwanamna ya pekee tunawashuku MICHUZI blg kwa hicho mlichokifantya.
  Ila swali linabaki kuwa, JUZIJUZI TU WAWAKILISHI WETU WALISEMA KUWA GHARAMA ZA MAISHA ZIMEPANDA NA HATA KUFIKIA MAAMUZI YA KUJIONGEZEA POSHO HIVI KWELI JAMANI, HATA HILO NA LENYEWE HAWAJALIONA? MAANA KUPITA KOOTE NI MBUNGE MMOJA TU ANAONEKANA. TUWE NA UBINAADAMU KWAKWELI.

  ReplyDelete
 26. Ndugu zangu Wa Tanzania poleni sana kwa janga kubwa la mafuriko. Mie mlala hoi nilicho nacho ni imani kwa Mola awalinde na awaokoe na hili janga. Lakini picha zote zilizo postiwa hakuna hata mwananchi mmoja anaeonekana kuwa na wasi wasi naona kila mtu yuko poa na hata wngine wakicheka/tabasamu sijui hii ndo culture yetu kuchukulia mambo kiurahisi?? hayo mabarabara ya lami yanamong'onyoka kama udongo jamani ni nini? Na ni nani anaeyatengeneza? Hivi na sisi tunaweza kujivunia kitu chochote cha quality? Ni aibu saana Waziri wa mambo ya ndani na time yake wafunge mkanda na kuboresha nchi yetu. mafuriko ni nje ya uwezo wetu lakini barabara, sewage na ujenzi wa nyumba ni mikononi mwetu wananchi. Narudia kusema pole sana Tanzania kwa janga hili

  ReplyDelete
 27. SERIKALI YETU IMETAWALIWA NA SIASA TU..HAIPO SENSITIVE KABISA KWENYE ISHU KAMA HIZI...

  ReplyDelete
 28. ndugu zetu poleni kwa maafa ila kumbukeni kua MUNGU is always there for us na haya yote ni mitihani ambayo inabidi tuishinde, tafadhali tuwe na subira katika kipindi hiki kigumu. MUNGU afanyike faraja yenu.

  ReplyDelete
 29. Dah pic zinatisha Tanzania.Mungu wabariki watanzania wenzangu.Hebu angalia nyumba za ndungu zangu hapo Jangwani ni duni, maskini eti twasheherekea miaka 50 ya uhuru.Sioni chochote hapo mambo niyaleyale kwa walala hoi.Wabunge wataka kuongezewa posho kweli huu ni unyonyaji walala hoi wanateseka.Nasikia hata kulia.
  UK

  ReplyDelete
 30. Kazi nzuri Michuzi kutuhabarisha sisi tulioko mbali. Keep up the good work!Mdau, Denmark.

  ReplyDelete
 31. TANZANIA TUWE NA SUBIRA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU NI KWELI MAKOSA YAMEFANYWA NA SRIKALI YETU AU WANANCHI LAKINI TUSILAUMIANE KWANZA TUMALIZE HILI TATIZO NDO TUANGALIE TUMEKOSEA WAPI

  ReplyDelete
 32. Jamani mbona serikali iko kimya, Kikwete where are you? Wapiga kura wako wanakufa na maji, tuma zile Helkopta tatu ulizokuwa unatumia kipindi kile cha kampen kuwanusuru wananchi wako, wake up

  ReplyDelete
 33. Neville MeenaDecember 22, 2011

  "Tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele". Ya kweli haya jamani katika hali hii? Ee Mungu tuwezeshe kuondokana na adha hizi.

  ReplyDelete
 34. TUPOE NA JANGA kwani inasikitisha sana kuona zoezi la uokoaji halina nguvu kwa serekali. Hii ni ishara kubwa tunajali sana matumbo yetu kulikoni kingine. Ila tufahamu kama wamekufa 13 na je wanyama idadi gani ipo??? hii ni estimation ya haraka haraka. Na kama wengine hawatopatikana wataishia wapi kuozeana ndani ya maji na maji hayo tukumbuke yanasafiri sehemu tofauti hata kuungana. Na maji haya yatakuwa contact na wananchina wanyama waliokufa. Chimbuko lakuenea kwa maradhi mbali mbali. Serekali kuanza kutumia pesa iliyokuwa na yo kama ipo kununulia madawa na nyenzo zingine....catastrophic!!! tunaomba iforecast mbali kwa janga hili.

  ReplyDelete
 35. R.I.P remmy aliimba kilio cha samaki machozi kuishia majini hizi kelele zetu hazifiki popote

  tuendelee kutoa kura kwa wajuaji kula sisi tulale na njaa
  habari ndio hiyo

  ReplyDelete
 36. Naona watu wengine wanasema tusilaumu serikali au vyama kitu tunacholalamikia serikali kutofatilia sheria ambazo wanazitunga wao kama kuwaachia watu kujenga kwenye mabonde ambayo mengine ni mikondo ya mito ambayo tunajua wazi kwamba pakitokea mafuriko watu watapoteza maisha, hatusemi kua serikali imeleta hizi mvua tunachouliza ni serikali imejitayarishaje kwenye matukio kama haya, kwanini wasiwatoe hao watu kwa nguvu kusudi kuokoa maisha yao especially ya watoto ambao hawana hatia, au mnatuambia kwamba mnawaonea huruma wataenda wapi kwa hiyo ni bora wapoteze maisha yao mimi nafikiria tumekua na uvivu wa kufikiria na nidhamu ambayo naona hatuna kabisa.

  ReplyDelete
 37. Ndugu zangu Nimezipokea taarifa hizi kwa masikitiko makubwa sana kwa ndugu zetu Tanzania kwa maafa yaliyowapata.Poleni sana ndugu zangu mliosalimika na wale ndugu walofariki katika maafa haya nawaombea M/Mungu awalaze mahali pema peponi.Wale wote waliowezesha zoezi zima la kuokoa ndugu zetu mwenyezi Mungu atakulipeni. Changamoto yangu naitoa kwa Serikali Wenzetu nchi zingine wanazo tume za uokoaji na kama hivyo ndivyo basi, Sisi tuna
  Jeshi ndio mara kwa mara wamekuwa wakitumika basi wapatiwe vifaa endapo dharura kama hii inatokea waweze kufanikisha zoezi kama hili
  vizuri tumeona vifaa vilivyotumika ni duni na vikuu kuu, kama posho zinaongezwa na watu wanapiga kelele wanaongezewa nasi tunasema kwamba boresheni na hili basi.Hili suala ni la kitaifa ni vyema watanzania kuonyesha uzalendo,upendo,kujali,kujitolea kuwasaidia ndugu zetu kwa kila hali."Kutoa ni moyo na sio utajiri" MUUMINI BORA NI YULE ANAYEMSAIDIA NDUGU YAKE. MOLA AJAALIE MVUA HIZI ZINAZOENDELEA KUNYESHA ZISILETE MADHARA ZAIDI,M/MUNGU ATUPE MOYO YA HURUMA NA UPENDO KUWASAIDIA NDUGU ZETU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU, AMIN.

  ReplyDelete
 38. YAANI NINYI WABUNGE WA ILALA, TEMEKE NA KINONDONI, MMENITIA AIBU SANA TU!!! YAANI MBUNGE WA MAFIA ANAKUJA KUTENGENEZA CV YAKE JUU YA VICHWA VYENU!!! HAMNA HATA AIBUUUU!!!?! MKO WAPI???? THANX SANA MBUNGE WA MAFIA, WELL DONE NA MUNGU AKUBARIKI SANA. MI NADHANI NYIE WABUNGE WAZALENDO UBAHILI UMEWAZIDI SANA,HUYU BWANA WA MAFIA YAMKINI KATOA HELA ZAKE MFUKONI,AU POSHO YA UBUNGE WAKE,NYIE ZENU MMEPELEKA WAPI??????????????????? WANANCHI WAKIJENGA KWENYE MITARO YA MAJI, MNAWAAMBIA HAPO NI POA,WEWE SI MTANZANIA BWANA? UNA HAKI ZOTE.. MAFURIKO YAKIJA ,AIBU!!!! MNAJIFICHA!! WAKOMBOENI SASA ATI!!??? SI MLIWAONA WAKIJENGA WAKATI MNATAFUTA KURA KWAO??? NYOOOO.!!!??. MKEREKETWA,COMRAD Kim.

  ReplyDelete
 39. Mbunge wa MAFIA,,,Tafadhali sana afikiriwe!!!.

  Tunataka safu ya viongozi wa ngazi za juu wenye moyo kama huu nadhani tutafika!

  Yeye amejitoa kama alivyofanya Raisi yule wa Chile wakati wachimbaji mgodi 33 walipokwama ardhini kwa siku 33 lakini wakakombolewa na kutoka salama nje ya ardhi!

  ReplyDelete
 40. Tunataka Viongozi wa aina hii ya Mhe. Mbunge wa Mafia ambao huzama ktk maji na hawaangalii ubora wa suti walizovaa ila kwa ajili ya Maslahi na maisha ya Wananchi!

  ReplyDelete
 41. mafia?huyo mbunge apewe sifa kwani hiyo ngalawa alipo simama ni hatari tupu.huyo aliyemkodisha akamatwe kwani anazidi kuongeza stress za watu.hongera mbunge.mwananchi mwenzio.

  ReplyDelete
 42. Ama kweli mtu mmoja alisema kuwa siasa ni mchezo mchafu na karibu wote wanaocheza mchezo huo wamejaa uchafu pia. Kwenye kampeni ya kutafuta kula helicopta zipo, kwenye maafa kunakohitajika hurma za vitendo ni Mbunge mmoja wa Mafia ndiye kajitokeza! Sio serikali, sio ccm, chadema, wala nani, uzalendo wa Tanzania alizikwa nao Nyerere na Sokoine,waliobaki ni tumbo na anasa tu.

  ReplyDelete
 43. serikali isaidie wananchi kwa kuwapa hifadhi,hali kama hii inasikitisha sana. Wakubwa kao ahh salama kabisa lakini walala hoi ni vilio tu.

  ReplyDelete
 44. Pole Sana. All the very best to all that are in hardship at the moment

  ReplyDelete
 45. Hayo ni mavuno ya dhambi zetu. NA BADO! Dawa ni kumrudia Muumba wetu.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...