Katibu wa NEC ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipongezwa na mama yake, Bi Kezia Alfred, baada ya kutunukiwa shahada ya pili ya uongozi katika mahafali ya kumi ya Chuo Kikuu Mzumbe, leo.
Nape Nnauye (kushoto) akijadili jambo na wahitimu wenzake wa Shahada ya pili ya uongozi katika mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu Mzumbe, leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Wengine kutoka  kushoto ni, Anedina Hongele, Zakia Omari, Magnus Mahenge na Meja Joseph Masanja.
Watangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Channel 10 Fredy Mwanjala, Salama Hamadi na Zainab Abdul, wakimpa zawadi ya hongera Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye ametunukiwa shahada ya pili ya uongozi leo kwenye mahafali ya kumi ya Chuo Kikuu Mzumbe, kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. 
Picha na John Bukuku wa Full Shangwe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Kamanda NAPE NNAUYE,
    Hongera sana kwa hatua mpya ya kujifunza mbinu za kutatua mafumbo ya TAALUMA na mikakati ya kufanya MAAMUZI.

    ELIMU ya kweli ya UONGOZI imejikita kwenye kuwasikiliza wananchi kwa makini, kuwaitikia na kuwashirikisha ktk Kutatua KERO zao.

    Kwa kuwa unaishi kwa Vitendo basi Allah'hamdulillah!!! Mapinduzi Daima.

    MAINA ANG'IELA OWINO
    UK.

    ReplyDelete
  2. HUYU NAPE KAFANANA SANA NA MAMA YAKE,INGAWA INAKUWA NI NGUMU KUELEWA KAMA NAPE ANA SURA YA KIKE AU MAMA YAKE ANASURA YA KIUME.

    ReplyDelete
  3. Wewe Nape hatufahamiani ila nakupongeza sana..pamoja na 'kuzurura' kote huko kwenye shughuli za CCM bado ulikuwa unatenga muda wa kujisomea..halafu nimependa sana hiyo ya kusomea kwenye vyuo vyetu hivi..naelewa una uwezo wa kusomea chuo chochote duniani.Safi sana kijana tunakutegemea 2015 au 2025!

    David V

    ReplyDelete
  4. duh huyo mama ana damu kali sana

    ReplyDelete
  5. Hongera JEMBE kwa kupata sahada ya pili ,sasa tumia elimu hiyo kubebea JEMBE na NYUNDO ktk chama na kukatua ardhi sawasawa !!!

    IMANI YETU IMEBAKI KWA VIONGOZI WACHACHE WANAOHESABIKA KAMA WEWE,,,UNATEGEMEWA SAANA BAADAE 2015 NA KUENDELEA!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  6. Ukirejea kumbukumbu ya marehemu Moses Nnauye iliyotolewa humu tarehe 5 Dec, kuna wadau walikuwa wanaulizia mbona jina la Nape halimo kwa watoto wa marehemu, nadhani jibu mmepata kwamba waliotoa tangazo ni familia ya mke wa marehemu ambae alisomeka kama Mwanaisha na mama wa Nape amesomeka leo kama Kezia Alfred

    ReplyDelete
  7. Asikwambie mtu mwanaume akifanana na mama yake anakua bomba, mzuri anavutia, angalau anakua kwenye muonekano wa mwanaume, lakini amebeba sura ya mama

    ReplyDelete
  8. Asikwambie mtu mwanaume akifanana na mama yake anakua bomba, mzuri anavutia, angalau anakua kwenye muonekano wa mwanaume, lakini amebeba sura ya mama

    ReplyDelete
  9. huo muda wa kusoma aliupata wapi wakati mara nyingi alikuwa nazunguka. Nina mashaka na hiyo shahada. Labda kama Mzumbe wanatoa shahada za heshima kwa level ya Master.

    ReplyDelete
  10. Wewe Anonymous wa 03:48:00 kwa nini unapenda kudharau wenzako? Muda wa kusoma huwa unapatikana pindi unapopanga mipango yako vizuri.

    Mbona wengine wanakwenda kunywa pombe halafu na kurudi kupiga kitabu?

    Hongera sana Nape, way to go!

    ReplyDelete
  11. MDOGO WANGU ULIYEULIZA NAPE ANAPATA WAPI MUDA, ELEWA KUWA HII NI KARNE YA 21. HATA KAMA UMELAZWA HOSPITALI YA MUHIMBILI UNAWEZA KULAMBA NONDO YA UNOVERSITY OF PHOENIX. HONGERA MTOTO NAPE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...