THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

house for rent @ Sinza, Dar es salaam

 A 5 unfurnished bedrooms house for rent at Sinza. It is a well fenced house with one master bedroom and four singles,water facility,luku,tiles,water tank,water pumps - You named t. It is on a good location just 40 meters from the main road. Serious tenants. Quick tenants are encouraged to apply. No Madalali(agents) or go-between Pse!
Price $ 500 Per month(1 year advance)a


Kuna Maoni 23 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  nyumba ipo sinza dolla ya nini si useme shilingi,mbona munazidi sasa tunaelekea wapi?wa tanzania

 2. Anonymous Anasema:

  Machangu doa wataivamia mara moja hiyo nyumba!!

 3. Anonymous Anasema:

  vipi mafuriko huko? tusije lkujukuta tunaelea kwenye maji???????

 4. Anonymous Anasema:

  Mnhh Sinza kwa malezi ya watoto pagumu kidogo, hebu tupe mkao wa kiujumla na taswira ya upatikanaji wa vituo vya malezi ya watoto na maisha ya jamii yanayozunguka eneo hilo la nyumba...kulingana na utitiri wa ma Baa maisha ya usiku na Klabu za usiku!

 5. Anonymous Anasema:

  $500 sinza! Kalaghabaho!

  Kama nina nia ya kupanga nyumba ya kiwango hicho ziko kibao Mikocheni, Ada Estate , Regency na hata Masaki. Sehemu ambapo sitabughudhiwa na mazingira ya kiswahili kwa watoto wangu (Baa nyumba ya pili, Mateja kukaa nje ya geti langu nk)

  Economic depression iliyokumba makampuni mengi yamefanya siku hizi hawalipii nyumba wakurugenzi wao, na mtu kutoa hela yake mfukoni ($6000) alipie kupanga si ni bora aanze kujenga moja kwa moja!

  Watanzania tuache kukurupuka na bei zisizo realistic!

 6. Anonymous Anasema:

  KWA NINI DOLA?

 7. Anonymous Anasema:

  dola 500 ni sh laki 8 kwa mwezi . , watanzania msiropokwe ropokwe , ati mimi siwezi kukaa sina ni uswahilini , hivi wewe ni mzungu mbona hujaishi london , kama tabia chafu ni sisi tutajirekebisha , mimi ninakaa sinza nikifunga geti langi hata sijuwi kama niko dar , kweli kuna mabaa nikaweka sound proof window , kwahiyo hijuwi hata kinachoendele huko mitaani , uswahili ukiutaka utaupata popote hata ukiwa london ,upo na umejaa sana kuliko huko manzese ,

  kharama za ujenzi hazina huruma anayejenga sinza manzese au osterbay ananunua cement kwa bei hiyo hiyo , huwezi kujeng nyumba sinza chini ya sh million 100 na huwezi kununua kiwanja sinza chini ya sh million 100 total thamani ya nyumba nzuri ni sh 200 milion , hebu nenda kakope benki sh 200million riba yake kwa mwaka tuu ni sh milion 20 , hii ni riba ya asilimia 10 , na sjuwii kama benki itaweza kumpatia mtu wa kawaida riba ya aslimia 10 sasa ukiambia kodi ya nyumba ni milion 10 kwa mwaka ki uchumi una kaa bure ,
  maisha ya tanzania ni ya kutumia ubongo na ndiyo maana inaitwa BONGO

 8. Anonymous Anasema:

  Mdau inawezekana anakusanya DOLA ana azma ya kwenda China kukusanya mzigo wa biashara!

 9. Anonymous Anasema:

  Mazingira ya nyumba ilipo na mazingira na uchumi wa Tanzania malipo hayo kwa mwezi ni mno, labda ningekushauri uifanye Guest House hapo utafikisha faida hiyo, kwa mtu binafsi afadhali akapange aneo jingine ambalo hadhi yake inaweza kulingana na kiwango hicho.

 10. Anonymous Anasema:

  Mbona mimi naona bei yake poa? vyumba vitano, master bedroom na gate..hpa ughaibuni nalipa chumba imoja kwa karibu mara mbili ya hapo..kwa mamnen mengine,
  kwanini wabing wengi wanakimbili akujenga kama faid yenyewe ndiyo hiyo..binafsi naona bora kupanga na msimlaumu huyu, hii ni nyumab safi na bei safi..ningekuwa nakuja likizo, sioni nikae hotelini, bora kwa kupanga

 11. Anonymous Anasema:

  Sinza na dola wapi na wapi?

 12. Anonymous Anasema:

  Hilo ni gate la kuingilia mbele au nyuma, maana kama ni mbele hata Bajaji haiapita, labda iende moja kwa moja sebureni!!! Halafu, eti Dola??? Dola ndio nini???? Sema Tshiling utaeleweka zaidi!

 13. Anonymous Anasema:

  Nyumba yenyewe haina hata parking. Halafu sinza ni uswazi sana. Kwa hiyo bei ni wizi mtupu. Nakushauri uishi wewe mwenyewe, siyo lazima upangishe.

 14. Anonymous Anasema:

  mimi nimemuelewa kwa nini anasema kupangisha kwa dola ni sahihi kabisa hela yetu ya madafu itatabia ya kushuka thamani kila kutwa, ndio maana amesema dola ili asipate hasara haya yakitokea.

  Dar es salaam mbona mabaa yako kila mahali na kila mahali kuna kelele, msipende kugomba kwa jazba sana fanya uchunguzi kwanza.

  kama unahitaji nyumba pia unaweza ukaongelea swala la parking na labda mwenyewe anaweza akawaza kupunguza bei.

 15. Anonymous Anasema:

  wewe unaijua dola?au unasikia hilo jina,hakuna mazingira ya dola hapo.

 16. Anonymous Anasema:

  acha pumb*v* jenga yako sh*nz type!!!

 17. Anonymous Anasema:

  Huu umaskini na ukosefu wa regulatory kwenye biashara ya nyumba unaumiza hivi kulipa $6,000 upfront kwa uchumi wa kitanzania katika eneo la sinza ambapo kuna kilele za bar, mziki, utulivu hafifu..n.k haviendani kabisa na thamani ya pesa hiyo (value for money).

  Mbona real estate industry imeendelea sana Kenya, yaani kwa bei hiyo unapata apartment iliyokatika hali nzuri sio nyumba kuu kuu hivi ambayo imepakwa tu rangi, ambayo mpangishaji anapanga tu bei yeyote bila kuzingatia thamani ya pesa. Wenye mihela jaribuni kufanya real estate business mtengeneze quality residential houses kama majirani zetu wakenya.

 18. Anonymous Anasema:

  naona watu wana jazba kuhusu bei ya nyumba, naona ni muhimu kuwaza kwa mapana zaidi badala ya kum attach mwenye nyumba. Mfano mfanyakazi wa kati serikani anayelipwa kwa shilling akihitaji hii nyumba itabidi akope maana hela ya mwezi haitoshi

  then kulipa kwa mwaka? Mpangaji atapata wapi Rushwa itaendelea kwa mtaji huu

  Serekali inahitaji kuweka misingi bora ili wote wapangaji na wenye nyumba wafaidike. Ni mawazo yangu tu. mpangaji Sinza

 19. Anonymous Anasema:

  Mdau wa
  Sat Jan 07, 01:51:00 PM 2012
  Ukienda kukopa benk ukakatwa hiyo hela 800,000 utakua umerudisha milioni 88, unaweza jenga nyumba nzuri ya m60

 20. Anonymous Anasema:

  Sijui kama Mtanzania na mfanyakazi wa kipato cha kati anayeweza kutoa Dola 6,000/ kwa mkupuo anaweza kupanga nyumba hiyo! Labda Wachina....na wafanyabiashara wakubwa! Ambao wengi kwa ajili ya hadhi wanaikimbia Sinza ambayo siku za miaka ya karibuni imekua ikishuka hadhi ghafla....lAKINI kama kwa wafanyabiashara wa Unga....wenye fedha za mkupuo....nyumba ndogo za vizito.....inaweza kupata mtu! BONGO HAKUNA LISILOWEZEKANA!

 21. Anonymous Anasema:

  jamani ni vichekesho sana kwa nyumba ya thamani hiyo siyo unaweza tumia hela nyingi kwenye kujenga lakini ni bure kabisa ukisema ulipie gharama zako unajisumbua tu weka fair bei watu watapanga

 22. Anonymous Anasema:

  Jamani ni lini tutathamini fedha yetu kila anayekodisha kwa dola kwa dola, hapa hatupo marekani ni vyea kusema unakodisha kwa bei mbya kuliko kwa dola kwa dola

 23. Anonymous Anasema:

  Si useme Tshs, hizo dola za nini kwani ikiwa Tshs haipangiki? Kwanza yaonekana ina mapungufu kibao, parking hapo majanga.