Kumewahi kuzuka malalamiko kadhaa ikiwemo na ushahidi wa picha katika suala zima la kufanyika kwa uhalifu na wizi wa mali za watu (kwa baadhi ya watu) ndani ya Mlimani City,La kustaajabisha wizi huo umehamia kwenye maduka yaliyomo ndani ya eneo hilo,safari hii angalia video hii iliyokuwa imerekodiwa na Camera ndogo zilizokuwemo kwenye duka hilo la vipodozi,na kuwanasa wezi hawa (akina mama hawa) na kuondoka na briefcase yote ya fedha za mauzo ya siku nzima,wezi hao ambao mpaka sasa hawajajulikana ni akina nani.! Kwa hivyo ni vyema wamiliki wa maduka ndani ya eneo hilo wakawa makini sana kwa watu mbalimbali,kwa anayeingia na kutoka .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. Mhh, poleni sana wenye mali. Ila natumai kuna uwezekano wa kuzoom hizo picha na kuwatambua japo kwa sura. Ikiwezekana, itakuwa hatua nzuri ya kuelekea kuwatia nguvuni. Wenye maduka wekeni kamera jamani, wadokozi wengi siku hizi mjini.

    ReplyDelete
  2. Huyo mhudumu alivyoreact kwa kupoint inawezekana ni inside job! Angereact haraka au kulia labda ingekua vinginevyo. Alijua kuna makamera kwajiyo kafanya usanii. Inawezekana lakini mimi sio sahihi. Polisi wafanye uchunguzi wao.

    ReplyDelete
  3. duh kwanza nakubali kabisa kama hao mabinti ni wataalamu wa kazi yao, yaani namna walivyoweza kumbabaisha muuza duka hadi wakafanikiwa kuiba ni mbinu yakinifu.

    Pili mwenye duka hili atapata masomo mawili, kwanza duka na aina ya bidhaa anazouza inahitaji kuwepo na wauza duka zaidi ya wawili, jengine ni kuwa pesa asiweke nje nje namna ile, pesa huhifadhiwa ndani ya meza.

    Tatu mleta taarifa unahakika walichobeba hao wezi kinaitwa briefcase? mimi si mtaalamu wa kiingilishi lakini naamini briefcase haiko vile.

    ReplyDelete
  4. Ee eee hii inatisha sana,,ina maana huyo mama aliyejifanya amevaa hijab,kavaa ili aonekane mstaarabu na mtu wa dini,,Hawa watu ndo wanautukanisha Uislam,,Yaani wana laana hawa watu,,,huyo shetan mwingine alijaribu na kujaribu kuvuta hiyo briefcase mara ya tatu ndo akafanikiwa,mimi nilifikiri hiyo ni labtop,,Ee hawa watu ni maprofessional,lakini huyu Dada muuzaji anaweza kummark sura huyo aliyekuwa anazunguka nae mwenye kujistir hijab ya kinafiki,na watakuwa wako na gari nje linawasubiri ili watokomee haraka kutoka eneo hilo,,,EE nimelaani hicho kitendo sana!Hawa watakuwa wameishawaliza watu wengi sana,,Watafutwe kwa udi na uvumba.
    Wakikamatwa watangazwe Bongo nzima,ili na walioibiwa mwanzo wawatambue...siamini Dar wizi umefikia hapo!!Utafikiri kweli ni Movie!
    Ahlam ,,,UK

    ReplyDelete
  5. Hiyo kali sana, na hizo CCTV wasiziweke sababu ya kunasa wizi wa wafanyakazi tu, ilipaswa kuwe na mtu maalum wa kuitazama muda wote. Niliwahi kufanya kazi hii katika ubalozi mmoja mkubwa tu hapa bongo japokuwa screen moja ilikuwa ikionyesha kwa muda kamera zaidi ya mbili.

    ReplyDelete
  6. Police watawapa tu, nahiyo camera ya cctv inonyesha vizuri kuliko za ulaya,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuliko za ulaya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

      Delete
  7. Wanatisha hao wadada,wako timu na inaonekana ndio kazi yao..maana walivyomchanganya dada wa dukani huku mwenzao anaiba inaonekana ni wazoefu..ila tu hawajui kama siku hizi CCTV zakumwaga..anayewajua atuambie ni wakina nani kwani ni wakuogopa kama ukoma

    ReplyDelete
  8. yaani hii clip kiukweli imenisisimua na kunisononesha sn, sijategemea wadada wazuri hivyo wanaweza kuwa wezi. Yaani hawana woga kabisa, wangekamatwa je? Hao inaelekea ndo mchezo wao, watarudi tu tena, kama sio duka hilo hilo basi duka lingine, wenye maduka wakishirikiana wakaoneshana hii clip, wakija next time watawagundua tu.

    Kuna sehemu pale mwanzo huyo dada mwenye ushungi wa bluu anamuonesha mwenzie kwa kidole kuwa aibe kile kibegi cha blue, daaah!!

    Poleni sana Shear Illusions, wekeni wahudumu zaidi, mmoja hatoshi.
    Ippy

    ReplyDelete
  9. Bwana michuzi nunayo technology ya kuweza kupata clear image ya hao wezi na kubandika kila sehemu wanted..sema bongo wa bahili..mtu akkibiwa anataka msaada wa bure

    ReplyDelete
  10. Haya makurumbembe yakikuta barabarani ukitoa lift tu umeliwa.....ni majambazi yaliyobobea.

    ReplyDelete
  11. Wenzao wakiweka kamera kama hivyo, huko ndani kuna mtu anaangalia kwenye monitor. Hawa wangekamatwa mlangoni tu kabla hawajatoka. Sasa wanaweka kamera na hawaifuatilii faida yake nini.

    Wengine wajifunze kutokana na uzembe huu. Tena wateja wenyewe hata si wengi ni rahisi kuwanasa. Kawaida mtu akiingia tu kuna mtu huko kwenye chumba cha pili anamfuatilia nyendo zake kupitia hiyo kamera, akiiba kitu unamuarifu mlinzi mlangoni, au unatoka mwenyewe kumkamata, hiyo ndiyo faida ya kuwa na kamera ya ulinzi. Vinginevyo kamera uliyoiweka itakuwa haida maana.

    ReplyDelete
  12. Duh! hii atarias sana. hata wanawake timing namna hiyo?!! Mama aliniambia: Mwanangu, angalia sana. Siku hizi hakuna cha mwanamke wala mwanamme. Wote wamechakachuliwa

    ReplyDelete
  13. Pole mwenyeduka; ila jamani hao wamama inaonekana walikuja kabisa wakiwa na nia ya kuiba HOPE WATATAMBULIWA NA KUKAMATWA SHAME ON THEM. Alafu jamani hizo ela zilivyokuwa zimewekwa was not sage enough I can't believe wafanyakazi wanatumia njia kama ile kuwekea ela. TOO RISKY.... too tempting kwa wajanja!!!!

    ReplyDelete
  14. jamani sidhani kama kuna sehemu ina wizi wa madukani kama kariakoo, hao wenzetu wa mlimani city watuulize sisi wa kariakoo tunafanyaje biashara.

    ReplyDelete
  15. Sijaona mtu pumbavu kama huyo mwenye duka. ameweza kuweka security cameras lakini amshindwa kui secure hilo sanduku la fedha. kweli waswahili wanasema akili ni mali.

    ReplyDelete
  16. Duuhh....hii kali kweli, yaani akina dada wazuri wezi hata aibu hawana.

    Hali hii inatisha sana, dunia ya sasa si ya kumwamini mtu....hao wasichana ukiwaona hivi huwezi kuamini kama niw wezi.
    Lakini naamini watapatikana tu, Polisi wakifanya kazi yao vizuri, lazima wawanase tu. Na wakifanikiwa kuwanasa, tunaomba watuonyeshe kwenye mitandao, ili iwe fundisho kwa wote!

    ReplyDelete
  17. tunaomba hizo picha zikuzwe kisha ziwekwe front page kwenye magazeti. haraka kabla damage haijawa kubwa kwa watu wengine. Asante Michuzi

    ReplyDelete
  18. hao wamama ndo zao wanaingia kwa group kubwa dukani kuwachanganya nyie mnadhani ni wateja kumbe ni vibaka, kuna siku walikwapua laki tano kwenye duka moja la nguo mitaa ya namanga wakadakwa ee Mungu walikula kichapo cha kufa mtu ilikuwa ni aibu manake walichaniwa hayo mahijabu yao, tena huyo aliyevaa nguo ya dhambarau naye alikuwepo kwenye hiyo dhoruba hata huyo mwenye mkorogo ndo masta, ila kama kuchapwa walichapwa nikadhani watakoma kumbe ndo kazi yao inawaweka mjini, tena walikuwa wanne naona wameongeza mashambulizi. jamani wadada wa dukani mkiona group ina wamama kama watano wawili wanatumia mkorogo baasi nyie wachoreni muone, wakiingia ndani wanajidai wako bize kweli, huyu kashika hiki huyu kile halafu wote wanakusemesha mmoja anakuwa bize kwenye droo ya hela huku anacheki movement za dada muuza duka, hapo ndo unapigwa changa la macho!

    ReplyDelete
  19. Hii inaonesha namna vazi la HIJAB linavyoweza kutumiwa na watu wabaya vile vile

    ReplyDelete
  20. Hilo duka hua nanunua sana vitu na juzi tu nilikuwepo pale. Yaani, yupo mhudumu huyo mmoja tu mdada na mlinzi kwa nje. Huyo dada akiwa anakuhudumia, akija mteja mwingine ndo anakuacha anamfuata huyo, wewe hakuangalii unachofanya.. Hata ikifikia muda wa kulipa mpaka umuombe aje apokee hela...

    ReplyDelete
  21. Ndiyo maana kuna cash registers machine. Huifungui mpaka uwe na code yake na huwezi kuinyofoa kwa kuwa imewekewa makomeo.Mchezo kwisha!

    ReplyDelete
  22. Big up sana wadada sababu hata bei za bidhaa zipo juu sana wanatuibia sana mfano mr.price nguo sio nguo eti alfu 50,000/= me naona poa tu coz hata viongozi wetu ni wezi tu wanasababisha hadi tunakosa huduma za afya sa hivi. Kila mtu kawa mwizi bongo maisha tight sana

    ReplyDelete
  23. Thanks for our police force now they know about cctv.Kufunga wala sio gharama kubwa.




    Samwel- Arusha 0786 035 311

    ReplyDelete
  24. wizi kama huo umeshamili sana huku ughaibuni

    watu wanaingia kwenye duka kundi zima na wanamuweka mhudumu wa hilo duka busy na wengine wanaanza kujaza mabegi

    kuweni makini sana na hizo style zenu za maduka kufanya kama maduka ya mtoni mtu kujichagulia mwenyewe

    wekeni camera na wahudumu wa kutosha

    kumbukeni enzi za maduka ya wahindi au warabu kulikuwa hakuna hizo style za kujichagulia ilikuwa naomba kile nione naomba hiki nione mwenye duka anakutolea mwenyewe

    hawakuwa wajinga walijuwa wazi kuwa kuna mbinu nyingi za wizi.

    ReplyDelete
  25. Huyo mama na huyo dada nilikutana nao shopperz 1st floor kwenye boutique moja tukawashtukia mimi na mwenzangu. Wanauliza vitu kwa fujo ili wamchanganye muuzaji. wanatembea watatu huyo mama na binti na kijana mwingine. Baadaye wakaingia shopperz wakashika shika vitu hatukujua waliishia wapi. lakini mimi na mwenzangu tuliwashtukia kabisa na begi lao hilo hilo kubwa. Kuna haja ya wenye maduka kuwa macho na hasa wanawake siku hizi wamekuwa na mtandao wao wa wizi.

    ReplyDelete
  26. kuwa na kamera haisaidii kuzuia wizi, wenzetu wanaoweka kamera hizi wanakuwa na mhudumu pembeni anayezifatilia kamera hizo, yaani hapo angekutana nao mlangoni na walivyochelewa kuondoka. Nashauri mkiweka kamera muweke na mfatiliaji kwa nyuma ila hivi hivi mtaibiwa sana. Pole kwa mhusika

    ReplyDelete
  27. kidogo kuna tatizo la uvivu fulani hv wawauzaji maduka hasa wakina dada, wepesi kuomba kazi ili wawe wadokozi, sy wawajibikaji, maana hapo inaonekana kabisa ni uzembe wa muuzaji, hakuwa makini angekuwa mhindi angekuwa very sharp, very smart!

    ReplyDelete
  28. ukiangalia vizuri hi video kwanza utaona mwenye hijabuu anamuonyesha mwenzie kwa kidole achukue briefcase ,halafu muhudumu anawaamuru warudi nyuma wasimfuate,then wanamzungusha tena kwa kujifanya wanaangalia vitu vingine na kujishika kiuno,huyu mwenye hijabu anaonekana vizuri sana sura yake kwa kujikoboa sasa akikamwata huyu nae atamtaja huyo aliyekuwa nae.nawashauri waweke angalau wafanyakazi 2 ndani mwingine awe tu anaajifanya nae kama mteja anachagua kumbe anamonitor wateja ,mtu mmoja hawezi angalia kila kitu hasa wateja wakiwa wengi dukani,na kwa kawaida mlinzi aliyeko mlangoni pia anatakiwa kila mteja anaetoka ndani ya duka anamuamuru anafungue pochi au mfuko aliobeba kuonyesha ndani ana nini,na kama anavitu kanunua duka lingine aonyeshe risiti, maduka mengi ulaya hufanya hivyo hata kama kuna camera,huo ndio ushauri

    ReplyDelete
  29. Not very convincing. Was this made specially for YouTube or something? Sielewi mantiki ya kuweka kamera nne za usalama dukani halafu mtu ushindwe kuwakamata wezi kama hawa. Halafu swali lingine dogo: kwanini sura ya huyo dada aliyekwapua kasha hilo inafichwa?

    ReplyDelete
  30. TENA APA NI SHEAR ILLUSSION YAANI YULE DADA NAKUSOMA KOTE ULAYA AMESHINDWA KUSECURE SEHEMU YAKE YAKUWEKA PESA SHAME ON YOU SHEAR

    ReplyDelete
  31. mimi mwanzo nilifikiri kile ni kiboksi cha kuwekea mapambo (jewels) kumbe ni cash box? ya aina gani hiyo? hao hawajaiba bali wamehamisha tu...

    ReplyDelete
  32. sasa wabongo ndiyo watambue kuwa hakuna kuoneana uruma, watu wana roho mbaya sana. ukiwapa lift hao lazima waondoke na kilichopo nyuma au hata power window. kuweni makini Tanzania sasa imebadilika sana. na watu wajitahidi kuwa makini, wenye maduka wekeni uangalizi wa kutosha. mimi kwangu nimeweka camera ukisubutu tu ujuwe umekamatwa na ujue ni mwisho wako hapa duniani.najua polisi watakuachia huko wala sikupeleki mie nitakuwinda nikikukamata nitakachokufanya najua mie, huko majumbani tuweke hivi kamera zitasaidia sana wadugu

    ReplyDelete
  33. Sura haijafichwa bali ni position ya kamera iliyokuwa inarekodi eneo hilo na isitoshe huyo mwizi hakugeuka upande ulio na kamera ndo maana sura yake haijaonekana.
    Pia msimlaumu muuzaji, yuko pekeake na wateja wanamuita awaoneshe bidhaa, angefanyaje? si ni lazima ainuke aende walipo. Kama mmeangalia vizuri, huyo mwizi ameiba akiwa jirani yake kabisaa, yaani kwa nyuma yake ila kwa vile binadamu hana macho ya nyuma ndo maana hakuona na isitoshe wakati yule mwizi anachukua, yule mwenye hijab alikuwa busy kumsemesha ili kumpoteza asijue kinachoendelea nyuma yake.
    Mwingine juu anasema muuzaji kala njama na wezi kwa kuwa hakushtuka wala kulia, kupiga kelele alipogundua kuwa briefcase haipo. Mimi nadhani ame-act sawasawa tu wala haoneshi kuwa na mahusiano na wezi kabisa. Angeshtuka na kuanza kulia ingemsaidia nini kwa wakati ule? alitumia akili kukimbilia mlangoni nje ili awawahi kabla hawajapotea but ikawa bahati mbaya kuwa wakawa washapotea.
    CHA MSINGI BOSI WAKE AONGEZE WAUZAJI NA PIA KUWE NA MTU ANAE-MONITOR HIYO CAMERA ILI KITU KAMA HICHO KIKITOKEA AONE MARAMOJA NA KUMKAMATA MHUSIKA.
    Ippie, Mbeya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...