Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Emmanuel Humba (kulia) akiongea na waandishi wa habari juu ya mfuko huo kutimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake tarehe 19 mwezi huu ambapo Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe zitakazofanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa utafiti na Takwimu Michael Mhando akifuatiwa na Beatus Chijumba ambaye ni Mkurugenzi rasilimali watu na utawala.
Mkurugenzi Mwezeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Eugen Mikongoti akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mfuko huo kutimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001 ambapo waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe zitakazofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Emmanuel Humba na kulia ni Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na uwekezaji Deusdedit Rutazah.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Emmanuel Humba (kushoto) akiongea jambo na Mkurugenzi Mwezeshaji wa Mfuko huo Eugen Mikongoti wakati wa mkutano kati yao na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Mfuko huo utatimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake tarehe 19 mwezi huu ambapo Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe zitakazofanyika makao makuu ya Bima ya Afya.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Emmanuel Humba wakati wa mkutano kati yao uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kuhusu mfuko huo kutimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001 ambapo waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo zitakazofanyika tarehe 19 mwezi huu.Picha na Anna Nkinda - Maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hawa watafuna pesa zetu tu....huduma ovyo...nenda zenu huko NHIF huduma zenu hazikidhi mahitaji hasa siku hizi

    ReplyDelete
  2. Hawa akina Mikongoti wamefanana balaa dah huyu ni Pius kila kitu. Hongereni sana ndio faida ya kusoma.

    Ntimizi Jr
    Indiana TL

    ReplyDelete
  3. Mfuko huu HAUFAI NA WALA HAUNA MANUFAA HATA KIDOGO;sababu ya kusema hivyo ni kwamba binafsi ninakatwa zaidi ya elfu 30 na mwajiri wangu anachangia kiwango hicho,jumla ni zaidi ya elfu 60 kwa mwezi. Juzi juzi nilipata tatizo huwa natibiwa Regency,nikaambiwa hicho kipimo hawana niende Aghakhan,kufika kule naambiwa kulipia cash elfu 50,nikashangaa sana nikaamua kufatilia ofisi za bima ya afya lakini niliambulia patupu kwa kujibiwa majibu ya ajabu na mmoja wa wahusika waratibu wa mfuko wa bima ya afya Makao makuu-kurasini. Iliniuma sana, nikapiga mahesabu tangu nianze kuchangia ni zaidi ya milioni mbili lakini kulipiwa elfu 50 inakuwa utata. Ina maana bima ya afya ni kwa ajili ya malaria na magonjwa ambayo naweza kujilipia!!!?? NARUDI KUSEMA, MFUKO HUU HAUFAI HATA KIDOGO. Ni mtazamo wangu binafsi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...