mdau mkubwa tu wa Globu ya Jamii wa pale A city zamani A town ama ukipenda jiji la Arusha, Novatus Makunga, amefumwa mahali akibariki kumeremeta kwake lakini mwenyewe amedai alikuwa hana leseni sasa ameipata na hakutaka kuongea mengi lakini picha ndo hizo zinajieleza anaeleza atakuwa tayari kueleza baada ya wiki kama tatu kwani ameandaa hafla kubwa ya yeye kupata leseni ila kwa mbali katika picha hizo ameonekana mzee richard mwangulube akisaini labda kama shahidi wa kutolewa kwa leseni hiyo kwa mdau,hongera
  mzee Richard Mwangulube akianguka kama shahidi wa baraka hii ya kumeremeta
Mdau na mai waifu wake wakifurahia tensdo hilo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Baraza na upendo ninyi!

    ReplyDelete
  2. Picha ya mwisho naona leboz..duh hili naona ni tatizo la kitaifa!! hahaa

    ReplyDelete
  3. Kumbe jamaa siku zote alikuwa hajaoa?

    ReplyDelete
  4. Eee bwana laziam uangalie utamu kwanza kwa miaka kadhaa halafu ndio uoe! Manake unaweza kuuziwa mbuzi kwenye gunia!

    ReplyDelete
  5. meseji ya pili ndugu yangu jadili mambo mazito si mambo madogo madogo nasi hata za toyota,lexus inatakiwa kuziondoa cha msingi tumpe ndugu yetu makunga pongezi kwa tendo hilo muhimu bila kujali muda kwani kuna watu mpaka miaka sitini wanaoa sembuse hiyo arobaini plus

    ReplyDelete
  6. Nikiripoti kwa Nipashe kutoka Arusha mimi ni.....hingera mkuu.Anabariki ndoa hafungi ndoa,tusome vizuri swali kabla ya kulijibu.

    David V

    ReplyDelete
  7. Suala la ndoa kwa maisha yetu ya sasa imekuwa kizungumkuti kwa vile wanawake wengi 'HAWAOLEKI' na ndoa inataka ujasiri kwa kuwa mara zote ni sawa na 'KUKALIA KUTI KAVU'

    1.Ni vigumu kuishi kwa kumwamini mtu kwa maisha ya sasa yaliyojaa vigeugeu kibao.

    2.Kwa hivyo tusimshangae Mdau kukaa muda wote huo mpaka sasa ni kuwa amekuwa ni mtambuzi na hivyo tumpongeze kwa kuwa sasa amefikia LENGO !

    HONGERA MDAU NOVATUS MAKUNGA!

    ReplyDelete
  8. Watoto wetu wa siku hizi anaonja kwanza halafu anabariki. Afadhali hata yeye, kuna wengine wanakaa tu na mwanamke, hata wazee mkipiga kelele, anasema (bila ya kukwambia kwamba mnamwingilia maisha yake. Watoto hawajui baraka au radhi za wazee ni muhimu sana katika maisha. Mradi tu wanaenda kama magombe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...