HABARI MDAU HASA MWANAMKE,
NALETA TAHADHALI KWA WANAWAKE WAENDESHAO MAGARI,MIMI ILINITOKEA NILIENDA SHELI MAENEO YA VICTORIA NIKITOKEA MAKUMBUSHO MAJIRA YA JIONI,NIKAONA MADAM NAELEKEA MBALI NIKAJAZE UPEPO, NIKAENDA KWANZA PALE OILCOM NIKAFIKA PALE NIKAMWONYESHA YULE KAKA TAIRI MOJA LA MBELE NA SIKUSHUKA, MATOKEO YAKE KUJAZA UPEPO ALITUMIA MUDA MWINGI NIKAMUULIZA KULIKONI MUDA WOTE AKADAI OOH PAMPU MBOVU NIKAMWAMBIA BASI NAENDA PENGINE AKADAI OOH HUTAFIKA NIKAMUULIZA KWANINI?AKANIJIBU HAKUNA UPEPO NIKAMWELEZA MBONA UPEPO ULIKUWEPO IKANIBIDI NISHUKE KUSEMA UKWELI NINA KAWAIDA KABLA SIJAONDOKA LAZIMA NICHEKI MATAILI NA NILICHEKI KABLA SIJAWASHA GARI!NILIKUTA KAUTOA WOTE NA AKISISITIZA UTAFIKA POPOTE!NILIMJIBU UMEUTOA UPEPO NA SIJATOKA MBALI KWASABABU NILIKUWA NAWAHI NIKALIONDOSHA KWENDA SHELI YA VICTORIA ,FUNDI WA PALE AKASEMA DADA MBONA WAMETOA VALI KATIKA TAILI YAKO?KWELI NILISONONEKA SANA KUONA WATANZANIA TUMEKUWA WANYAMA KIASI HICHO!WALINIJAZIA NA KUNIWEKEA TENA VALI NA WALINIDAI 4,000/= NIKAWALIPA WALE WAKAKA WALIOKUWA WAMEVAA NGUO ZA BLUE!

NILIRUDI KUMUULIZA NA NILIPOFIKA AJABU NILIKUTA HIYO PUMP WALIOSEMA MBOVU WAKAWA WANAJAZA PRADO ALIKUWA ANAENDESHA MKAKA!NIKAMWELEZA NJAA ITAKUUA AKAJIFANYA KUWA MKALI NA AKAWA ANATETEWA NA WENZAKE KWASABABU NILIKUWA MWENYEWE NA MWENYEZI MUNGU HAJANIPA KIPAJI CHA KUONGEA NILIONDOKA LAKINI NIMEONA BORA NIWASAIDIE WANAWAKE WENZANGU WAJUE!
KWELI NASIKITIKIKA SANA TENA SANA!NA SIJUI WALIKUWA NA MAANA GANI KWANI HATA NAKUMBUKA SANA ALINISIMAMISHA NA KUSISITIZA HUFIKI MBALI!NA ALIKUWA AKIWASILIANA NA WENZAKE
WAMESABABISHA RING YA GARI YANGU IMEPINDA INABIDI NITAFUTE PESA YA KUNUNUA UPYA.
NIMETOA ANGALIZO HILI ILI KINA MAMA MUONDESHAO MAGARI MUWE MAKINI UKITAKA KUWEKEWA UPEPO NAOMBA MUWE MNASHUKA!MSIKAE KAMA MIMI NILIKAA MANA SIKUANGALIA KINACHOENDELEA NA MUWE MAKINI NA HIYO SHELI!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. Watanzania hatuna kawaida ya kusaidiana pale ambapo tunaona mmoja wetu anaonewa hata katika suala la kuibiwa barabarani!

    ReplyDelete
  2. Dada pole sana kwa kutolewa upepo. Shukuru Mungu sana. Siku nyingine ukiwa unajaza upepo hakikisha unashuka na HANDBAG yako maana hapo walikuwa wanakupoteza maboya baada ya kuona hushuki.

    ReplyDelete
  3. DADA KWANZA POLE SANA NA ASANTE SANA. TANZANIA SIJUI TUNAELEKEA WAPI. HAYA YANAWAKUTA WENGI BALI WACHACHE WANATOA TAARIFA. NAOMBA VYOMBO VYA USALAMA VIFANYIE UCHUNGUZI WA KITUO HICHO KWANI MWAKA JANA NILIWA KULIPIA LITA 10 ZA DIESEL HAPO HAPO NA SIKUFIKA KWA NYERERE GARI IKAWA IMEZIMIKA. NILIFIKIRI NI MASWALA MENGINE BALI NILITAMINI KUDONDOKA WAKATI FUNDI ALIPONIAMBIA HAKUNA MAFITA. NILIPORUDI WALIKUWA MBOGO. MIND YOU MIMI NI MWANAUME NA MBISHI. ILA NILIJISIKIA SINA MSAADA WOWOTE.
    TUNAOMBA MASHUSHU AMBAO TENA WAKO HAPO KARIBU WAFAMYIE KAZI. TUNAJUA KAMA NI PETROL HAWAWEZI KWA KUWA KITUO NI HA MABOSI WAO, LAKINI UPEPO WATAWEZA. NCHI INAPOROMOKA. MDAU

    ReplyDelete
  4. Asante mdau, tunashukuru kwa kututahadharisha sisi wanawake. Ningependa kushauri hata wakati wa kuwekewa mafuta tuwe makini ili tusiwekewe upepo.

    ReplyDelete
  5. tukipata watu kama wewe kadhaa, wenye kutoa ushetani wa baadhi ya sehemu chafu na kuzitaja kwa majina itakuwa vizuri ili biashara yao idode washenzi wakubwa hao...lakini hujatutajia jina la hio sheli au gereji walikotoa vali kama sikosei..lakini kibaya zaidi pamoja na dhamira yako njema lakini wewe pia una kasoro zako tena ni mbaya zaidi pengine kuliko hao waliokutolea vali maana umeonyesha ubaguzi wa dhahiri kwa kutoa ushauri kwa wanawake tu na si madereva kwa ujumla na hili ndilo linanifanya nisikuonee huruma kwa yaliyokufika..mwizi ni mwizi tu haangalii mwanamke au mwanaume bali huangalia yupi mzembe/anaeweza kumkwapua...ungetoa angalizo kwa madereva na si wanawake madereva.

    ni hayo tu
    ahsnte

    hsm

    ReplyDelete
  6. DADA YANGU!MWENYEZI MUNGU AKUJA'ALIE KWA HILO,UNAJUWA SIO RAHISI MTU JAMBO KAMA HILO KUMKUTA KISHA AKAWAPA ANGALIZO WENZIWE..LAKINI NINAKUOMBA KATOE HIYO TAARIFA KATIKA MAGAZETI NA VYOMBO VYA HABARI NA UTAJE HIYO SEHEMU ILI WATU WAIKWEPE KAMA UKOMA,,,HAO WATU WANA LAANA MAANA,MTU WANAKUTIA HASARA MARA KUMI NA FAIDA YAO JUU,,WOTE WALE WALIKUWA NI WEZI MAANA KAMA ULIVYOSEMA WALIKUWA WANAWASILIANA NA WENZIE...UTANGAZE KAMA KUNA BOSS MWENYE HIYO PETROL STATION AWAFUKUZE WOTE NI WEZI HAO,NAJUWA OILCOM WATAWAFUKUZILIA MBALI,INA MAANA WAMEISHA WALIZA WATU WENGI SANA,NA KAMA KUNA NA WENGINE WANAFANYA HIVYO WATAKOMA HIYO TABIA,,
    JAMANI NI KWELI HIYO NI NJAA IMEWAFIKISHA PABAYA WANAWEZA KUSABABISHA AJALI BARABARANI,,MTU UNATOKA NYUMBANI GARI NZIMA KISHA INAKULETEA MATATIZO NJIANI
    KUMBE NI HAO LAANA QUMM!
    NI BORA UWATAARIFU WATU KATIKA VYOMBO VYA HABARI,,MAGAZETI NA UWAMBIE WATU WA TV WAWATAHADHALISHE WATU WOTE,NA SANA SANA WANAWAKE NDO WANAONEWA SANA MASIKINI,,EE!IMENIUMA HII KITU!

    AHLAM...LONDON

    ReplyDelete
  7. Pole sana, ila tunashukuru sana kwa mchango wako. Ni vizuri sana hata ukiwa unaweka mafuta ushuke pia.

    ReplyDelete
  8. Wajinga na wapuuzi wachache hawakosekani. Nategemea mwenye hiyo biashara hapo ajitokeze na kuomba msamaha kwa huyu dada, pia atoe ahadi kwamba atawasimamia vizuri wajinga wake.

    ReplyDelete
  9. Ashante sana my dear kwa hii news kweli watu wamekuwa matapeli sana

    ReplyDelete
  10. acha taibia ya kujifanya bosi
    mamdogo,huku ulaya service ndogo
    kama ya upepo unafanya dereva mwenyewe.
    siku nyingine shuka na uangalie nini kinachoendela.Sio wewe unachuna tu ndani kwenye kiyoyozi alafu ukiondoka unataka hata mia 5 upunguziwe.
    Mwenzio anasomesha watoto kama wewe,Kwani Bongo nani anayeishi kwa mshahara ?? Hivyo ukitoa upenyo utapigwa kama wewe unavyowapiga kazini ukipata mwanya , sema kwa style nyingine tu.
    cha msingi hata kama unanunua Gazeti lazima uwe makini lasivyo utakuta kurasa flani hakuna,kumbe mtu anajikusanyie kurasa zake masikini ,akiuza magazeti manne anapata jingine moja , watoto nao nyumbani,wanapishana chooni. ajira zenyewe taabu hapa mjini.

    ReplyDelete
  11. Tafadhaliandika kiswahili kinachoeleweka. Au andika kizungu kama kiswahili hujui. Sasa vali ndio nini?

    ReplyDelete
  12. Dada yangu pole kwa mambo yalikukuta...Asante kwa uthubutu wa kuwaambia wengine kuwa na taadhari na hiyo 'Petrol Station' na mafundi wa aina hiyo. Siku nyingine nakushauri ukitaka kuandika ujumbe kama huu panga mawazo yako kabla haujaanza kuandika na ufahamu nini unataka kusema!!Nimekuelewa lakini imenichukua muda. Pili zingatia matumizi ya 'comma' na 'full stop' ili kumpa unafuu msomaji wako na kumfanya aelewe kwa haraka ujumbe unaotaka kumpa. Asante!!!

    ReplyDelete
  13. makubwa!!

    huyu dada ana moyo! tunashukuru mwaya. ila umeeleza uzembe wako vzr!! hii tabia ya ubosi bosi hii inavyoonekana unahela sana au hiyo gari umenunuliwa huna uchungu nalo. ila mamii hata kama umelipata buree, thamini juhudi za mtu kwa kuwa mwangalifu na makini siku zote. haiwezekani jamani mdada upambane upate gari kwa hela yako afu ufike kwenye service ulale kwenye gari/unasikiliza kitchen pt yako leo.....never. take care!!

    ReplyDelete
  14. dada pole na asante kwa ujumbe.ila jifunze hiyo si shell ni petrol station au kituo cha mafuta kwa kiswahili..shell ni kampunikama zilivo BP orix na hata hiyo oilcom dada... na si peke yako wengi tu wanakosea..nije kwenye point yako sasa..uzembe pia unachangia..kwanini usishuke kwenye gari jamani? anyway ni fundisho pia kwa wengi..pole tena

    ReplyDelete
  15. dada pole na asante kwa ujumbe.ila jifunze hiyo si shell ni petrol station au kituo cha mafuta kwa kiswahili..shell ni kampunikama zilivo BP orix na hata hiyo oilcom dada... na si peke yako wengi tu wanakosea..nije kwenye point yako sasa..uzembe pia unachangia..kwanini usishuke kwenye gari jamani? anyway ni fundisho pia kwa wengi..pole tena

    ReplyDelete
  16. Jee, unamaanisha Oilcom kijitonyama? Au ile petrostation ya victoria kwenye duka la nguo na vivyozi? Maelezo yako ni muhimu tuyafanyie kazi.

    ReplyDelete
  17. couch potatoes wengi dar....., wao wanafanya kazi kwa remote control,....hapa ni Africa, siku nyingine na kokote kule uwe unashuka na kusimamia shughuli hiyo, kuhakikisha anajaza kiwango cha upepo kinachotakiwa na anaifanya hiyo kazi vizuri. Je bila kushuka ungejuaje kama kajaza hilo tairi au la?

    ReplyDelete
  18. Nyinyi munaopenda kulaumu bila ya sababu, kwani huyo anaeweka upepo si analipwa? Sasa kwa nini mumlazimishe kutoka kwenye gari ili kushadidia wizi wa hao vijana?

    Mimi naendesha kwa zaidi ya miaka 20 lakini nilikuwa sitoki kwenye gari wakati wa kujaza upepo. Ila kutokana na funzo la huyu binti ndiyo sasa nitafanya hivyo.

    Asante sana na wala usivunjike moyo kuna binadamu kazi yao kulaumu tu hawana wema.

    Na yule aliyeandika vali maana yake nini, vali ni kiswahili cha neno valve. Amelitumia sawasawa.

    ReplyDelete
  19. HATA MIMI WALINIFANYIA VISA SANA HAO WAKAKA, WALINIJAZIA UPEPO LAKINI BAADA YA KUMALIZIZA WAKANIAMBIA NISHUKE ILI NIRUDISHE MWENYEWE COVER YA SPARE TYRE WALIOIVUA ILI WAJAZE UPEPO! KWA KWELI SINA HAMU NA HIYO SEHEMU KABISA!!!!

    ReplyDelete
  20. oil com ni kawaida yao kuweka vijana wahuni kuna nyingine mandela road kabla hujafika tazara washawah kuniwekea upepo kwa sh 20000 badala ya mafuta nikarudi walikuwa mbogo kuteteana iliniuma. but naona oil com ni wezi tu sababu malalanmiko ni mengi

    ReplyDelete
  21. wabongo bana ujumbe umefika mnajifanya kukosoa oh nukta oh mkato mbona we umechanganya lugha mbili tumia moja basi kama wajua sana

    ReplyDelete
  22. Asante kwa kutujuza ila hayo matatizo yanawakuta wanawake/wanaume wazembe coz mtu kama mimi ninapokwenda popote ninapohitaji kupatiwa service ya gari yangu even garage huwa nakuwa sambamba na mafundi, simpi hata nafasi ya kunifanyia chochote hata kwenye vituo vya kujazia mafuta.

    Mama Abdul - Morogoro

    ReplyDelete
  23. Pole Shangazi kwa kutolewa 'Stimu' na Vibarua wa Sheli !

    Tatizo watu wana njaa na hawachagui ni njia gani ya busara ili kupata kula wanakuja wanakuonea bure Bibie.

    ReplyDelete
  24. we nawe ulaya yako haitusaidii ukoje huna akili ,mwenzio anatupa tahadhari wewe unatuletea mambo ya ulaya kubeba mabox,usifananishe bongo na ulaya

    ReplyDelete
  25. wewe hapo juu ulitaka atumie lugha ipi?mbona huyo mdau ameeleweka vizuri na ujumbe umefika iwe vali,vila,veli

    ReplyDelete
  26. Dada usiwe na wasi hilo swala litasawazishwa nitaongea na mwenye petrostation Ambae nirafiki yangu lakini kama ungeweza kuweka namba ili uje utuonyeshe alofanya hivyo afukuzwe mara moja!

    ReplyDelete
  27. mijitu mengine bwana, badala ya kushukuru mmepewa taarifa mnaanza kukosoa ushuzi. ngojeni yawakute then ndiyo utajua ubosi au director (MSONYO)

    ReplyDelete
  28. Wewe anonymous wa Thu Apr 19, 10:06:00 AM 2012 acha upumbavu.Huyu Dada anaongea mambo ya maana.Unaonekana ni mtu wa ovyo ndio maana unatetea uovu.Halafu unalinganisha vitu vya Ulaya na Bongo

    ReplyDelete
  29. Hiyo tabia iko kila mahali duniani. Hiyo sio kwa gereji tu bali hata madaktari, maprofesa, na watoa huduma wengine. Daktari unayemlipa atakutaji maradhi mengi ambayo hata huumwi ili umlipe pesa nyingi. Unafiki na kuliyana pesa ndio dunia ya sasa.

    ReplyDelete
  30. dada hao walikua AMATURE- wangekua PRO na taili la spea lingepotea...may be hadi site mirror.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...