Wakala wa Vipimo (WMA) kwa sasa iameanzisha huduma ya ukaguzi na uhakiki wa mitungi ya gesi ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata thamani ya fedha zao.
Ni ukweli usiopingika kuwa, hivi sasa wananchi wengi hutumia nishati ya gesi kwa ajili ya matumizi ya kupikia. Hii inatokana na kuwa, nishati za umeme, mafuta ya taa na mkaa kuwa ghali sana na kwa wakati mwingine, kutopatikana kwa urahisi.
Mambo muhimu ya kuzingatia:
Mwananchi anapokwenda kununua gesi kama ana wasiwasi kuhusu uzito wa mtungi wa gesi, ni vema akahakiki kwa kuupima kwa kutumia mzani ambao upo katika sehemu hiyo ya biashara.
Tunasisitiza kuwa kila sehemu inayouza gesi ya kupikia, kuhakikisha kuwa inao mzani ambao umehakikiwa na Wakala wa Vipimo kwa mwaka husika.
Hivyo, unapotaka kununua gesi ya kupikia, hakikisha unahakiki uzito wa mtungi wake kwa kutumia mzani ulio sahihi.
Endapo sehemu hiyo haina mizani, toa taarifa kwa ofisi yoyote ya vipimo iliypo karibu nawe.
Tunasisitiza kuwa, usinunue gesi bila kuhakiki uzito wake kwanza.
Afisa Vipimo akichukua maelezo
muhimu mara baada ya kuhakiki uzito wa mtungi wa gesi.
Uhakiki uzito
wa mitungi kwa kutumia mizani iliyo sahihi
Afisa Vipimo akihakiki uzito
wa mitungi kwa kutumia mizani iliyo sahihi
Mitungi ya Gesi ikiwa kwenye
chumba maalum kabla ya kukaguliwa na Wakaguzi
kutoka Wakala wa Vipimo.
who is paying for this kama sio mlaji??
ReplyDeleteToka lini gesi inaliwa.
ReplyDelete"MLAJI" ni neno linalotumika kama tafsiri ya "CONSUMER", ikimaanisha kuwa ni "MTUMIAJI" wa mwisho wa bidhaa, bila kujali kama bidhaa hiyo inaliwa au ni kwa matumizi mengine katika jamii.
ReplyDeleteAsante sana Yesu for this.....hii kitu inanichanganya sana.....mara gesi utumie mwezi....then next mtungi hardly a week!
ReplyDeleteWakala wa vipimo wangeweka matangazo yao katika kila wakala wa Gesi na kuweka namba zao za simu zao ili iwe rahisi kwa mlaji kufikisha malalamiko kiurahisi kwao iwapo atahitaji kufanya hivyo.
ReplyDeletehiyo mitungi tumeiyona lakini hivyo vichwa vyamitungi nibomu ukinunua gesi ukigunga gesi inatoka ilembaya nishanunua vichwa vitatu ukiwafahamisha wauzaji wanasema siyo kaziyao kaziyao nikuuza hebu fuatilieni jamani hili watu wengi wanalalamikia tatizo hili angalieni na hivyo vichwa
ReplyDeleteHivi hawa mbona kama wanapima uzito tu! - kwa nini wasipime kama ni salama yaana kama kuvuja kwa gas au kama inaweza kulipuka?!
ReplyDeleteThanks God for this kwa kweli jamani wauza Gas wamezidi kutubambika yani mitungi haijai kabisa!!! kama mdau hapo juu kasema kweli unatumia week 2 inakwisha. Pia tusaidieni kukagua exp date ya kwenye mitungi nilikuwa sijui kama hua inaexpire. Tafadhali wananchi chunguzeni mitungi yenu wakati munanua gas ndo chanzo cha kulipuka majumbani.
ReplyDelete