TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Gazeti la kila wiki la Dira ya Mtanzania toleo la leo, Jumatatu, Mei 7, mwaka huu, 2012,  limechapisha habari yenye kichwa cha habari, “Familia ya JK yachafuliwa”.

Katika habari hiyo, Gazeti hili linadai kuwa familia ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete inafanya biashara na kampuni ya Home Shopping Centre (HSC) ya Dar es Salaam.

Aidha, Gazeti hili linadai kuwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Bwana Said Saad ndiye msimamizi wa biashara za familia hiyo ya Mheshimiwa Rais.

Tunapenda kuujulisha umma habari hizo si za kweli. Ni uongo unaolenga kuupotosha umma na kuchafua jina la Mheshimiwa Rais Kikwete na familia yake. Na, au vinginevyo unalenga kuchafua jina la Kampuni ya Home Shopping Centre. Kama nia ni kufanya hivyo tafadhali msilitumie jina la familia ya Rais.

Mheshimiwa Rais Kikwete haendeshi, hajawahi kuendesha, na wala hana mpango wa kuendesha biashara iwe ni yeye binafsi au na familia yake. Shughuli azipendazo na ambazo anajishughulisha nazo ni kilimo na ufugaji. Kwa ajili hiyo ana mashamba Sanzale, Kiwanga na Msoga. Hata shughuli hizo hazijafikia kiwango cha kibiashara kwani hutumia pesa yake ya mfukoni kugharamia shughuli hizo.

Badala ya kutoa tuhuma za jumla jumla zisizokuwa na ushahidi wowote ni vema muwe wawazi. Ni vema gazeti likaeleza namna gani au likamtaja ni nani ndani ya familia ya Mhe. Rais Kikwete anaendesha biashara kwa kushirikiana na Kampuni ya Home Shopping Centre.

Kwa kufanya hivyo , Gazeti la Dira ya Mtanzania litawathibitishia Watanzania kuhusu ukweli wa habari hizo. Aidha, litaondoa doa baya na chafu linalotaka kuelekezwa kwa Rais na Familia yake. Kitendo hicho hakimtendei haki Rais na Familia yake.

Ni imani yetu kuwa Gazeti hili litatoa majibu ya masuala haya muhimu katika toleo lake lijalo, vinginevyo Familia ya Mheshimiwa Rais itakuwa na haki ya kuchukua hatua stahiki za kisheria.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
7 Mei, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2012

    Kama habari hizi ni za uongo kwanini wenye chombo hicho cha habari wasifikishwe kwenye vyombo vya sheria kujibu shtaka hili! Wanaosema uongo waburuzwe mahakamani ili kuleta heshima katika kutoa habari zisizoposha umma!

    ReplyDelete
  2. What happened to them good old days?, ingekuwa kwanza gazeti linafungiwa, muhariri anarundikwa, halafu maswali, in the same exact order.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 07, 2012

    wacha tuwachezee maraisi wetu wema na wapole, Allah forbid watanzania siku wakipata raisi dictetor watajuta, maana sasa kila mtu kamgeuza raisi kama tambala la viatu, ukiingia kwenye mitandao ndo usiseme, na hasa hawa wana chadema am sorry lakini chama hiki kimenitumbukia nyongo hasa naona kama kimejaa ulafi tu na ukanda na udini na wafuasi wake matusi matusi si wastaarabu, (sio wiote)africa ina maraisi wangapi kama kikwete? Allah atamlinda inshaallah

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousMay 08, 2012

      Wewe! Wacha ujinga! Kuna vile unaweza kuwa bora zaidi ya hivyo. Huwezi kuuzuia ukweli kutokusemwa, Kama kuzuia upepo, jua, mvua nk. Kwakifupi hatupo kwenye kanisani ama msikitini Bali tunatetea nchi yetu.
      Ooh nimetumbukiwa nyongo! Hahaa utaipenda na kuisoma number
      Mdini we!
      Na hapo utasema umetukanwa?

      Turudi kwenye mada sasa, yeye mwenyewe amejifanyisha tambara la Deki. Sio makosa yetu kumpa yeye meno Makubwa Na magumu kung'atia! Ni uswahili wake umemponza, Leo hii tumefikia kubaguana kwa dini zetu? Kupendana kwa dini zetu?
      Alafu Allah awepo mahali hapo.
      Na yeye Ni mdeeeen!
      I am sorry, Kama vipi jifanye hujaiona.

      Delete
  4. Hayo ndio magazeti ya Tanzania na ndio maana nina heshimu mtandao huu wa ankal ambao hauchapishi magazeti ya kizushi. Magazeti mengi yamekuwa yaupotoshaji, ya uchochezi na kujenga chuki.............kwani hata hivyo rais au familia yake ikifanya biashara ambayo ni halali kuna ubaya gani? kwa hiyo familia ya rais hawataki kujiendeleza kimaisha au tusema familia nzima inatunzwa na serekali, sasa kama baba yako au ndugu yako akiwa rais basi wewe tena ujibweteke kula ikulu kulala ikulu, anayelipwa mshahara na alieajiriwa ni Jakaya, sasa na wengine wakale wapi? Na wakienda kula ikulu hayo hayo magazeti, itakuwa kawajaza ndugu zake ikulu, wanakula bure wanalala bure hela ya walipa kodi..............eeh walimwengu nyie muogopeni Mungu jamani.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 08, 2012

    Tusikurupuke kutetea vitu ambavyo, wewe na mimi hatuna ushahidi. Gezeti liliandika hiyo habari, ila Ikulu imekanusha. Ni vyema tusubiri kujua ukweli wa mambo. Ni wakati Watanzania tukaamka. Na mtoa maoni hapo juu, CHADEMA inahusika vipi na hii habari? Watanzania tusiwe wanafiki..
    Ni mtazamo wangu tu..

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 08, 2012

    tusijiingize katika migogoro isiyokuwa na ushahidi. Chadema inahusikaje katika hili! Nisipotoshe umma na kuingiza vyama katika habari tusizozijua. Kuweni wastaarabu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 08, 2012

    tusijiingize katika migogoro isiyokuwa na ushahidi. Chadema inahusikaje katika hili! Nisipotoshe umma na kuingiza vyama katika habari tusizozijua. Kuweni wastaarabu.

    ReplyDelete
  8. Ni vyema hili gazeti likawajibishwa. Watanzania walio wengi wanaamini raisi au kionogozi alie bora lazima awe masikini kumbe ni upuuzi mtupu, hata kama HSC yote ingekua ya kwake ubaya uko wapi kama anafanya biashara kihalali, wabongo acheni fikra za zamani na za kipuuzi eti raisi au kiongozi hatakiwa kuwa na biashara na lazima awe masikini.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 08, 2012

    Acheni upumbafu nyie kila nchi huru ina ma-tabloid chungu mzima. Yanaandilka yanayosemwa mitaaani na watu wa kawaida. Sijaona Raisi wa nchi yoyote anashitaki matabloid. Angalia yalivyokuwa yanaandika kuhusu ufalme wa Uingereza etc etc

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 08, 2012

    wewe anonym wa mwanzo kifuu kweli unauliza kuhusu kushitakiwa gazeti, lakini umesoma hiyo habari, familia imesema kuwa wathibitishe au ndio watashtakiwa kwani hilo gazeti halijathibitisha limedai tuu, hebu watanzania tuhoji vitu in logic badala ya kusukumwa na ujauzito wa mawazo kwenye mibongo yetu migando

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 08, 2012

    jmani mi naogopa hii Tanzania ya kwetu.. kusema ukweli hofu imenishika jana nimeota tumepatwa na political instability hali ni chafu mi naanza kuogopa sasa,,, hayo maudini watu wanayoyachochea wanadhani watafika nayo wapi hata wao watakufa tuu pamoja na ndugu zao.. kama mtu hauko competant ofisini kimawzo kiakili na kielimu eti unakimbilia udini.. matokeo yake tuinapachikana watu ambao ni ooooovyo !!!!!!!! i hate this smell of udini unanchefua ulieanzisha storry ya udini umeacha kuwaza ya msingi ya kuleta amani unawaza udini huna jipya1think positive

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 09, 2012

    Udini upo, na Chadema wamehusikaje wao ndio walioanza kutumia majukwa ya kidini na ya kikabila, na wao ndio wanaochochea udini na ukabila na wao ndio wenye kuandika magazeti ya uzushi na uchochezi, na tusiende mbali juzi juzi tu Rais alivyoteua tume ya katiba wa kwanza muasisi wao Mzee Mtei kusema waislam wengi katika tume, kishindo juzi mbunge wao Nassari katamka hadharani kuwa wao wengependa kanda ya kaskazini, kilimanjaro, arusha na manyara wajitenge, hawa si watu wajinga au wanachama wa kawaida ndani ya chama kwa hiyo wanajua sera na madhumuni ya chama chao, sasa kama mtei yeye ndio muasisi unafikri malengo yake yalikuwa nini, na hali ya chama inajieleza, mgawanyo wamadaraka ndani ya chama, nguvu yao wanailekeza ukanda huo ambao wamedhamiria iwe nchi huru, naona makao makuu yatakuwa arusha. Wameivuruga Arusha hadi sasa idadi ya utalii imepungua na arusha inaandikwa kwenye vitabu vya utalii ulaya kuwa ni sehemu ya kutembelea kwa tahadhari. Unatuambia udini hukuna upo, wakati wa uchaguzi mgombea wao kasafishwa na kanisa ilhali kaenda kimyume na maadili ya dini yoyote ile, sasa mnataka mpaka watu wachomane moto ndio mmjue kama kunaudini? Ukweli ndio huo na ili kupingana nao ni lazima tukabali upo na tuepukane na makundi na vyama vinavyochochea mambo hayo
    Na wewe unayesema kuwa Rais kajitakia mwenyewe amejifanyisha kuwa tamabara la deki, na kuwa uswahili wake umempoza, ni kweli maana sisi waswahili tuna methali isemayo “MBWA UKICHEKA NAYE ATAKUFUATA MPAKA MSIKITINI”. Haya ndio makosa yake!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 05, 2012

    mimi sijataka kuingia katika majadiliano haya, lakini ningependa kushauri, watu wengi wanazungumzia udini, lakini hamna hata mmoja aliyekaa akasema tukae tuongee tujadiliane kuhusu suala hili la udi, nafikiri ingekuwa busara zaidi kama watu wangekaa pamoja wakaulizana kwanini mnasema kuna udini, tupeni sababu za huu udini, na wale wanaokataa kama hamna udini na wao watoe sababu zao kwanini hamna udini, natumai kwamba kila mmoja ana sababu zake za kusema kwanini kuna udini na kwa nini hakuna udini. Mzee mtei katoa mfano wa nini udini kwa mawazo yake binafsi, na wengine watoe mawazo yao kwa nini kuna udini, halafu sisi kama watu wastaarabu tukae tuone kama kweli upo au haupo halafu tuchukuwe maamuzi ya pamoja kuondowa malalamiko, au kuyakataa kwa sababu za msingi.
    leo kuna gazeti limeandika baraza la mitihani limebadilisha matokeo ya mtihani kimya kimya naona tuisome habari hii halafu tuone kuna nini ndani yake.

    halafu kitu kingine acheni kututukana sisi waswahili kwa sababu ndani ya nchi hii kuna waswahili ambao ni wastaarabu ambao wajerumani walikuwa wakiwalipisha kodi kubwa. na pia kuna kundi la washenzi ambao walikuwa wakilipa kodi ndogo, lakini leo washenzi ukiwaita washenzi wanasema wametukanwa, kumbe wao ni washenzi kweli na neno hili sasa hivi linaonekana kama tusu kumbe ni kundi la watu katika tanzania hii.

    mimi sina zaidi wakati hauniruhusu ya kuandika ni mengi sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...