BARAZA la Mtihani la Tanzania (Necta), limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha sita iliyofanyika Februari mwaka huu yakionyesha kuongezeka kidogo kwa kiwango cha ufaulu kwa ujumla huku wavulana waliofaulu wakiwaacha mbali wasichana.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), Dk Joyce Ndalichako (pichani), kati ya watahiniwa 46,499 waliofanya mtihani huo, wavulana waliofaulu ni 30,466 wakati wasichana ni 16,033. Hata hivyo, kumekuwa na mchuano mkali katika ufaulu kwa asilimia ambao wasichana walipata 87.37 na wavulana 87.69.

Sekondari ya Wasichana ya Marian, Bagamoyo ndiyo iliyoongoza kitaifa na mwanafunzi wake, Faith Assenga ndiye aliyeshika namba moja katika masomo ya Sayansi.

“Katika masomo ya Biashara, aliyeshika nafasi ya kwanza ni Alex Isdor wa Sekondari ya Kibaha na Lugha ni Faridi Abdallah wa Sekondari ya Mpwapwa,” alisema Dk Ndalichako.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 02, 2012

    Kuna shule fulani fulani walimu wao walikuwa wananunua mitihani kisha kuwafundisha wanafunzi wao, sasa hali imekuwa ngumu kidogo ndio maana shule za serikali zimeongoza --- Watu bwana hamuachi!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 02, 2012

    Pia, hawajaweza kudhibiti uvujaji wa mitihani! Kuanzia, baraza, kwny misafara na vituo vya mitihani. Mitihani bado inavuja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...