Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanahabari wakati wa kutangaza Baraza la Mawaziri,Ikulu Jijini Dar es Salaam Jioni hii.


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Makamu wa Rais,Dkt Mohamed Gharib Bilali na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda muda mfupi baada ya kutangaza Baraza la Mawaziri leo.


Wanahabari wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kutangaza Baraza la Mawaziri leo 
MAWAZIRI HAWA WATAAPISHWA JUMATATU MEI 7, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2012

    Hongera Mhe Rais. Sasa tuwape nafasi mawaziri wafanye kazi kwa kuwasaidia na kuwaunga mkono kwa jitihada zao.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2012

    Mawaziri na manaibu wao, wakurugenzi na watendaji wengine waliowajibishwa kwa kuenguliwa ni sawa kwa upande mmoja mdogo, lakini viongozi hao kuchukuliwa hatua stahiki ndio lililo la msingi zaidi.

    Walio jilimbikizia mali za umma, mali hizo zitaifishwe na wao wafikishwe mahakamani kwa mujibu wa sheria.

    Kibanga Msese

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2012

    Baraza la mawaziri bila WAZIRI MKUU?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2012

    Haya haya, ongera sana Dr. Mwakyembe imarisha reli na anga. Mafisadi wanaotela maroli na mabasi yao kuwaumiza wananchi waipate vizuri

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2012

    Sasa mtukufu rais tueleze jinsi utakavyo wakaanga kina Maige Mkullo Nundu na wenzake. Nchi ya Tz si ina sheria. Ngoja tuone maana wasipochukuliwa hatua hata hao waliopo wataiba tena ili mladi hawa fungwi. Sasa jumba la dollar 700,000 itakuaje? Ama ata mwuzia fisadi mwingine
    Mimi napendekeza litaifishwe liwe kituo cha kutunza watoto wa mitaani.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 04, 2012

    Pongezi kwa Rais kwa Timu Nzuri. Tunawatakia kila la kheri, na tunawaomba muweke maslahi ya taifa na wananchi mbele! Pia tunaomba waliotajwa kufanya ubadhirifu wachukuliwe hatua kali za kisheria haraka sana ikiwemo kutaifishwa mali zao.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 04, 2012

    Suluhisho siyo kuwajibika kwa kuwastaafisha mawaziri bali ni kuwafungulia mastaka na kutaifisha mali za Mawaziri walio tumia madara yao vibaya ili iwe fundisho kwa hao wanaoingia madarakani sasa vinginevyo tatizo lipo pale pale.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 04, 2012

    Nimeridhika na kuondoka kwa Ngeleja na Mkulo...basi...hao wengine sijali sana...Asanteni....!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 04, 2012

    Mbona kuna watu hawatoki huko serikaliwni miaka yote kwani hakuna watanzania wengine wenye uwezo wa kuongoza !!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 04, 2012

    mawaziri 55, bado kuna wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi wa halmashauri ......list ni ndefu, ndo maana maendeleo yanachelewa fedha zote zinaliwa na watawala!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 04, 2012

    Waheshimiwa nawapongeza mpeni rais wetu ushirikiano tujenge taifa letu.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 04, 2012

    Haya mambo ya siasa bwana...ndiyo maana JK juzi wenye hotuba yake ya Mei Mosi alisema ukiwa Kiongozi lazima uwe na ngozi nene.Nawapongeza wote waliorudi kwenye nafasi zao,waliohamishwa wizara na wateule wapya.

    David V

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 04, 2012

    Karibuni kwenye viti vilivyowekwa makaa ya moto.

    Jitahidini sana lakini siku hizi wananchi wako macho.

    JK nakupongeza kwa kuwawajibisha wote na siyo mawaziri peke yao. Labda majungu yatapungua kidogo.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 04, 2012

    hivi watanzania tunachezea nchi ama?maana tulikua wapi tukachagua mawaziri wabovu ambao utendaji kazi wao sio mzuri, tunasubiri mpaka mambo yaaribike ndipo tuone umuhumu wa kubadilisha viongozi, je hao tunawaweka nao wapo salama ama mambo yale yale?????Ni vema kuondoa uongozi mbovu ila kama miaka mitatu minne ya uongozi akuna kilichofanyika tena ni uongozi wa juu kabisa "WAZIRI", sasa sijui maendeleo tunayotaka tutafikia malengo, tuendelee kujifunza kutoka kwa wenzetu...

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 04, 2012

    OMBI OMBI KWA MH. RAIS! CHONDE CHONDE NI NANI MWENYE NAMBA YA SIMU YA RAIS NIONGEE NAYE;
    ASIJE AKAWARUDISHA HAO MAFISADI KWENYE NGAZI YOYOTE YA SERIKALI. ITAKUWA FUNDISHO KWA WENGINE.HATA KAMA WAKO AMBAO HAWAKUHUSIKA BASI WASWAHILI TWASEMA "SAMAKI MMOJA AKIOZA......."
    YAANA WAFUTIWE KAZI NA UTUMISHI KABISA WALISHAVUNA VYAKUTOSHA.
    MICHUZI POST HII NOTE LABDA ITASAIDIA JAMII.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 04, 2012

    mama na mwana hongereni!!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 04, 2012

    Hapo sawa. Je yale majizi yatafanywaje? Muhimu ni mali walizoiba.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 04, 2012

    MICHUZI NINAFURAHIA KWELI HII BLOG YETU YA JAMII YAANI WANACHAMA WOTE WALIOCHANGIA HII MADA YA BALAZA JIPYA LA MAWAZIRI WAMESAHAU HISTORIA YA TANZANIA? KUNA MAMBO MATATU KWANZA 1. MTUKUFU RAIS KAMA WALIYO MTANGULIA AMEZIBA BAADHI YA VIDONDA KWA KUTOA BANDAGE YA MGONJWA HUYU NA KUWEKA KWA MGONJWA YULE I MEAN RESHUFFLE. PILI 2. HISTORIA INATUFUNDISHA UKIIBS KIJINGAJINGA UNAPOTEZA TU KIBARUA CHAKO SASA UKIWA MJANJA IBA PESA YA UHAKIKA SIYO TU DOLLAR LAKI MOJA CHOTA ZA KUTOSHA HAPA SITOI MIFANO YA MAJINA MNAWSJUA WENYEWE WALIOCHOTA MPAKA PESA ZINADONDOKA. TATU 3. HISTIRIA YA TANZANIA KAMA VIONGOZI WAKUU WA NCHI WALIO TANGULIA INATUFUNDISHA UKIIBA UKAKAMATWA HUFIKISHWI MAHAKAMANI HATA KAMA KUNA USHAHIDI LUKUKU UNAPEWA LIKIZO YA MILELE UKAZITAFUNE VIZURI HIZO PESA ZA WALIPA KODI KAMA NI HUMU HUMU NCHINI AMA NJE YA NCHI. SASA BASI KWA KIFUPI NAWAPONGEZENI SANA MLIOFANIKIWA KUCHOTA MPAKA ZIKAMWAGIKA MTAISHI VIZURI RAHA MSTAREHE WENZANGU MLIO JARIBU KUCHOTA KIDOGO HAZIKUJAA BASI POLENI SANA. MMECHEZEA SHILINGI CHOONI HAMKUITUMIA VIZURI HILI SHAMBA LISILO NA MWENYEWE LIITWALO TANZANIA MAMA HURUMA. MWENYE MASIKIO WATAKUWA WAMENIELEWA NA WASIO NA MASIKIO WAULIZE WENYE MASIKIO WATAWAELEZA HUU UJUMBE WANGU. ASANTENI

    ReplyDelete
  19. MDAU WA DC,ZEE LA NYETI.May 04, 2012

    Hapo ni sawa na kutoa chungwa na kuingiza limao.Tatizo letu sio waziri,naibu waziri peke yao,tatizo ni kurundikiwa masuala mengi na nyeti chini ya mtu mmoja.Mfano Waziri wa Nishati na madini yote kwa Tanzania.Mifumo yetu inahitaji kufumuliwa na kuundwa upya.

    Mdau wa DC.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 04, 2012

    government of the new people, new style, old dances.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 05, 2012

    Mawaziri na manaibu jumla ni 55,.nadhani iko haja katiba mpya iwe na limit yao..ninapendekeza katiba mpya iandikwe kuwa jumla ya mawaziri na manaibu wao isizidi 30..uchumi wetu hauwezi ku-support mawaziri 55,bado wakuu wa mikoa,wilaya n.k.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 05, 2012

    Actually ninachoharibu serikali ni wanasiasa wa vyama vya upinzani walioko katika vyeo vya serikali. Taratibu za siasa ni kwamba huwezi kuleta siasa maofisi ya serikali. Wanaoiba sio mawaziri. Baba zenu na kaka zenu ambao wapo miaka nenda rudi pale nafasi za serikali na walizowaridhisha watoto wao au tuwataje mjue kwamba serikali kuna udugunization. Akiwa mtu wa kabila moja au ukoo mmoja basi ndugu zake mpaka mfagiaji ofisini atakuwa ndugu yake. Hicho ndicho kilichotokea na kinachoendelea mpaka leo. Huwezi kupata kazi kama huna ndugu yako akakuunganisha. Mtu afanya utafiti ya Masters juu ya udugunization katika maofisi ya serikali. Hao wanaopiga makelele humu globuni ni watoto na ndugu wa hao hao. Akina pangu pakavu mtu amegraduate mwaka juzi anabidi aombe kazi Usalama wa taifa au jeshini.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 05, 2012

    Wembe ni ule ule tuu.
    CCM ni wezi tuu! Hakuna jipya.
    Kilichobaki ni kuwaondoa madarakani tuwafunge, kwisha mchezo.

    Swali la kizushi, kwa nini Michuzi blog mnapenda kuweka Dkt mbele ya jina la Mheshimiwa Raisi Kikwete, yaani hata taarifa rasmi kutoka ikulu huwa haifanyi hivyo ila ni nyinyi tuu, najua mnapenda kumfagilia raisi, lakini kumuandika kama Dkt.Kikwete...
    Ni kwa nini?

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 08, 2012

    the reign of hypocrtes is about to end, therefore, let those who are clean and loyal patrictics to serve this nation work valiantly to restore our national pride as the country of peace, tranguility and true Brotherhood.
    Diplomat

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...