THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Balozi Seif Ali Iddi akutana na Mwakilishi wa Taasisi huduma za Teknolojia ya Afya Nchini Marekani ya Med International

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mwakilishi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi inayojihusisha na huduma za Teknolojia ya Afya ya Chuo Kikuu cha Brown Mjini Boston Nchini Marekani Bw. Jayson Marwaha hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.Kati kati ni Mkurugenzi Mwenza wa Taasisi hiyo ya Med Intarenational Bwana Han Sheng Chia.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mwakilishi wa Taasisi inayojihusisha na huduma za Teknolojia ya Afya Nchini Marekani ya Med International Bwana Jayson Marwaha ambaye wapo Nchini kufanya utafiti wa Afya kwa Hospitali za Zanzibar. Hatua hii ni utekelezaji wa ahadi waliyompa Balozi Seif wakati walipokutana nao Nchini Marekani Mwezi Oktoba Mwaka jana.Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Dr. Sira Ubwa Mwamboya.