Wakati Bunge liko kwenye mchakato wa Bajeti ya 2012/13, yameanza kujitokeza maneno na taarifa mbalimbali juu ya kupanda kwa mishahara ya watumishi wa Umma wakiwemo Wabunge. Mathalani, siku ya Jumatano tarehe 20 Juni 2012, gazeti moja linatokalo kila siku lilikuwa na habari yenye kichwa kisemacho “Mishahara ya Wabunge juu”.


 Ofisi ya Bunge imeona ni vyema kutoa ufafanuzi juu ya suala zima la mishahara ya Wabunge ili umma uweze kuelimika ipasavyo juu ya taratibu zinazotawala jambo hili kama ifuatavyo:

 ·         Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ambayo inajumuisha Fungu Na. 42 lenye Bajeti ya Bunge bado haijasomwa Bungeni, na hivyo haiwezekani leo hii kueleza kuwa kuna nyongeza ya bajeti inayohusu mishahara kwa Wabunge.
·         Si kweli kwamba mishahara ya Wabunge imeongezwa toka kiwango wanacholipwa sasa, kwa kuwa mishahara yao kama ilivyo ya watumishi wote wa umma, hurekebishwa kwa waraka maalum  toka Ofisi ya Rais,  na si Kamisheni au Kamati yoyote ya Bunge.
 ·         Waraka wa mwisho wa toka Ofisi ya Rais unaotoa Masharti ya Kazi ya Mbunge ulitolewa tarehe 25 Oktoba 2010, na kueleza kuwa Mbunge atalipwa mshahara katika ngazi ya LSS (P) 2, na ni waraka huo unaotumika mpaka sasa. 
 ·         Mapendekezo ya ongezeko la 32% ya Bajeti ya Ofisi ya Bunge yaliyooneshwa kwenye kitabu cha Bajeti namba 2, cha matumizi ya kawaida yaliyowasilishwa mezani ni ya matumizi mengine ambayo hayana uhusiano na ongezeko la mishahara.

 Mwisho, Ofisi ya Bunge wakati wote inathamini sana mchango wa vyombo vya habari katika juhudi za kuelimisha umma juu ya kazi za chombo chao cha uwakilishi. Hata hivyo, Ofisi inasikitishwa sana na habari za upotoshaji zinazotolewa kwa lengo la kujenga chuki kati ya Wabunge na watu wanao wawakilisha.
Kwa mantiki hiyo, tunazidi kuwasihi Waandishi waandike habari au makala baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusu jambo husika na pale inapobidi waweze kupata ufafanuzi toka Idara husika katika Ofisi ya Bunge, ili kuepuka kuupotosha umma.
  
Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 941, DODOMA.
21 Juni 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2012

    Imekuwa vema kuwa ofisi husika imeandika kukanusha uvumi ulioandikwa katika gazeti moja la kiswahili la hapa nchini.

    Tatizo linakuja pale ambapo wananchi wamekuwa wakidanganywa: Mfano halisi ni ule uliozua mjadala juu ya posho za hao hao wabunge mwaka jana. baadhi ya viongozi wa juu wa bunge walikanusha kuwa hakukuwa na ongezeko la posho. Hata hivyo kadri muda ulivyopita ikajadhihirika kuwa wabunge walikuwa wameongezewa posho.

    Hili kanusho la ongezeko la mishahara kwa waheshimiwa wabunge bado ni la kutiliwa shaka kwa sababu zilizoelezwa hapo juu. Inatuwia vigumu sana sisi wananchi kutambua tawaamini katika lipi na lipi tusiwaamini.

    Hebu tuhakikishieni ukweli ni upi katika hili. Waalimu wanadai haki zao, nao madaktari hawajatimiziwa haja zao, kisha nyie mnajiongezea mishahara eti kwa vigezo kuwa wabunge wenzenu wa mabunge ya nchi jirani wana vipato vikubwa!!!

    Khaaaa!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 22, 2012

    Sound ka kawa. Mnaposema matumizi mengine mi nilidhania mtafafanua! Kha!Plus nyie mmeongelea band ya LSS(P)2 hamjaongelea kiwango cha hiyo band. Tuko macho haibiwi mtu hapa!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...