Mratibu wa mabalozi wa kampeni ya uchangiaji katika ujenzi wa mabweni Rebeca Gyumi ambaye ni pia ni mtangazaji wa kipindi cha fema akielezea jinsi walivyojipanga kuhakikisha wanachangisha fedha za kutosha ili lengo la TEA likamilike.
Mabalozi wa kampeni ya TEA katika ujenzi wa hosteli wakiwaomba wananchi kushiriki kampeni hii kwa kuchangia kwa kutuma ujumbe CHANGIA TOFALI kwenda kwenye namba 15564. Katikati ni Mkurugenzi wa uhamasishaji wa TEA Seif Mohamed.
Mkurugenzi wa uhamasishaji wa Taasisi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Seif Mohamed akiielezea kampeni ya kuchangia ujenzi wa hosteli 30 zitakazowahudumia wanafunzi wa kike wa sekondari 1,504 nchini katika mikoa nane huku mabalozi wa kampeni hiyo wakifuatilia mazungumzo hayo kwa umakini katika uzinduzi wa muungano wa TEA na Mabalozi hao uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini DSM.
Jokate Mwegelo (kulia) akielezea imani yake kwa watanzania na kuwaomba raia wanaoiombea mema nchi yetu kuguswa kama walivyoguswa wao kujituma katika kuchangia kampeni hii ambapo ujumbe mmoja wa CHANGIA TOFALI ni shilingi 250/=, Kushoto kwake ni Mwanablog maarufu na mwanamitindo Mariam Ndaba
Mabalozi wa kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni katika picha ya pamoja, kutoka kushoto ni Nancy Sumari (Miss Tanzania 2005) Rebeca Gyumi(Mtangazaji wa kipindi cha FEMA), Mariam Ndaba(Mwana mitindo na mmiliki wa blog) Jokate Mwegelo(Mshindi wa pili Miss Tanzania 2006) na asiyekuwepo ni Faraja Nyalandu (Miss Tanzania 2004) ambaye alikuwa na udhulu na atakuwepo katika kampeni zinazoendelea.

Kikundi cha wasichana maarufu watano katika nyanja mbalimbali nchini wameungana kwa pamoja na kuamua kwa hiari kuunga mkono jitihada za Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) za kutafuta kiasi cha shilingi za kitanzania billion 2.3 zitakazotumika kujenga hosteli 30 ambazo zitahudumia wasichana wa shule za sekondari 1,504.

Kikundi hicho cha mabalozi wa kampeni hii kinaundwa na Rebeca Gyumi(Mtangazaji wa kipindi cha FEMA) Faraja Nyalandu (Miss Tanzania 2004), Nancy Sumari (Miss Tanzania 2005) Jokate Mwegelo(Mshindi wa pili Miss Tanzania 2006) na Mariam Ndaba(Mwana mitindo na mmiliki wa blog) kiliguswa kwa namna ya kipekee na na jitihada za TEA na hivyo wakaamua kwa hiari kuungana na TEA katika kuhamasisha watu kujitokeza na kuchangia kampeni hii.

Lengo la Mabalozi hawa ni kuhamasisha uchangiaji na kuwezesha kujenga zaidi ya hosteli 5 kati ya 30 ambazo TEA imepanga kujenga.

Katika Uzinduzi huo uliofanyika Tarehe 31/07/2012 katika hoteli ya Serena Jijini DSM kati ya mabalozi hao na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ambapo ni Faraja Nyarandu pekee ndie alikosekana kutokana na kubanwa na majukumu mengine lakini alithibitisha uwepo wake katika kampeni zinazoendelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

 1. AnonymousJuly 31, 2012

  Na wewe Jokate umeanza kujichubua, acheni hizo nyie watoto wa mjini

  ReplyDelete
 2. Anon hapo juu yaani namie nilikua najiuliza kama Jokate anajichubua?!!!

  ReplyDelete
 3. Big up girls.Ni wakati muafaka wa kuchange wabongo ili kuchangia maendeleo kwani utamaduni wetu ni wa kuchangia Arusi tu.kwa kweli kwa Arusi michango haichukui sekunde.I like that

  ReplyDelete
 4. anonymous 1 una mtazamo kama wangu, aliyewadanganya weupe ndiyo urembo ni nani jamani.

  ReplyDelete
 5. umeona mkorogo umekoleaje??!!! mfuuuuu hii haina wasomi wala wasiosoma.

  ReplyDelete
 6. hahah...mdau hapo juu umeniwahi, mtoto jokate ndio anapotea hivyo daaah yani fuluuu kujichubua

  ReplyDelete
 7. NANCY MISS TANZANIA. HAO ND'O WALIMBWENDE WANAOJIHESHIMU SIYO WAZARAMO WAZARAMO AKINA NANI SIJUI, KILA SIKU KWENYE MAGAZETI UCHWARA. NICE TO SEE YOU. WEWE NDIYE MISS WA KWELIIII. EMILY ADOLF NAYE YUPO WAPI SIJUI. HUNA MAKUU BALI VITU VYAKO VIKUU. KUSOMA NA KULELEWA VYEMA NA NI MFANO WA KUIGWA.

  ReplyDelete

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...