Na Shiffie Dauda


Akiwa ndio mchezaji aliyesajiliwa kwa fedha ndefu kutoka nchini Tanzania, Mbwana Ally Samatta anaishi ambayo mcheza soka wa kimataifa anastahili kuishi.


Akiwa ameuzwa kwa dola za kimarekani zaidi ya 100,000, kwenda TP Mazembe kutoka Simba, Mbwana Samatta analipwa kiasi cha dola 5000 kwa mwezi ambayo ni sawa na shilingi millioni 7.5 huku akichukua marupurupu ya kutosha.

Mbwana Samatta amekuwa akicheza na kuperfom kwa kiwango kikubwa katika kila nafasi anayopata anapoichezea klabu yake na kwa kiwango alichoonyesha kuna uwezekano mkubwa mkataba wake utaboreshwa zaidi na kuendelea kuvuna mkwanja mrefu zaidi.



Kwa sasa hivi Samatta amenunua gari la kisasa zaidi Chrysler Crossfire la mwaka 2006 ambalo limemgharimu takribani millioni 50 za kibongo.

Ikiwa Samatta ataendelea kucheza kiwango alichonacho sasa, basi ni dhahiri tutaendelea kuona akiishi kwenye majumba ya kifahari huku akipush magari ya gharama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Hongera zake,ila akumbuke kuwekeza kwa ajili ya baadae. Maisha sio magari tu,fainali uzeeni.

    ReplyDelete
  2. Na wengine zaidi watoto wa Tanzania wafikie ktk kiwango hicho pia.

    Inshallah, Mwenyezi Mungu kufungulie zaidi kijana!

    ReplyDelete
  3. Dola 5000 kwa mwezi ni mshahara safi sana, lakini kama vijana hawa wacheza mpira kwa majalio waliyozaliwa nayo, agents wao wajaribu kuwatafutia kazi kama hapa Ukerewe. Wenzao walipwa paundi mia-u-ishreen elfu kwa wiki

    ReplyDelete
  4. mwandishi,tumuombee kila la kheri, Ila tu naomba nikushauri kwamba, sifa kama hizi ulizozitaja za kuishi kwenye majumba ya kifahari na kupushi magari ya gharama -ni sifa za mbio za panya,kiufupi haziendani na maadili ya kuishi chini ya jua.Mwandishi unatakiwa uwe makini kwa kutoa maneno nasaha yenye ushauri na hekima na siyo maneno yenye kushinikiza tamaa,ufahari na ulevi wa pesa. Ni vyema ukamshauri aishi maisha ya kawaida na na awekeshe mali yake kwa ajili ya siku za uzeeni.Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  5. Zebedayo kwa Mara ya kwanza umeongea la Maana ni kweli anatakiwa kuweka maisha yake vizuri hasa na familia isije kutokea yale ya mchezaj iwa Simba elimu ni muhimu ya kujipanga vizuri mungu amlinde na akae na mali vizuri.

    ReplyDelete
  6. Jamani mshaurini awekeze hivyo "vijisenti" kwa sababu hutacheza mpira hadi uzeeni. Ukifikisha miaka 30 huwezi tena endelea kucheza kwa hiwango cha sasa. Nenda nyumbani na uwekeze kwenye mambo yatayokuwa yanakutengenezea hela hata baada ya kuacha kucheza mpira.

    ReplyDelete
  7. Zebedayo leo umeongea... siyo kuponda tu... hapo sawa... Mwenzako Peter Nalitolela yuko wapi ama umebadili jina?

    ReplyDelete
  8. wakumbukwe wakina jella mtagwa wakufa wanaishi mabondeni, mazense, kijana uza mtengu huo kajenge kwenu mbagalla mapema

    ReplyDelete
  9. hiyo gari ya 2006 kwa dola$30.000 ni huongo mtupu hiyo gari ni dola 5.000 sawa na shl 12.000 ach kuchalulua watu hapa

    ReplyDelete
  10. Wabongo mna dongge mtakufa maskini jeuri

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...