Katibu mkuu wa Chama chama cha Demokrasi na Maendeleo Dkt Wilbrord Slaa akihutubia wananchi wa Manispaa ya Morogoro katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Ndege mkoani Morogoro. 
 Katibu mkuu wa Chama chama cha Demokrasi na Maendeleo Dkt Wilbrord Slaa akiongoza umati  uliohudhuria mkutano wa hadhara wa Operesheni Sangara-Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) baada ya mtu mmoja kudaiwa kupigwa risasi na kufariki dunia wakati wengine wawili nao wakidaiwa kujeruhiwa kwa kupigwa na risasi na askari wa jeshi la polisi.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 5 asubuhi eneo la Msamvu barabara kuu Dar es Salaam-Morogoro wakati askari hao wakiwatawanya umati mkubwa wa wanachama na wafuasi wa chama hicho waliokuwa wakisubiri viongozi wa juu wa chama hicho ili waandamane kuelekea katika mkutano wa hadhara uwanja wa Ndege mkoani Morogoro leo.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Morogoro na vitongoji vyake, katika mkutano wa hadhara wa operesheni sanga ,kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Uwanja wa Ndege
 Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Morogoro waliojitokeza katika mkutano huo. 
 Makamu Mwenyekiti Chadema Zanzibar Said Issa Mohamed akifafanua jambo kwa wananchi hao.
  Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Igunda kupitia Chadema, Joseph Kashinde akizungumza na wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
 Mbunge wa viti Maalum Chadema akimwaga sera za chama hicho.
 Mbunge wa jimbo la Ubungo Jijini Dar es Salaam John Mnyika akipanda jukwaani wakati akiwasili katika uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.
Sehemu ya umati ambao ni wakazi wa Manispaa ya Morogoro na vitongoji vyake katika mkutano huo. Picha Zote na Juma Mtanda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Kwa utaratibu huu, sasa nitaanza kutembelea tovuti hii mara kwa mara, ngoja niwatumie rafiki zangu kama kumi hivi.

    Tunahitaji mabadiliko, tena tunayahitaji sasa

    ReplyDelete
  2. Ankal Hongera sana naona umeanza kutewatendea haki wapinzani wa ccm.
    Naona M4C imekufikia na umeikubali.

    ReplyDelete
  3. Mikutano ya hadhara kula kukucha maendeleo yatakuja saa ngani uchaguzi umeshakwisha kampeni zimeshafungwa serikali ipo madarakani fanyeni kazi mjitafutie maendeleo sio kungoja wanasiasa hawa wote ni waongo ni CCM wala CHADEMA watakaowaletea maendeleo maendeleo huja kwa kujituma mtu binafsi.

    ReplyDelete
  4. It looks like change is coming to Tanzania. Obama once said: "change has come to America"

    ReplyDelete
  5. Mhhh, naona hapa wazungumzaji ni wale wa Magwanda Mikono Mirefu - wa Mikono Mifupi wapo wapi??

    ReplyDelete
  6. Wapeni watu kazi acheni maneno!

    ReplyDelete
  7. sasa nitatembelea hii web ya ankal, na nitawajulisha na wengine kuwa Ankal amebadilika sasa.
    nakuhakikishia ile idadi ya milioni moja utaanza tena kuipata kama utatenda haki kma hivi.

    ReplyDelete
  8. Africa haiwezi kuendelea hata siku moja badala ya watu kufanya kazi wanaenda kusikiliza mambo ambayo hayana mbele wala nyuma..porojo tu. M4C then what? Maendeleo yatakuja kwa mtu mojamoja kufanya kazi siyo wanasiasa. Kama serikali imeziba opportunities ya wewe kufanya kazi basi ni jambo la kuungana siku moja na kudai then back to work...

    ReplyDelete
  9. KWELI KAMA UNATAKA KWENDA PEPONI....WAUE WANASIASA WATANO......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...